Uzi huu ni Kwa ajili ya wadau wa vyombo vya majini Kwa ajili ya shughuli za uvuvi,utalii na michezo.
Mnakaribiahwa Kwa ajili ya namna ya kufanya usajili,Sheria za vyombo vya majini, marekebisho, utunzaji, sehemu za kununua vipuri, changamoto za utumiaji vyombo, sehemu za kuunda boti na kununua injini.
View attachment 1637202
Kwa wale wa boti za mbao za kuchonga hutegemea aina ya mbao atakayo na zinazopatikana.
View attachment 1637167
Boti za fiber kuna za kuagiza nje au kutengeneza hapa hapa nchini, hizi hutumika sana kwenye shughuli za utalii,uvuvi na michezo kulingana na hitaji la mmiliki.
View attachment 1637190
Kwa upande wa injini kuna injini za ndani ya boti(inboard engine) na nje (outboard engine).
Boti injini zake zinatumia mifumo ya propela na jet propulsion.
View attachment 1637192
Kwa wadau wa michezo ya majini kuna Jet Ski (pikipiki maji) hizi zinatumia mfumo wa jet propulsion. Na zipo zinazotumia nishati ya umeme na petrol.
View attachment 1637191
Karibuni Kwa mawazo, maoni, maswali,ushauri, mchango wowote kuhusiana na vyombo vya majini.