Mimi baada ya kufaulu STD 7....mama wa kambo akafanya visa ili niondolewe nyumbani..baba akanichukuwa akanipeleka kwa mjomba wake,,ambaye mm namwita babu...nilikaa kuanzia form 1 hadi form 4.....muda wote huo baba alikuwa kila jioni anapitisha pesa ya chakula pale kwa MJOMBA ,,nakumbuka alikuwa anatoa kati ya sh 1000 na 2000 hyo ilikuwa mwaka 1991.......siku kama hajapita pale ujuwe ni deni kwake....na yule MJOMBA si kama alikuwa hafanyi kazi,,,alikuwa anafanya kazi bandarini kipindi hicho...kufika 1993 kampuni aliyokuwa anafanya baba iliuzwa na wafanyakazi walisitishiwa AJIRA ZAO.....hapo ndy VISA VILIVYOANZA kwa yule BABU....baada ya BABA kukosa pesa za kuleta pale nyumbani.....nilipata taabu sana....yule BABU alinifukuza pale nyumbani japokuwa ile nyumba ni ya family na BABA yngu pia inamuhusu,,lakini nilifukuzwa..nikawa nalala tu nje kwenye frem ya DUKA...au kwa friends tu..sometimes unakuta mshikaji yupo na demu wake..inabidi umsubiri hadi saa sita au saba wakimaliza mambo yao ndy na mm naingia kulala..... nikitaka kula nakwenda MIDIZINI MANZESE huko ndipo baba alipokuwa kapanga,,, baada ya baba kuachishwa kazi yule mama aliyokuwa anaishi nae alimkimbia...mzee akahama kule magomeni akahamia MIDIZINI MANZESE,,,,basi ikawa natoka magomeni kwa mguu napita border to border hadi manzese ..kwa siku nakwenda mara mbili...asubuhi na jioni..HEBU FIKIRIA NASOMA wakati huo nina kama miaka 15 tu,, mtu anakufanyia VISA HIVYO.. .sometimes BABA SIMKUTI....nikimkuta ndy nitakunywa chai,,, au nakula mchana,,,,nilipata taabu sana tu kwa mzee yule mjomba wa baba,,alikuwa ana search nyumba nzima ahakikishe mm silali mle ndani, ,MUNGU mkubwa baada ya kumaliza shule kwa shida sn,,,NDY SAFARI YA MWANAUME ikaanza....nilipambana sana hadi sasa hapa nilipo NAMSHUKURU MUNGU...leo hii yule MJOMBA wa baba anaishi VIBAYA SANA,,,watoto wake hawamsaidii...kuniomba mimi anashindwa,,kuna siku moja tulikutana kwenye SHUGHULI FULANI ya kifamilia alivyoniona akashangaa sana,,,akataka apaone ninapoishi,,ajiridhishe...,siku akaja kwangu ,,,ALISHANGAA SN....AKAANZA kulalamika sana juu ya watoto wake, na maisha anayoishi sasa,,nikafikiria sana hivi huyu mzee anakumbuka kweli aliyonitendea mimi nilimsaidia ...tena alilalamika hana SIMU NIKAMPA SMART PHONE..nzr tu..akalalamika habari ya KUPASHA CHAKULA,,, NIKAMPA NA MICROWAVE..MPYA KABISA...nilinunuwa south ...akaondoka navyo kwenda huko anapoishi sasa..na nilimpa kusudi ili akifika huko kwa MKEWE akimwambiya nimempa mimi VITU HIVYO,,,NDY WATAKUMBUSHANA VISA walivyonifanyia wakati nipo mdogo...MARA INGINE NAHISI ....maisha niliyoishi UTOTONI NDY YAMENIFUNDISHA LEO...KUPAMBANA.....tena mapambano ya USO KWA USO na ADUI...bila kupepesa macho...