Kwa wadada zangu ambao waume zenu wakimya/wapole msiwafanye na kuwaona wajinga

Kwa wadada zangu ambao waume zenu wakimya/wapole msiwafanye na kuwaona wajinga

Raha ya mwanaume kuwa mkali, mcontrol mkeo. Na kuwa mtaratibu, mwenye hekima pia mahali panapohitajika. Lakini siyo unakuwa mpoleee, then una visasi vyako vya chini chini. ..Sasa hapo ndo kafanya Nini?. Upumbavu
 
Wewe ulitaka afanye nini?
 
Raha ya mwanaume kuwa mkali, mcontrol mkeo. Na kuwa mtaratibu, mwenye hekima pia mahali panapohitajika. Lakini siyo unakuwa mpoleee, then una visasi vyako vya chini chini. ..Sasa hapo ndo kafanya Nini?. Upumbavu
Hata siku moja hamna kisasi kizuri, kisasi mara zote lengo lake ni kuharibu na kukomoa.
 
Hii itamuukiza sana mkewe maana kama kuna mwanamke kapata mimba yy hajapata maana yake yeye ndo tatizo
 
Ogopa sana mtu anapokuwa na hasira mara nyingi huwa hana hekima na busara ktk maamuzi yake,huyo muuza duka kuumia kaumia kwani hamna mtu anayependa dada yake awe single mother, pili jamaa kishakuwa shemeji yake.

Halafu huyo muuza duka hana mke so jamaa akaamua apite na dada yake.
upande mume mwenzie.
 
Hakuna upole wa kuvumilia upumbavu.

Kila kitu kina kipimo chake ukikizidisha
kinakuwa ni upumbavu.

Upole ukizidi unakuwa upumbavu .

Ukorofi ukizidi una kuwa upumbavu.

Upendo ukizidi una kuwa upumbavu.

Mwanaume kuruhusu mkeo akupande kichwani kwa kigezo cha upole huo ni upumbavu
Uko sahihi sana
 
Hii kitu nimeiona hasa kwa wanaume ambao ni wakimya/wapole, mara nyingi huwa hawana bahati ya kupata wanawake wazuri, huwa wanawapata wale machakaramu ambao huwafanya kama wajinga. Japo jamaa huwa wanawapenda sana wake zao.

Nishashuhudia kuna wengine wanavumilia na kuamua kuacha wake zao (nimeshudia ndoa mbili), tena moja jamaa kamuachia mke kila kitu sababu mwanamke alikuwa akimsaliti na alishamfumania mara mbili. Mara ya pili jamaa akaamua kusonga mbele, mwanamke akijifanya mbabe kwamba apewe kila kitu mwana akamuachia. Sasa hivi mwana yupo vizuri mkewe anahali mbaya.

Sasa hii imetokea mwanzoni mwa mwaka huu, kuna jamaa mmoja ni Muhasibu, jamaa ni mkimya, mpole, mstaarabu, na huwa hana mambo mengi. Ana mkewe ambaye mzuri kusema kweli, nyama anazo. Jamaa kamfungulia mkewe kampuni ya mapambo na mapishi, ila yule mwanamke anamwendesha sana na kumletea dharau.

Sasa hapo mtaani kuna jamaa anaduka, huyu muuza duka kwao wamebarikiwa rangi weupe yeye na dada zake. Basi yule mwanamke akaanzisha huhusiano na muuza duka, tena hilo duka lenyewe lipo nyumba ya tatu na walipo panga. Imeenda, kuna wana wakamwambia, ila yule jamaa haku-react ile kumuonyeshea mkewe amekasirika na anajua kinacho endelea yeye na muuza duka.

Jamaa akawa mkimya, watu walitegemea labda atajibu kwa kumpiga au kumkanya yule muuza duka au kumtimua mkewe ila hakufanya hivyo. Kwahiyo watu wakahitimisha jamaa ni kafanyiwa madawa ya kienyeji. Halafu jamaa tokea amuoe mkewe miaka mitano hawajapata mtoto, bado jamaa anamvumilia pamoja na ujinga anaomfanyia.

Hii imeenda enda yule muuza duka dada yake akapaata mimba, kubanwa akasema mimba ni ya yule jamaa ambaye kaka yake anamgongea mkewe. Yaani hapa kitaa jamaa kaacha historia, kumbe kisasi chake yeye alikuwa anakitafuta kimya kimya. Mkewe alichanganyikiwa na mtaa walihama mwezi uliyofuatia wakatafuta nyumba nyingine.
Mwamba katisha mno😂
 
Raha ya mwanaume kuwa mkali, mcontrol mkeo. Na kuwa mtaratibu, mwenye hekima pia mahali panapohitajika. Lakini siyo unakuwa mpoleee, then una visasi vyako vya chini chini. ..Sasa hapo ndo kafanya Nini?. Upumbavu
Kwaiyo alichofanya mwanamke ni sawa?? Agobeggg... Kamuumiza mme deliberately kisa mme mpole. Ulikua unataka wakae wazungumze nn labda. Mpumbavu ni huyo mke..
 
Atumie hekima. Hiyo ndo sawa sawa na mdada anaachwa Leo. Eti kesho anaenda kutembea na ndugu au rafiki ya ex wake ili eti kumkomoa[emoji16]
Hasira na hekima havikai pamoja na havitokuja kukaa pamoja.

Hata wewe mwenyewe ukiwa na hasira basi jua hekima kwako kwa muda huo haipo.
 
Kwaiyo alichofanya mwanamke ni sawa?? Agobeggg... Kamuumiza mme deliberately kisa mme mpole. Ulikua unataka wakae wazungumze nn labda. Mpumbavu ni huyo mke..
Maisha ndani ya ndoa ya watu usiyazungumzie abadani. Sbb huwezi jua alikuwa anamnyanyasa kisa azai na mdada kaamua kutoka kwenda kujaribu tafuta mtoto. Na huyo mbaba hata asijisifu kuwa huyo mtoto asilimia zote ni wake. Lbd amebambikiwa mimba je?. Maisha na ndoa ni fumbo.
 
Binafsi sipendi mwanaume mpole kupitiliza adi aniogope yani nimcontrol hapana
Raha ya mwanaume awe mkali sio legelege
kwamba umcontrol mwanaume? binafsi mimi ni mpole sana, na mkimya. mke wangu anaongea kuliko mimi na anajua hata kupangilia mistari kuliko mimi. ila anajua mipaka, sijawahi kumruhusu avuke mpaka hata kidogo tu, nitahakikisha nimemrudisha hatua 100 nyuma aanze kunisogelea upya. hiyo ni mbinu ya kivita kwetu sisi wanaume.

chukua mfano, Ukrain akisogea kuishambulia Urusi, atakachofanya russia ni kumtandika na kumrudisha nyuma kabisa akaanze kujipanga upya au ajue mipaka asije kuvuka tena. na hata nikikosea anapolalamika au kunikosoa ajue anaongea na kichwa cha familia, haongei na wanawake wenzie wa saluni huko, au asijefikiri anaongea na kaka yake. ni kwamba anaongea na father house, king of the house.

tunaheshimiana kwa namna hiyo. mimi pia yeye najua mipaka yake pamoja na kuongea kwake. nikimkera anaweza kuongeaaaa na mimi namwacha aongeee hadi hasira imwishe asije pasuka, ila aje tuongelee chumbani, akiropoka mbele ya watoto hata kama mimi ndio mwenye makosa, anajua amevuka mstari, makosa yote nitamhamishia yeye na nitahakikisha nimeshinda hadi ameomba msamaha tena wa dhati sio wa kinafiki. hivyo nikimkera, ananiambia tu "baba nakuomba chumbani kuna kitu unisaidie"au anasubiri wakati ule wa kulala, sio kwa kupiga makelele afaidishe majirani au watoto wajue tunagombana, kimyakimya, na kama ni kwikwi afanye kimyakimya.

nikija kwenye mada, nyie wanawake mlioolewa na sisi wanaume wapole au wakimya, fanya yooote ila usimcheat. hata kama yeye amekucheat ukijirudishia aidha muachane au subiri tu hata miaka 10 ikipita kuna kitu atakuja kukufanyia hautakuja kusahau. na huyo mwenye duka, kuna siku atakuja kulia (kama ni story ya kweli), labda jamaa awe boya.

anaweza asikuue ila ndio itakuwa fimbo yake kwako, au anaweza kukuwazia mabaya tu muda wote, anaweza kulipiza kwa kuzalisha wanawake hata 10 uje ulee watoto hadi ahakikishe moyo wake umesuuzika. binafsi nina watoto wa nje ya ndoa waliozaliwa ndani ya ndoa, lakini wife anajua kabisa mpaka ulipo, na anajua siku nikijua amefanya ujinga, fujo yangu haielezeki. kwanza najua hawezi kufanya icho kitu. nina maana yangu kusema hivi.
 
Raha ya mwanaume kuwa mkali, mcontrol mkeo. Na kuwa mtaratibu, mwenye hekima pia mahali panapohitajika. Lakini siyo unakuwa mpoleee, then una visasi vyako vya chini chini. ..Sasa hapo ndo kafanya Nini?. Upumbavu
Acheni tamaa na maisha ya purukushani, kama kuoa kunahitaji purukushani zisizona msingi basi haina maana. Kwelikweli unatamani purukushani maishani na kuanzisha maswaibu bila msingi, basi ni vema nikakaa pembeni nikuangalie tu. Sikuoa mtoto bali mtu mzima mwenzangu nikijua ni mtulivu ila ghafla unataka dramas, nivema nikatafute amani yangu. Wajua majukumu yako namimi nayajua yangu ila ghafla ukajigeuza akili, ni mpumbavu tu ndio awezaye kuyatenda hayo. Nahasira ya mtu mpole na mtaratibu ni mbaya sana, maana uchungu wake ni Mungu tu ajuaye ndani ya moyo wake. Usingemuigizia upole na utaratibu kipindi cha uchumba jua kwamba kamwe asingekuoa, ila mnaigiza baadae mwaja kubadilika, hiyo ni asili ya shetani. Ishi kwa amani na watu wote. Utulivu wangu wa akili (my peace of mind) ni bora zaidi kuliko ngono, maana ndicho kitaniwezesha kutunza wazazi wangu na kulea familia yangu kwakiwango kinachostahili. Ndio maana usifikiri single moms wataisha bali itaongezeka kwakuwa wanawake hutafsiri kuwa ubabe na kurukaruka ndio uanaume, mtazidi kuwaharibia hata vizazi vijavyo. Soma sana biblia, hili jambo limezungumziwa na madhara yake kutolewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kitu nimeiona hasa kwa wanaume ambao ni wakimya/wapole, mara nyingi huwa hawana bahati ya kupata wanawake wazuri, huwa wanawapata wale machakaramu ambao huwafanya kama wajinga. Japo jamaa huwa wanawapenda sana wake zao.

Nishashuhudia kuna wengine wanavumilia na kuamua kuacha wake zao (nimeshudia ndoa mbili), tena moja jamaa kamuachia mke kila kitu sababu mwanamke alikuwa akimsaliti na alishamfumania mara mbili. Mara ya pili jamaa akaamua kusonga mbele, mwanamke akijifanya mbabe kwamba apewe kila kitu mwana akamuachia. Sasa hivi mwana yupo vizuri mkewe anahali mbaya.

Sasa hii imetokea mwanzoni mwa mwaka huu, kuna jamaa mmoja ni Muhasibu, jamaa ni mkimya, mpole, mstaarabu, na huwa hana mambo mengi. Ana mkewe ambaye mzuri kusema kweli, nyama anazo. Jamaa kamfungulia mkewe kampuni ya mapambo na mapishi, ila yule mwanamke anamwendesha sana na kumletea dharau.

Sasa hapo mtaani kuna jamaa anaduka, huyu muuza duka kwao wamebarikiwa rangi weupe yeye na dada zake. Basi yule mwanamke akaanzisha huhusiano na muuza duka, tena hilo duka lenyewe lipo nyumba ya tatu na walipo panga. Imeenda, kuna wana wakamwambia, ila yule jamaa haku-react ile kumuonyeshea mkewe amekasirika na anajua kinacho endelea yeye na muuza duka.

Jamaa akawa mkimya, watu walitegemea labda atajibu kwa kumpiga au kumkanya yule muuza duka au kumtimua mkewe ila hakufanya hivyo. Kwahiyo watu wakahitimisha jamaa ni kafanyiwa madawa ya kienyeji. Halafu jamaa tokea amuoe mkewe miaka mitano hawajapata mtoto, bado jamaa anamvumilia pamoja na ujinga anaomfanyia.

Hii imeenda enda yule muuza duka dada yake akapaata mimba, kubanwa akasema mimba ni ya yule jamaa ambaye kaka yake anamgongea mkewe. Yaani hapa kitaa jamaa kaacha historia, kumbe kisasi chake yeye alikuwa anakitafuta kimya kimya. Mkewe alichanganyikiwa na mtaa walihama mwezi uliyofuatia wakatafuta nyumba nyingine.
kuna mzee moja alimwambia mkewe usiutumie upole wangu vibaya uvumilivu una mwisho wake
 
Back
Top Bottom