Asante sana mtoa mada, pia
FirstLady1 nashukuru sana na ubarikiwe mno kwa haya.
Kipipi nakushukuru sana kwa kuniita ili na mimi nitie langu japo dogo lakin litaongeza maarifa.
Kwanza kabisa ikumbukwe kuwa ndoa ni sehem ya ibada ambayo mtu anaweza kuitimiza akiwa hapa dunian. Tena Mungu aliiweka hii ndoa kuwa kitu kitakatifu sana ambacho kwa mapenzi yake mema alifanya ndoa kuwa chombo cha kufanya kazi ya uumbaji. Nafikiri kama watu wote wangepata kujua kuwa ndoa kama ilivyo Mungu kaifanya kuwakilisha utukufu wa Mungu duniani kwa kuruhusu tendo la ndoa kutumika kuumba kama alivyoumba yeye.
Sasa kwa kuyajua hayo yampasa mwanamke kuwa mwenye upole na upendo, anayeamka asubuhi kabla hakuja pambazuka na kuanza kuzipanga kazi za nyumbani kwake. Awe ni mtu anayelisha watu wake bila kunung'unika, awe ni mtu anayewavesha watu nyumbani kwakei. awe hodari katika kazi zote za mikono na apende kumtunza mumewe kwa uaminifu na mumewe huyu ajulikane aketipo barazani na wenzie. awe ni mtu mtu ambaye moyo wa mumewe humwamini na kamwe hatakosa mapato ya mikono yake.
BABA yampasa kuwa mtu anayeipenda familia yake, awe tayari kuihudumia pasipo kuchoka, apende kuona watu wa nyumbani kwake wanafuraha na amani muda wote. Tena asiwe mlevi, wa mtu wa kuhadaiwa na mwanamke malaya, atamani sikuzote kuona mkewe na watoto wanastawi.
MziziMkavu Asprin,
Nyaningabu,
Mr Rocky nk mnayatimiza hayo kwa familia zenu? mko responsible juu ya wake na watoto wenu wanakula nini wana lala wapi na wanaish vipi? hizi ndizo quality za baba bora. jitahmin mtuambie kama ninyi ni akina baba bora au ni bora baba. Tena mtuletee jibu hapa.
Tena ikumbukwe upendeleo hudanganya kuwaandalia watu wa nyumbani kwake