Kwa wale mnaopenda kula hotel ya Aljazeera

Kwa wale mnaopenda kula hotel ya Aljazeera

Kuna watu Kweli wanashindana kununua Chakula njiani. Sio kitu kizuri, Nakumbuka kuna kipindi nlisafiri na wenzangu,walipofika pale Liverpool mbioo kwenye mabufee,nyamachoma nk.
Kama mashindano vilee. Mm nliyechukua Soda Take Away na biskuti,Wakaanza kuniita Mbahili na majina kibao!! Ukweli jamaa wa hii migahawa wanachojali ni pesa tu.
 
safarini ni sehemu nzuri sana ya kujipima ni muda gani unaweza kaa na njaa.
Maajabu wengi wetu hushindana kula.

Nakumbumbka wakat narudi home wakat nasoma, nliwaiga wenzangu nunua vyakula,lakin wala sikula.

Kwanini hukula.?!
 
Habari wakuu

Nikiwa safarini kutokea Songea kuja Jijini Dar ili kupata Mlo wa mchana imebidi tupitie hotel ya Aljazeera, kwa wale wanaotokea Iringa, Njombe na makambako wanajjua.

Huduma za vyakula ni mbovu kupita maelezo nikimaanisha ubora wa chakula chenyewe ni mbovu kwani kidogo waniuzie kiporo cha wali kuku nikawaambia huo ujanja wenu naufahamu time na kama hakuna chakula kilichopikwa Leo basi rudisheni hela Yangu.

Mdada akaja juu ananifokea nikamwambia chakula chenu hicho hapo kwenye Meza nawaachieni mle Mimi naendelea na safari.

Nikatoka zangu nje nataka kuingia kwenye Gari Mara MTU ananivuta shati chukua hela yako, ilikuwa shilingi elfu tano, nikacheka kimoyomoyo nikaondoka zangu. Huwa sina tabia ya kula safarini ila kwa sababu natumia dawa ilinibidi.
Nitaenda kula mbele ya safari.

Nilikuwa nikisikia watu wakilalamika kuhusiana na hii hotel kuhusiana na chakula kibovu na lugha chafu za wafanyakazi ila Leo nimeshuhudia mwenyewe.
Hiyo Mbeya kwa father G enzi hizo, ukizubaa unapigiwa mpe wali jaa mchuzi juu, kumbe ni wali wa jana na mchuzi wa juzi,yaani ni shida sana.
 
Duh, aisee. Wapi hio.?
Pale Al Jazeera Ruaha Mbuyuni, chooni ni kuchafu balaa, kiasi kwamba huwa najiuliza, wamiliki wa mradi ule hawakagui hali ilivyo? Ni lazima uwe na tatizo kidogo kula pale al Jazeera. Ni hatari kwa afya yako.
 
Hakuna mtu anayetambua anakulaga hapo mahali. Hao waarabu ni wachafu kama wachawi.
 
Back
Top Bottom