Kwa wale 'not eligible' kutoka NACTE mmeshajijua?

kijimsela

Member
Joined
Mar 17, 2013
Posts
97
Reaction score
15
Habari wana JF,

Naomba kuuliza kama kunayeyote anataarifa kwenye CAS-Profile yake kuwa not eligible.

maana kwenye tangazo lao linasema kuwa:

17043 applicants who have applied to Bachelor degree programs so far.
15090 applicants have reached program selection stage and made choices of the programs they want to study.
1053
applicants have not made any selection.
11,881 are eligible choices
4562 slots being filled as FIRST BATCH applicants.

Kutokana na maelezo hayo inamaana kuna watu ambao not eligible, je wametumiwa tangazo la second round?
Maana mi kwenye profile yangu sioni chochote na nashindwa kujielewa na siku ndo hiyo inakaribia ya tarehe 22 ambayo watatoa majina rasmi, sijui hiyo second itatoka siku hiyo ya tar 22?

Kwakweli wana jamvi naomba mnieleweshe mlivyoelewa wenzangu au profile zenu zinasemaje.

KARIBUNI!
 
Kuna sms wametoa iko mwisho kabisa kwenye profile yako toka jumapili

MKUU mimi NILIVYOIELEWA ILU UJUMBE KWENYE PROFILE YANGU NI KAMA INATUOMBA KUWA WAVUMILIVU WAKATI ZOEZI LA KUCHAKATA ELIGIBILITY LINAENDELEA.

KWA HIYO HAPO BADO UJATOA JIBU LINALOENDANA NA SWALI.

NI KWELI MM NAHISI NI VEMA WATUJIBU KWENYE PROFILE ZETU KAMA MTU KAFANIKISHA KUPATA CHUO AU LAA KAMA WALIVYOFANYA TCU KWA WATU WA FORM SIX.
 
Haswaa, ufahamu wako unaenda na wangu.

Inamaana kutakuwa hakuna mtu aliyetumiwa ujumbe wa kurudia maombi mpaka leo? kama ni hivyo wote tupo njia panda na ukizingatia zimebaki siku chache duh!
 
subirini majibu ninyi diploma mmegaiwa au mmesoma wenyewe. mbona hamuelewi yote mmnaye ambiwa. nahisi hata chuo hamtapata hata mkipata safari yenu huko sio ndefu. vuteni subira na acheni kukiana presha diploma sio sawa na form six na hazitaweza fanana na ndio maana zipo kwenye mifumo tofauti.
 
Ndio hicho tuu unachoweza kusema?
 
Ile sms inatosha kabisa kuto kuhoj, coz wametuambia tuwe wavumilivu, sas kwanin tuendelee kuulza, tucwe na haraka jaman tutapata 2 Vyuo, tuwe wavumilivu jaman
 
subirini majibu ninyi diploma mmegaiwa au mmesoma wenyewe. mbona hamuelewi yote mmnaye ambiwa. nahisi hata chuo hamtapata hata mkipata safari yenu huko sio ndefu. vuteni subira na acheni kukiana presha diploma sio sawa na form six na hazitaweza fanana na ndio maana zipo kwenye mifumo tofauti.

AKILI YAKO UNAHISI WALIOPITIA DIPLOMA HAWAJAPTA F6!?
Subiri Uende Chuo Wakakuburuze
 
Ile sms inatosha kabisa kuto kuhoj, coz wametuambia tuwe wavumilivu, sas kwanin tuendelee kuulza, tucwe na haraka jaman tutapata 2 Vyuo, tuwe wavumilivu jaman

Tatizo sio haraka, tatizo kuwa informed na system.
Ni vema kuwashirikisha wenzio na kujua kweli system kwangu ipo sawa na wenzangu? maana hizi system sio za kuziamini sana na ndiyo maana kuna watu wameapply na wamekaa wakisubilia sellection kumbe nacte hawajaona sellection zao thats why wametoa mchanganuo. Kwa hiyo kuulizana hivi kwa kutumia mitandao inasaidia mtu kujihakikishia zaidi kuwa upo updated.

Lakini pia NACTE na TCU hawapo pale na usemi wa Idumu kauli ya mwenyekiti, wanasikiliza sana maoni kutoka kwa wadau wa aina zote kwani wao pia ni binadamu kama ulivyo wewe na ndiyo maana watu walilalamika sana kwenye mitandao kuwa mbona hawa watu wapo kimya hakuna taarifa yoyote? ndipo wakatoa tangazo lile ambalo tunaloliona chini ya profile zetu na matangazo kadhaa kwenye website yao.

Ushauri wangu nikwamba tusijiaminishe sana na hizi system, basi tukabweteka na laptop zetu au simu zetu kumbuka hizi system ndiyo kwanza zinaanza kwenye nchi zetu hizi masikini kuna errors kibao zinazojitokeza kwenye hizi system, na kama haija kukuta wewe basi imemkuta mwenzio.

Kwa hiyo ni bora kujulishana na kuhakikishiana kupitia kwenye mitandao yetu hii, pia ni vema kukosoana kwa lugha nzuri tu pale kwenye mistake lakini siyo kutukanana au kukashifiana kama jamaa mmoja hapo juu amejikuta akilopoka hoo! "nyie na diproma zenu hizo za kupewa hamtopata chuo na mkipata hamtadumu" mi nimuhakikishie tu kwamba diproma zetu hizi tumezisomea kwa kuhoji, kudadisi na kuchanganua mambo kwa hiyo tutadumu katika level yeyote ile ya elimu.

I'm sory kama ntakuwa nimemkwaza mtu.
 
Embu nisaidien me nimeapply Tcu kwa chet cha diploma sikujua tunatakiwa tuapply nacte kuna shida kwel
 
Mh! cha kukushauri wasiliana na TCU pamoja na NACTE uwaeleze hali halisi.

maana nijuavyo mimi unavyojaza maelezo yako kwenye system ya TCU unajaza data za FM 6 na si za diproma, sasa kama wewe uliona sehemu ya diproma na ukajaza basi wanaweza wakakutransfer kule NACTE ila cha muhimu wasiliana nao mapema wote kabla ya second round haijaisha kwa upande wa nacte.

Chakushukuru leo wametoa majina kwa ambao hawajachaguliwa first batch, hivyo jitahidi kuyaangalia majina hayo na kama haupo basi fanya hima uombe tena Nacte lkn wasiliana nao kwanza.
 
subirini majibu ninyi diploma mmegaiwa au mmesoma wenyewe. mbona hamuelewi yote mmnaye ambiwa. nahisi hata chuo hamtapata hata mkipata safari yenu huko sio ndefu. vuteni subira na acheni kukiana presha diploma sio sawa na form six na hazitaweza fanana na ndio maana zipo kwenye mifumo tofauti.

pathetic
 
Tatizo sio haraka, tatizo kuwa informed na system.
Ni vema kuwashirikisha wenzio na kujua kweli system kwangu ipo sawa na wenzangu? maana hizi system sio za kuziamini sana na ndiyo maana kuna watu wameapply na wamekaa wakisubilia sellection kumbe nacte hawajaona sellection zao thats why wametoa mchanganuo. Kwa hiyo kuulizana hivi kwa kutumia mitandao inasaidia mtu kujihakikishia zaidi kuwa upo updated.

Lakini pia NACTE na TCU hawapo pale na usemi wa Idumu kauli ya mwenyekiti, MUACHE HUYO FARA,AJUI KAMA DIPLOMA NDIO UWA TUNAKULA BATA VYUONI,TUNASOMA BILA STRESS.FORM SIX WENGI UISHIA NJIANI.
 
Embu nisaidien me nimeapply Tcu kwa chet cha diploma sikujua tunatakiwa tuapply nacte kuna shida kwel

kama kulikuwa na option ya kuapply diploma husiwe na hofu,wale ni kama ofisi moja tu na tarehe 22th sept tcu na nacte wanakutana kujadili na kupitisha walivyonavyo mikonono.
 
Duh asante kwa kunitoa hofu,,Option ya diploma ilikwepo
 
Mh! cha kukushauri wasiliana na TCU pamoja na NACTE uwaeleze hali halisi.

maana nijuavyo mimi unavyojaza maelezo yako kwenye system ya TCU unajaza data za FM 6 na si za diproma, sasa kama wewe uliona sehemu ya diproma na ukajaza basi wanaweza wakakutransfer kule NACTE ila cha muhimu wasiliana nao mapema wote kabla ya second round haijaisha kwa upande wa nacte.

Chakushukuru leo wametoa majina kwa ambao hawajachaguliwa first batch, hivyo jitahidi kuyaangalia majina hayo na kama haupo basi fanya hima uombe tena Nacte lkn wasiliana nao kwanza.

Nashukuru kwa ushauri ila option ya diploma ilikwepo
 
majina yaliyotelewa ni ya wale ambao hawakumaliza application mpaka program selection sio kwamba hawakuchaguliwa.. kwa maana hata choice zenyewe hawajafanya. kwahiyo wanahimiza kumalizia ili wawepo kwenye selection.
 
Back
Top Bottom