Kwa wale tuliolelewa kwa ndugu,tukutane hapa na kukumbushana changamoto,chuki na mateso.

Kwa wale tuliolelewa kwa ndugu,tukutane hapa na kukumbushana changamoto,chuki na mateso.

Nilishasema na kula kiapo sitakaa na ndugu katika maisha yangu yote hata kama sitakuwa na watoto. Hakuna watu wana inferiority complex kama ndugu, hawataki kabisa kuambiwa kama wanakosea sana sana wanaona wanaonewa kisa sio watoto wa kuzaa. Kuna jamaa alilelewa na bi mkubwa wangu toka kijijini amekuja kulijua jiji akawa mlevi anataka arudi home mida anayotaka yani ujinga tu, kawekwa chini na kuambiwa akaondoka bila kuaga na kutangaza kafukuzwa. Japo watu wenye akili lakini watoto wengi wa ndugu ni mzigo na wamejawa Ile kitu huyu sio baba angu mazazi au mama.

Namkubali sana mshua wangu huwa hataki huo ujinga wa kulea Mizigo isiyo yake and I will follow the steps.
 
Nilianza kulelewa na ndugu wa upande wa baba angu, Nimemjua mama angu baada ya kupata akili zangu, nikagundua kinachosumbua watoto wanaolelewa na ndugu/mtu baki ni inferior complexity (psychological problems)ile hali ya kuhisi kuonewa onewa tu kwa kila jambo lakini ,(though wapo walezi wenye kuonea watoto wasio wao) ila mara nyingi mtoto asiye wako akili yake mda wote inawaza kuonewa onewa tu, ukimtuma kazi ataona kama umemuonea, akikosea ukamsema atafeel the same way, etc

Swali , Je hakuna wazazi wanaowapiga au kuwapa adhabu watoto zao??

[emoji1426][emoji1426]Hii akifanya mtu ambae sio mzazi wako utahisi 100% umeonewa na utalia sana tofauti na akikuadhibu mzazi wako baada ya muda utasahau.
Yaani kweli tupu nimeya shuhudia kwenye familia yangu yani mtu anafanya ujinga hataki kuambiwa kisa baba/mama sio wake.
 
pamoja na hayo yote ila kuna mema pia tunapata. Kama kupewa hifadhi na sehemu ya kuishi, kupelekwa shuleni na kupata elimu, pia zipo faida nyingi siwezi kuziandika zote. Cha muhimu tusipende kuangalia upande mmoja wa kero na tukasahau kuwa bila hao ndugu labda tusinge fika hapa. kuna wengine tulikuwa na wazazi ila tulilelewa na ndugu, je huoni kama hapo walitutakia mema?. So usipende kulalamika sana maana jukumu la kukuandalia maisha ni la baba yako na mama yako, kwa kuwa ndugu nao wana watoto wao ambao inabidi wapate maisha mazuri.
Point kabisa, na hii ndio kauli mbiu yangu mimi kama sio baba yako pita wiki mbili urudi kwenu kwangu nakaa na watoto wangu tu.
 
Kipindi hicho,naishi kwa bro,shemeji yangu,kila wimbo wa twangapepeta uliokuwa na maneno,"chande kula na kulala kwa kaka,"ulipokuwa ukipigwa,lazima aniite nije nisikilize,ilikuwa inaniuma sana,lakini mtoto wa kiume utafanyaje?unaishia kusikiliza,unajichekesha,kama utani vile,kumbe moyo unauma,
Mchana msosi hakuna,ni kawa nashinda kijiweni tu,mpaka jioni,huyo shemeji,alikuwa ni mrembo balaa,mpaka nikawa nashangaa,inawezekana vipi,MTU mrembo namna hii,anaweza kuwa na roho mbaya kiasi kile,nikaapa kwamba IPO Siku nitapita nae,
Miaka mingi imepita,nimeishasahau maumivu,Shem wangu ni best yangu sana sasa HV.
Da tumetoka mbali.
 
Mlambe
 
pamoja na hayo yote ila kuna mema pia tunapata. Kama kupewa hifadhi na sehemu ya kuishi, kupelekwa shuleni na kupata elimu, pia zipo faida nyingi siwezi kuziandika zote. Cha muhimu tusipende kuangalia upande mmoja wa kero na tukasahau kuwa bila hao ndugu labda tusinge fika hapa. kuna wengine tulikuwa na wazazi ila tulilelewa na ndugu, je huoni kama hapo walitutakia mema?. So usipende kulalamika sana maana jukumu la kukuandalia maisha ni la baba yako na mama yako, kwa kuwa ndugu nao wana watoto wao ambao inabidi wapate maisha mazuri.
Ningekua na mamlaka nchi hii ningekupa uwaziri maana umeongea point tupu.
 
Nilianza kulelewa na ndugu wa upande wa baba angu, Nimemjua mama angu baada ya kupata akili zangu, nikagundua kinachosumbua watoto wanaolelewa na ndugu/mtu baki ni inferior complexity (psychological problems)ile hali ya kuhisi kuonewa onewa tu kwa kila jambo lakini ,(though wapo walezi wenye kuonea watoto wasio wao) ila mara nyingi mtoto asiye wako akili yake mda wote inawaza kuonewa onewa tu, ukimtuma kazi ataona kama umemuonea, akikosea ukamsema atafeel the same way, etc

Swali , Je hakuna wazazi wanaowapiga au kuwapa adhabu watoto zao??

[emoji1426][emoji1426]Hii akifanya mtu ambae sio mzazi wako utahisi 100% umeonewa na utalia sana tofauti na akikuadhibu mzazi wako baada ya muda utasahau.
Umeongea neno mkuu, mimi ni moja ya walio lelewa na ndugu nilikuaga na mawazo hayo lkn mwisho wa siku nimekuja kugundua pengine ulikua utoto tu . Kuna mazuri mengi wanatufanyia hawa ndg zetu we can remember that also.
 
Poleni sana mliopitia hayo. Mimi niliishi kwa miaka miwili na watu wasio ndugu zangu na wala hawakuwa na ukaribu ana uhusiano na familia yangu na mimi ni mkristo na wao ni waislam lakini nakiri kuwa mimi ndiye nilikuwa napendwa kuliko watoto wengine. Tulizoeana sana kiasi ilikuwa ngumu wao kuniruhusu niondoke nilipohitaji kufanya hivyo.
Watu wenye roho nzuri bado wapo
Mungu awajalie maisha marefu hao walezi wako[emoji120] [emoji120]
 
Aisee unanikumbusha mbali sana ndugu. Huwa sitaki nikumbuke kwa sababu hata sasa ninaandika, machozi yananilenga lenga nikiwa kijana wa kiume.

Nimelelewa na ndugu tofauti tofauti tangu nikiwa mdogo sana baada ya baba kufariki.
Mama hakuwa na upendo sana na watoto wake hivyo alitugawa kwa ndugu ila mimi ndo nililelewa na ndugu wengi.

Treatment niliyoipata, anajua Mungu tu.

Inafikia wakati unaambiwa unakula kama mchwa.

Leo hao waliokuwa wakinitreat hivyo ndo wanataka niwape hela.

Inauma sana.

Nimejifunza, sitaruhusu mke wangu anyanyase mtu yeyote.

Machungu yake ni mabaya sana na upendo hupotea
[emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Shukuru Mungu kwamba pamoja na hayo bado unaweza kuandika na kuifahamu hata JF.

Jifunze kushukuru zaidi ya kulaumu.

Ipo siku famili yako itakumbukwa kwa haya unayoyataka.
 
Mimi kwangu pia ilikuwa tofauti nilikaa kwa dingi mkubwa nikafukuzwa lakini nilipohamia kwa watu baki nilisoma kula na kuvaa vizur na hawakunibagua na mpaka picha yangu ya graduation wameweka sebuleni kwao much respect
 
Umeongea neno mkuu, mimi ni moja ya walio lelewa na ndugu nilikuaga na mawazo hayo lkn mwisho wa siku nimekuja kugundua pengine ulikua utoto tu . Kuna mazuri mengi wanatufanyia hawa ndg zetu we can remember that also.

For sure mkuu
 
Mimi baada ya kufaulu STD 7....mama wa kambo akafanya visa ili niondolewe nyumbani..baba akanichukuwa akanipeleka kwa mjomba wake,,ambaye mm namwita babu...nilikaa kuanzia form 1 hadi form 4.....muda wote huo baba alikuwa kila jioni anapitisha pesa ya chakula pale kwa MJOMBA ,,nakumbuka alikuwa anatoa kati ya sh 1000 na 2000 hyo ilikuwa mwaka 1991.......siku kama hajapita pale ujuwe ni deni kwake....na yule MJOMBA si kama alikuwa hafanyi kazi,,,alikuwa anafanya kazi bandarini kipindi hicho...kufika 1993 kampuni aliyokuwa anafanya baba iliuzwa na wafanyakazi walisitishiwa AJIRA ZAO.....hapo ndy VISA VILIVYOANZA kwa yule BABU....baada ya BABA kukosa pesa za kuleta pale nyumbani.....nilipata taabu sana....yule BABU alinifukuza pale nyumbani japokuwa ile nyumba ni ya family na BABA yngu pia inamuhusu,,lakini nilifukuzwa..nikawa nalala tu nje kwenye frem ya DUKA...au kwa friends tu..sometimes unakuta mshikaji yupo na demu wake..inabidi umsubiri hadi saa sita au saba wakimaliza mambo yao ndy na mm naingia kulala..... nikitaka kula nakwenda MIDIZINI MANZESE huko ndipo baba alipokuwa kapanga,,, baada ya baba kuachishwa kazi yule mama aliyokuwa anaishi nae alimkimbia...mzee akahama kule magomeni akahamia MIDIZINI MANZESE,,,,basi ikawa natoka magomeni kwa mguu napita border to border hadi manzese ..kwa siku nakwenda mara mbili...asubuhi na jioni..HEBU FIKIRIA NASOMA wakati huo nina kama miaka 15 tu,, mtu anakufanyia VISA HIVYO.. .sometimes BABA SIMKUTI....nikimkuta ndy nitakunywa chai,,, au nakula mchana,,,,nilipata taabu sana tu kwa mzee yule mjomba wa baba,,alikuwa ana search nyumba nzima ahakikishe mm silali mle ndani, ,MUNGU mkubwa baada ya kumaliza shule kwa shida sn,,,NDY SAFARI YA MWANAUME ikaanza....nilipambana sana hadi sasa hapa nilipo NAMSHUKURU MUNGU...leo hii yule MJOMBA wa baba anaishi VIBAYA SANA,,,watoto wake hawamsaidii...kuniomba mimi anashindwa,,kuna siku moja tulikutana kwenye SHUGHULI FULANI ya kifamilia alivyoniona akashangaa sana,,,akataka apaone ninapoishi,,ajiridhishe...,siku akaja kwangu ,,,ALISHANGAA SN....AKAANZA kulalamika sana juu ya watoto wake, na maisha anayoishi sasa,,nikafikiria sana hivi huyu mzee anakumbuka kweli aliyonitendea mimi nilimsaidia ...tena alilalamika hana SIMU NIKAMPA SMART PHONE..nzr tu..akalalamika habari ya KUPASHA CHAKULA,,, NIKAMPA NA MICROWAVE..MPYA KABISA...nilinunuwa south ...akaondoka navyo kwenda huko anapoishi sasa..na nilimpa kusudi ili akifika huko kwa MKEWE akimwambiya nimempa mimi VITU HIVYO,,,NDY WATAKUMBUSHANA VISA walivyonifanyia wakati nipo mdogo...MARA INGINE NAHISI ....maisha niliyoishi UTOTONI NDY YAMENIFUNDISHA LEO...KUPAMBANA.....tena mapambano ya USO KWA USO na ADUI...bila kupepesa macho...
 
Watu wengi hasa wanawake hawapendi na hunyanyasa ndugu. Watu ambao hawajawahi kuishi kwa ndugu hawawezi kuona haya. Niliishi miaka minne kwa ndugu sikufurahia kabisa maisha. Manyanyaso ya kijinga hadi watu wa nje wakawa wanasema tunajua we hapo unanyanyaswa.
 
Back
Top Bottom