Kwa wajuzi na wajuvi wa Kiswahili, nini Kiswahili cha haya maneno?

Unateuliwa baada ya majadiliano ya wanafamilia na kukubaliana kisha ndio wanakuchagua/kukuteua wewe,

Huwezi ukateuliwa na watu wengi bali unachaguliwa,mtu mmoja ndio anaweza kuteua coz inakua ni amri yake yeye pekee na hakuna wa kumpinga.
Sasa kama huwezi kuteuliwa na watu wengi, bali unachaguliwa, iweje sasa Rais aliyechaguliwa ambaye bado hajaapishwa aitwe ‘Rais mteule’ na si ‘Rais mchaguliwa’?

Manake huyo Rais ndo kachaguliwa na watu wengi waliopiga kura kwenye uchaguzi.

Make it make sense, please.
 
Ni kweli!

Na ukweli huo ndo huivunja hoja ya wale wasmao kwamba eti Kiswahili hakijitoshelezi na ndo maana lugha ya Kiingereza bado inatumika kwenye sehemu kama mahakama.

Swali langu kwao, ni lugha gani/ ipi hapa duniani inayojitosheleza?
mandarin/chinese

kwa nionavyo, sijahakiki

lugha ya tofauti sana hiyo, over 7,000 characters
 
Sasa kama huwezi kuteuliwa na watu wengi, bali unachaguliwa, iweje sasa Rais aliyechaguliwa ambaye bado hajaapishwa aitwe ‘Rais mteule’ na si ‘Rais mchaguliwa’?

Manake huyo Rais ndo kachaguliwa na watu wengi waliopiga kura kwenye uchaguzi.

Make it make sense, please.
Mkuu,

Toka mwanzo nakwambia kua Mteule na Mchaguliwa yote ni maneno yenye maana moja tu,

Ukiyatafsiri kwa Kiingereza ndio inakuletea utatanishi.
 
Kateuliwa na nani?
Mkuu Nyani Ngabu, swali hili wengi tuliliona kama ni poa tu. Lakini linafikirisha. But anyway ngoja nidadavue .
Kwanza kabisa hufanyika uchaguzi wa kumchagua mmoja kati ya wagombeaji wa kiti hicho cha urais. Sasa katika kuhesabia matokeo uchaguzi huwa umekwisha, zitahesabiwa na mwisho kumpata mshindi wa kinyang'anyiro cha urais. Huyu mtoa sauti huyu yeye humtangaza mshindi kati ya wawili wa ambao kura zao ni za juu kuliko wengine. Kwa kawaida Rais huyu huwa anakuwa ameshinda na wakati huo akisubiri kuapishwa. Kile kitendo cha kusubiri kuapishwa huwa mtu huyu yuko katika nafasi ya uteule na baada ya kuapishwa rasmi kuwa Rais ni kukamilika rasmi kwa zoezi cha kuchaguliwa kwako kuwa Rais.
 
Hmm 🤔 🤣.
 
Kateuliwa kwenye uchaguzi au kachaguliwa kwenye uchaguzi?

Wananchi walipiga kura kuchagua au kuteua Rais?
Kuchagua, unaweza kuchagua ata kisicho faa.
Ila kuteua, ina maana umeona anafaa.
Kwa kuwa wananchi ni wengi, na ni vigumu kusikia sauti yao katika kuteua, ndio maana wanatumia njia ya kura kuteua na si kuchagua.
Kwa mazingira hayo, tunasema wananchi wame mteua​
 
1. President-elect; kwa Kiswahili tafsiri yake ni Rais mteule.

Rais aliyechaguliwa anakuwaje rais mteule? Mteule si yule anayeteuliwa?

President - rais.

Elect-chagua/ chaguliwa.

Kwa nini huyo anayeitwa rais mteule asiitwe ‘Rais-mchaguliwa’, badala yake?

2. Nini Kiswahili cha haya maneno?
  • shule
  • chai
  • pesa.
  • redio
  • shati
Mara nyingi raisi anakuaga anajulikana ni nani kabla hata kampeni hazijaanza...

Sasa wale waliomteua ndio wanamuita raisi mteule, baadae ndio anakuja kuchaguliwa na wananchi
 
Kuchagua, unaweza kuchagua ata kisicho faa.
Ila kuteua, ina maana umeona anafaa.
Kwa kuwa wananchi ni wengi, na ni vigumu kusikia sauti yao katika kuteua, ndio maana wanatumia njia ya kura kuteua na si kuchagua.
Kwa mazingira hayo, tunasema wananchi wame mteua​
Equation x mteule vs Equation x mchaguliwa , mteule kuna namna ina sound🤔
 
Wabantu hatujawahi kuwa na uchaguzi,viongozi walikuwa wanateuliwa au kusimikwa kuchagua kumekuja na democracies za magharibi...
Kwani ndipo umekurupuka usingizini, mkuu? Mbona uko nje ya mada, kana kwamba umetokea kwenye vikao vya vyama vya siasa?
 
Unateuliwa baada ya majadiliano ya wanafamilia na kukubaliana kisha ndio wanakuchagua/kukuteua wewe,

Huwezi ukateuliwa na watu wengi bali unachaguliwa,mtu mmoja ndio anaweza kuteua coz inakua ni amri yake yeye pekee na hakuna wa kumpinga.
OP & nonsense. Dhana ya elect ni uchaguzi, na wala siyo mineng'eneko unayojaribu kuuaminisha umma hapa jukwaani.
 
Back
Top Bottom