kwa wakaka wa kitanzania tu

kwa wakaka wa kitanzania tu

Hata mimi sijawai kuskia baba mwenyn gari...naskia tu BABA MWENYE NYUMBA.
 
We binadamu upo? nina kama wiki sijakutia machoni, well ujumbe umefika ila kiukweli hata wadada magari mnayoendesha kadi zipo kwa waliowapa magari siku ukiwa goigoi kwenye kutoa huduma unanyang'anywa gari unarudi kwenye daladala!

Sasa sijui yule wa kukopa na wa kuhongwa yupi yupo juu..........

nipo moh'd. Vipi kisomo cha uzeeni? Mi staki gari ya kupewa, labda nipewe na baba. Lol.
 
Hii thread utadhani imeniongelea mimi, Nna ka gari kamkopo, Nimepanga upande wa nyuma ya nyumba sinza, Na starehe nimeeendekeza kila weekends. Lakini baada ya kujifikiria sana naona sio tatizo. Sijaoa, Sina majukumu na mshahara wangu unamaliza mwezi bila kujibana sana pamoja na kuwa ninahonga from time to time. Baada ya ku graduate ukibahatika kupata kazi haraka unakuwa unafikiria nifaidi vipi maisha.

Sikuwa na matumizi makubwa wakati niko chuo hivyo kinachobaki ukitoa makato mwanzo wa mwezi kinadumu vizuri tuu. Alafu Ningeambiwa nitoe 12m cash kulipia gari nisingeweza so sio kosa. Hadi nitakavyokuwa na Commitments sioni kuwa nakosea. You only live once sijui wewe ulitaka nichukue 12m nikanunue kiwanja? alafu ningejengaje wakati ninalipa mkopo? Bongo tambarare
 
Ebu tuongee kuhusu pasaka bana..or shud i PM u!??
 
raha jipe mwenyewe!

Hii thread utadhani imeniongelea mimi, Nna ka gari kamkopo, Nimepanga upande wa nyuma ya nyumba sinza, Na starehe nimeeendekeza kila weekends. Lakini baada ya kujifikiria sana naona sio tatizo. Sijaoa, Sina majukumu na mshahara wangu unamaliza mwezi bila kujibana sana pamoja na kuwa ninahonga from time to time. Baada ya ku graduate ukibahatika kupata kazi haraka unakuwa unafikiria nifaidi vipi maisha.

Sikuwa na matumizi makubwa wakati niko chuo hivyo kinachobaki ukitoa makato mwanzo wa mwezi kinadumu vizuri tuu. Alafu Ningeambiwa nitoe 12m cash kulipia gari nisingeweza so sio kosa. Hadi nitakavyokuwa na Commitments sioni kuwa nakosea. You only live once sijui wewe ulitaka nichukue 12m nikanunue kiwanja? alafu ningejengaje wakati ninalipa mkopo? Bongo tambarare
 
I dont care how you might be looking like, your age and everything you might be lacking! All i need to know, are you single and you wish to have someone serious for your future? Your brain tells that you are the best wife material. Bahati nzuri kigari ninacho na kijihouse cha kuanzia maisha tayari kipo so unaweza kuni-PM tu for more details. Am eagly waiting
 
Smile umeongea ukweli but umesahau wazazi nao wanachangia kuharibu watoto, wengine since childhood shule unapelekwa kwa gari, sekondari ndo hizo za kina mwanaasha, sasa daladala inakuwa adhabu kweli ndo maana ukianza kazi fasta gari hata ya mkopo,

But through experience ni ushauri tu wadau usinunue gari kama una kipato kilichosimama,to be honest gari inanishinda baada ya kuanza kujitegemea few months ago, nilibahatika kupata kibarua soon after xul, and b mkubwa alininulia gari ndogo for work, tatizo toka nilipoondoka home na kwenda kujitegemea naona inachukua sana my income hadi nashindwa kufanya vitu vingine na kuamua kuitumia wekend tu au siku nikijisikia mchovu but other days daladala so that mambo mengine yaende hasa kupata kibanda hata mapepwande...through my experience Budget ya gari ndogo tu ya cc 1500 ni not less than lak 3 na hapo ikiwa haijaharibika wala kupata ajali yoyote,motorvehicle and insurance haudaiwi, parking is free na wala traffic hajazingua.. so kwa mkopo sikushahuri hata iweje maana utachanganyikiwa bure ndugu yangu, car is for young proffessional galz as wao hawana majukumu ya ujenzi wala nini zaidi ya kusubiri kuolewa
 
Gari ni asset kama asset zingine,nikipigika nauza napata changu, kuaribika hata nyumba inaweza kusombwa na mafuriko then ukaumia,jua jinsi ya kutumia gari ili maisha yaendelee! Narrow minded!
 
Tuache masihara nyie akina dada mnapenda magari vby sana tena nnapenda madereva mkijua ndo wenye magari hata kama gari lina namba PT hamjali. Nimefanya reseach fupi huwa nikiwa kwny gari naangalia wakina dada wakiona gari wao wako kwa miguu wanatoa macho kwa dereva tena yale ya husuda lakini ukw vt vya abiria hawana hbr nae. Hata ukw na mdada kwa miguu we mtazame usoni gari ikw inapita kama g friend wako unaweza rusha ngumi. Hapo unamfanya bfrnd wako akimbie benk or saccos.
 
Dada yangu smile, nimeisoma threat yako kwa umakini mkubwa kabisa na nimeielewa baraabara na yote uliyoyasema ni ukweli mtupu ila kwa upande wangu sioni haja ya wewe kumwaga mchele kwenye kuku wengi hasa ukizingatia jamaa mwenyewe yumo humu humu ndani. Ungetumia tu busara kidogo ya kulimaliza jambo hili kimya kimya bila ya kuaibishana na ninaamini angekuelewa tu. Kama ingelikuwa ni wewe sidhani kama ungelifurahi kuanikwa hivi hadharani na kuabishwa kiasi hiki. Ingawa hujamtaja jina lakini napata hisia ni jinsi anaumia kwa kumuanika kiasi hichi. Jambo usilopenda kufanyiwa usimfanyie mwingine. Huo ni ushauri wangu tu.
 
Simile, nikopeshe basi dola 200 nipate za kunywea wiki end hii. Mwenzio niko kona kabisa na wikend ndo hiyo imefika. Please, usinangushe. Ntakurudishia pay check yangu ikitoka. Najitolea kukutoa out in return. (Ngoja nione kama utachomoa hapo).
 
Back
Top Bottom