Hili ndio tatizo lako dearest mambo ya moyo hayaendani na logic follow your heart stop using your head in matters of love.Mmh na kama mimi sio princess wako je??
Hili ndio tatizo lako dearest mambo ya moyo hayaendani na logic follow your heart stop using your head in matters of love.
Ohoo nisitumie kichwa alafu nikiumizwa nikiadhibu kwa kukigonga ukutani?Gd nite dearest!MWUAAAHHH!
unaweza ukatongoza kumbe njemba mwenzako.. Lol!
Lazima watu waogope.
napenda tu kuwachanganya ila nitaacha.
hawa my dear hauko mwenyewe.....nina kimeo kimoja....tangu niko form 3,kaoa na ana watoto lakini bado tu anataka kuonja....kila mara ananiapia...hata kama tukiwa wazee ipo siku tu tutajuwa pamoja......its insane.....siwapendi mimi ving'ang'anizi......
Kwa wadada wenzangu....wanasema experience is the best teacher....leo tu share experience na tupeane ushauri......
Wengi wetu tutakuwa tumekutana na wanaume ambao mimi ninawaita wanaume malengo ya mbele na wanaume waharakisha mambo na wanaume maneno.....
Mwanaume ya malengo mbele ni Yule ambaye kupitia maneno yake anakujengea picha ya baadaye ili apate mahitaji yake ya sasa.Yeye anakujengea picha ya nyie mkiwa na familia yenu,watoto,ndoa nzuri,mkienda matembezi pamoja mwisho wa mwaka nk....hii yote ni ili kukujengea picha kuwa wewe ni sehemu ya maisha yake na kwamba kila analoliwaza analiwaza kulifanya akiwa na wewe siku za mbeleni.
Kwa furaha wanawake walio wengi huwapokea wanaume wa aina hii kwa mikono miwili na wengine wetu huenda hata kutoa sadaka maombi yetu yamejibiwa na kuanza kuwaweka maanani aina hii ya wanaume......
Wanaume waharakisha mambo ni wale ambao wana haraka sana utafikiri wanakimbizwa na moto...hawa ni wale unakutana nae na mara moja anahakikisha umekuwa nae karibu sana kwa wakati mfupi....anahakikisha huoni wala huzifahamu tabia zake chafu.hawa tofauti na wanaume malengo mbele,kwa muda mfupi sana wanahakikisha umewaweka kwenye akili yako,kila saa wanapiga simu,wanaandika message,wanataka kuwa pamoja nawe kila saa,wanakutambulisha kwa ndugu wale kama binamu,mpwa na si wazazi na marafiki zao,wanakupa funguo za nyumba zao na ujanja mwingine wa aina hiyo.
Hawa wanajenga hisia za msichana kwao haraka na wanataka muwe na uhusiano wa kimapenzi haraka.....
Kwa akilo ya kawaida utajiona hakuna kama wewe hapa duniani na una bahati sana,ila baada ya muda mfupi sana watakuliza vibaya walio wengi.
Wanaume maneno.....hawa ni wanaume wazuri sana kwenye kusema...yaani anaweza kuahidi kila awezacho na atakujengea mazingira ya kuamini anaweza kufanya hivyo....ila hawatekelezi na hawana uwezo huo wa kufanya hivyo ,na wengine hata kama wanao uwezo hawafikirii ndani ya roho zao kufanya hivyo,wanaahidi wapate wakitakacho........
Ushauri wangu sasa:
1.Wasichana tuwe makini na tuchukue muda kuwafahamu wanaume wanaokuja kutaka mahusiano na sisi....haraka haraka haina baraka.....mtu hata jina lako la pili halijui anakuahidi ndoa sijui nini....tuweni makini....there is no fire,you do not have to rush kutoa akili.moyo na mwili wako kwa mwanaume usiyemfahamu vizuri. Kile kipindi cha dating tukitumia vizuri kuwasoma na kuwafahamu wanaume...na si wakati wa dating umeshatoa mwili na akili yako na hata moyo wako.....open your ears and eyes and intelligency 100% and not your legs.
2.Tuache tabia ya kuamini ovyo,mtu anakuahidi hiki hafanyi,kile hafanyi....he does not keep promises....wewe nawe umo tu unaendelea nae ukiamini atabadilika au amesahau au unaogopa kumuuliza.....mtu anayekupenda atatenda lile alisemalo kwa wakati,na kama atashindwa utakuwa wa kwanza kujua sababu na zitaeleweka......tuwe wakali kidogo na tuhoji....unamuogopa oh,nikimuuliza ataniacha,kama ni wakukuacha atakuacha tu.
3.Tukubali kuwa tumedanganywa na tuwe wajasiri wa kusonga mbele.Mara kibao unasikia msichana anasema najua ananidanganya ila sasa nifanyeje ndo nimeshalala nae,nimezaa nae,siwezi muacha,tutabanana hapo hapo hadi anioe.....we si wa kwanza kudanganywa,kaa chini lia kama inakubidi,fikiria ulivyodanganywa na ukadanganyika na jifunze then tulia kwa muda na chukua uamuzi wa kuondoka kwenye utumwa wa kosa la kudanganyika then songa mbele kwa kujiamini,kuwa makini na kumuomba Mungu kwa sana.
Ni hayo tu,.....nawapenda wote na nawatakia wikiendi njema.
i think we ought to work together.....but if you do not keep promises, you dissapear and come back after sometime.....how am i suppose to work with you to build something out of the so called "LOVE?"
Hayo maneno huku juu mengine kweli mengine sio kweli,love is very complicated,unaweza kujikuta umependa tu ghafla na ukatupa kila kitu chako pembeni ukawa kama mgonjwa wa akili vile,wanaume wako kila style na nivigumu kuwafahamu,hapo maelezo yako bado hujamchambua mwanamme,umeeleza kwa ubaya tu ila wema hukuueleza,sas aushauri gani huo ulio utoa ?
Mimi experiance yangu naweza kusema mtu anaweza kukupenda just one day,inawezekana,na mtu huyo akawa ana nia safi kabisa,unajua wakati mwengine unaweza penda mtu hata jina usiulize ,,,na hata ukilijua basi hata la baba usilitambuee na unaweza ikapita miaka hamuja funga ndoa just relationship.
Dada nanona mawazo yako mgando kabisa...mi nawashauri ukipenda wala usisite ukitaka kumjua mtu dai cv tu,hahahaha
Michelle,
Asante kwa maelezo yako mazuri. Kwa upande wangu naona umezungumzia mapenzi ya wanawake wanaotafuta kupata kitu fulani kutoka kwa mwanaume na wala sio mapenzi. Kama unampenda mtu kutoka moyoni, hizo ahadi za vitu ni immaterial kabisa!!! Kwa mtindo wa kuhaidiwa vitu ndio umkubali mwanaume, then wewe mwenyewe unakuwa umejiingiza mtegoni na wala huna mapenzi na huyo mwanaume bali unachotaka na kufuata kwake ni hivyo alivyokuahidi. Kwa kuwa wanawake wengi sasa hivi hawana mapenzi ya kweli bali wanataka mali na vitu, then wanaume nao wanalazimika kudanganya ili kuwapata kiurahisi kwa kuwa wanajua wanawake wa sasa wanataka nini?
Hubiri mapenzi ya kweli!!!!
Tiba
Michelle,
Asante kwa maelezo yako mazuri. Kwa upande wangu naona umezungumzia mapenzi ya wanawake wanaotafuta kupata kitu fulani kutoka kwa mwanaume na wala sio mapenzi. Kama unampenda mtu kutoka moyoni, hizo ahadi za vitu ni immaterial kabisa!!! Kwa mtindo wa kuhaidiwa vitu ndio umkubali mwanaume, then wewe mwenyewe unakuwa umejiingiza mtegoni na wala huna mapenzi na huyo mwanaume bali unachotaka na kufuata kwake ni hivyo alivyokuahidi. Kwa kuwa wanawake wengi sasa hivi hawana mapenzi ya kweli bali wanataka mali na vitu, then wanaume nao wanalazimika kudanganya ili kuwapata kiurahisi kwa kuwa wanajua wanawake wa sasa wanataka nini?
Hubiri mapenzi ya kweli!!!!
Tiba
Mimi kwa upande wangu naona hizi sifa zipo kwa wanawake zaidi kwasababu;
1. Wanawake pengine ndio wanapenda sana kuharakisha suala la ndoa. Umekutana nae tu leo, kesho nataka kuolewa. So the best way ni kumfanya aamini na kumuwekea mazingira ya kuamini kwamba mtakua na famila nzuri, mtaenda kutembea n.k.
2. Pia ujue katika mahusiano wakati mwingine huwa inakua ngumu kuchukua muda mrefu kuchunguzana bila kujikuta mmeanguka katika mapenzi na hatimaye ngono )normaly chemistry goes fast that common sense in relationship). Unajua mapenzi yanapoanza kikubwa huwa ni kuvutiwa na mwenzio. Sasa kama mwenzio anakuahidi kila kitu ambacho ulikua unakitegemea kwa nini umhisi vibaya? Vipi kama wewe dada ndio umebadilika au baada ya muda imegundulika hauna vile vigezo vilivotarajiwa? Hapa utamlaumu mwanaume?
3. Huu ushauri umewalenga wanaume kwa kuona kwamba wanaume ni wadhalimu sana katika sauala zima la mepenzi, vipi kuhusu akina dada ambao nao hudanganya? Husema uongo na kupoteza muda, fedha na rasilimali za wanaume?
Anyway, it is difficult to strike a balance between men and women when it comes to relationship matters bse everyone sees it in a different angles and emotions normally override logic sometimes.
inabid tuanze kuita JF university ni zaid ya darasa