Hii thread utadhani imeniongelea mimi, Nna ka gari kamkopo, Nimepanga upande wa nyuma ya nyumba sinza, Na starehe nimeeendekeza kila weekends. Lakini baada ya kujifikiria sana naona sio tatizo. Sijaoa, Sina majukumu na mshahara wangu unamaliza mwezi bila kujibana sana pamoja na kuwa ninahonga from time to time. Baada ya ku graduate ukibahatika kupata kazi haraka unakuwa unafikiria nifaidi vipi maisha.
Sikuwa na matumizi makubwa wakati niko chuo hivyo kinachobaki ukitoa makato mwanzo wa mwezi kinadumu vizuri tuu. Alafu Ningeambiwa nitoe 12m cash kulipia gari nisingeweza so sio kosa. Hadi nitakavyokuwa na Commitments sioni kuwa nakosea. You only live once sijui wewe ulitaka nichukue 12m nikanunue kiwanja? alafu ningejengaje wakati ninalipa mkopo? Bongo tambarare