Nelson Kileo
JF-Expert Member
- Oct 29, 2011
- 3,053
- 3,259
1. Huku pia tuna TV lakini chaneli zetu ni TBC na ITV hakuna mambo ya kuangalia series na TV tunawasha kuanzia saa 12 jioni baada ya kutoka shamba, acheni shobo.
2. Mje na dada wa kazi huku hakuna mtu wa kubeba mtoto wako anaye deka-deka.
3. Hakuna kuchotewa maji ya kuoga, ndoo ya maji kutoka Bomba la nje mtabeba wenyewe.
4. Mje na midoli ya kuchezea watoto wenu wasije kutunyongea vifaranga.
5. Hakuna kuchinjiwa kuku hadi siku ya christmas.
6. Ukimaliza kuoga toka na sabuni kwa sababu hiyo hiyo ndiyo tunaoshea vyombo.
7. Ukija na mke au mume wako asianze kusema mboga hii akila anaumwa tumbo sisi tunakujua tangu ulivyokuwa mdogo ulikuwa unakula makande au viazi chukuchuku na haukuwahi kuumwa tumbo kwa hiyo mtakula chochote kitakachopikwa.
8. Huku hakuna kumbembeleza mtoto wakati wa kula akikataa kula sisi tunakula na tunamaliza.
9. Usiku hakuna kumulikiwa tundu la choo unapapasa na mguu tu.
10. Hakuna Kutupa ugali au wali uliolala huo ni mkate wetu asubuhi.
11. Hakuna mto wa kulalia huku unalalia mikono kwa kukunja ngumi.
12. La mwisho wale mliopo kwenye ajira zaidi ya miaka 10 na huku nyumbani hamjajenga mtakuwa mnalala kwa mwenyekiti wa Kitongoji/Kijiji.
Ahsanteni na karibuni sana 🙏🙏