Kwa wale tuliowahi kupika tukapika maboko.

Siku moja niliamka na hangover zangu, nikatoa lock kwanza then nikasema ngoja nitengeneze mchemsho.. Maana Aunty yenu huwa ananitengenezea mara moja moja akiwa amekuja ghetto nikiwa kama jana yake nimepiga vyombo vyangu

Kwakua akiwa anapika tunakuaga wote nikawa nasema mbona simple tu, basi nikatengeneza nyama yangu fresh mixer tangawizi na vitunguu swaumu nikaweka jikoni. Yale maji ya nyama yenyewe yalipokauka nikasema huu sasa ni wakati wa kutia viazi,hoho pamoja na carrot.

Kimbembe kimekuja hapa sasa[emoji28], viazi vimeiva tayari nyama bado ngumu, ikabidi niongeze maji ili nyama iive.. nikafunika nikawa busy na simu, kuja kufunua nilichokikuta uji wa viazi pamoja na nyama.[emoji28][emoji28]

Naomba niishie hapa.
 
Home walipika ugali nikagoma kula walivyoenda kulala usiku saa sita nikaamka ili nipike wali.

Nikawasha mkaa.

Nikaweka mchele maji mafuta nikafunika.

Harufu ya kuungua ikaanza. Sasa nashangaa kitu kinawezaje kuungua huku maji yanaonekana kwa mbali?

Mi nakazana kugeuza, kisha nikaona imetosha nikapalia kwa mkaa matokeo yake yakawa ni ubwabwa fulani hivi wenye mchele ulioungua mpaka ukawa mkaa.

Halafu mboga ilikua spinachi.

Hatari sana unakula klipsi na spinachi.
 
Mpaka Leo sijui kupika tambi na pilau
Haya mambo tuwaachie wanawake
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mikate ya Yesu mkuu kama nyingi naomba na mm

Natamani kuona chips za @figganiga [emoji23][emoji23] zilikuwaje
yupo humu tafuta uzi wake wa chips
 
[emoji23] [emoji23]
 
hahaha... wali unatabia mbovu saana unaungua huku juu haujaiva
 
Itabidi tubadili jina yaitwe maandazi ya nyama sio sambusa tena [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Mkuu naomba kupika hili wowowo lako[emoji13][emoji13]
 
Niliwahi kupika wali kwa rice cooker, baada ya kuiva nikashangaa nikipakua unanata sana kwenye kipakulio, nimeanza kula nashangaa tena unanata mbaya kwenye kijiko. Nimefika katikati kama sio mwishoni najagundua kua sikuweka mafuta kwenye chakula, hahahahah nilicheka mbaya
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hapo kwenye kula kidogo kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…