Wapendwa waishio mijini, tunayo furaha kuwakaribisha nyumbani kwa ajili ya kusherehekea Krismasi. Lakini kabla hamjakanyaga ardhi ya kijiji, tafadhali zingatieni mambo haya muhimu ili kujiepusha na migogoro isiyohitajika:
1. TV ZA KIJIJINI:
Ndiyo, tuna TV. Lakini sahau kuhusu "Netflix and chill." Huku ni "TBC and patience." Na hata hiyo TV haijawashwa mchana, inangoja saa mbili usiku, baada ya mbuzi kurudi zizini na watoto kulala.
2. HATUNA WAFANYAKAZI WA NDANI:
Hii sio mjengo wa mtaa wa Mbezi. Kama umezoea kubebwa mabegi na kufanyiwa kila kitu, basi njoo na huyo dada wa kazi wako. Huku hakuna mtu wa kubeba watoto wako wala kukuambia, "Chai yako iko tayari."
3. MTONI NI GYM YA KILA MTU:
Kama unaogopa kuchota maji, ni bora ubaki mjini. Huku unachukua ndoo yako mwenyewe, unashuka mtoni, na unajifunza uzalendo wa kufua nguo ukitumia mawe.
4. VIFARANGA SIO MIDOLI:
Kama watoto wako hawana midoli, tafadhali wape. Huku vifaranga hawana nguvu za kujitetea. Tumeshaona vifaranga wakinyongwa kwa kamba za viatu wakibadilishwa kuwa "midoli."
5. KUKU WA KRISMASI:
Kuku wetu sio wa kuchinjwa kabla ya tarehe 25. Ukisikia harufu ya kuku mapema, basi jua ni ndoto yako tu. Tuna sheria za kidini kuhusu siku za kuchinja.
6. SABUNI ZA MULTIPURPOSE:
Usijali kuhusu "Omo" au "Sunlight." Sabuni ya kuogea ndiyo hiyo hiyo ya kufulia na kuoshea vyombo. Ukimaliza kuoga, acha sabuni ikauke vizuri kwa matumizi mengine.
7. MKE/MUME MSONYO:
Tafadhali mwambie mke/mume wako kuwa huku "Tumbo linauma" sio kisingizio. Ulivyokuwa mdogo ulikula hata maembe yenye ukungu na hukuwahi kulalamika. Kwa hiyo chochote kitakachopikwa, kinashuka tumboni bila mjadala.
8. WATOTO WAKATAA KULA:
Huku hakuna drama za kumbembeleza mtoto. Akikataa kula, basi chakula hakilali. Sisi tunakula hadi kisahani kinang'aa.
9. CHOO CHA USIKU:
Huku tunaitwa wapiga ramli wa kitaalamu. Tundu la choo halimulikiwi, unapapasa tu kwa mguu mpaka ulifikie. Hakuna "torch" wala "flashlight."
10. UGALI ULIOPUMZIKA:
Ugali wa jana sio chakula kilichoharibika. Ni "mkate wa kijiji." Usishangae tukiamka na kuunga chai na ugali uliolala. Ni utamaduni!
11. MITO YA ASILI:
Sahau kuhusu mito ya masponji yenye 'memory foam.' Huku mikono yako ndio mto wa kitaifa. Tunaita "biceps comfort."
12. WAJENZI WA NDOTO:
Ukiwa na zaidi ya miaka 10 kwenye ajira na bado hujajenga kijijini, nafasi yako ni kwa mwenyekiti. Hatuwezi kukuandalia malazi huku hata tembe moja hujajenga.
Tunaomba mzingatie haya yote. Siku ya Krismasi siyo tu sherehe, bali ni mafunzo ya kurudi kwenye asili! Karibuni sana, lakini mjue, vijijini ni shule ya maisha.
AHASANTENI NA HERI YA KRISMASI!