Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Sio kweli...mie nna miaka kumi toka nianze ujasiriamali...ukitaka ujimix nenda huko[emoji28]! Mie hata shipa la kuwaza kwenda huko halijawah amka
Mimi pia naamini hivyo, I wouldn't go to a witch ili tu niwe na pesa, kwanza pesa za namna hiyo hazina amani wala hazileti maendeleo. Pamoja na viajira vyetu uchwara bado tunajitahidi kuwekeza na hatuendi kwa waganga katu. My principle remains so!
 
Mie bahati mbaya au nzuri marafiki na baadhi ya ndugu zangu walienda kwenye hizo ndago...hha awakikuelezea utabaki kucheka ufe . mtot wa aunt alienda fata utajiri kigoma akaambiwa aoge nje ya mlango wake mchana kWeupee🤣! Kweli akawa tajiri btn 1998-2000 visiwani huko alikua title😅😅..akarudi kwenye umaskn baada ya kuambiwa inahitajika damu ya mwanae ya nn yote hiyo sasa
Hivi umegoma kunigawia Dagaa?
 
Mimi pia naamini hivyo, I wouldn't go to a witch ili tu niwe na pesa, kwanza pesa za namna hiyo hazina amani wala hazileti maendeleo. Pamoja na viajira vyetu uchwara bado tunajitahidi kuwekeza na hatuendi kwa waganga katu. My principle remains so!


Nisaidie laki moja hapo mtumishi!😅😅
 
Ila waganga wanajitahidi. Nilipeleka majina ya wanawake watatu na tarehe zao za kuzaliwa huwezi amini baada ya nusu saa akaniambia baki na huyu fulani wawili hawa watakuingiza matatizoni. Nikapiga mahesabu nikagundua kweli hao wawili kunammoja Kika siku kwao magonjwa tu, mara mama mara shangazi. Alafu mwingine huyo kama unamilioni ndani akukuomba hata elfu ishirini unajikuta mwezi mzima unaisha hela zinapotea potea tu. Nikamuuliza mganga nikulipe sh ngapi akasema 3000. Nikampa 5000 nikamwambia chenji baki nayo. Tangu siku hiyo sikurudi tena maana eneo lake lilikualinanuka ubani si ubani, daaah ila nishatubu kwa Mungu kitambo sana.
 
Mimi binafsi nimekulia kwenye familia ya dini. Na toka nipo mdogo , nilishawahi kukiri, hata itokee nini kwenye haya maisha, Siwezi kumuacha Bwana Yesu , Kwani yeye Ndio kila kitu kwangu , hakuna kinachomshinda.

Na siku zote nikiona mtu akizungumzia masuala ya kwenda kwa mganga Sijui nilikua namuonaje, yani nilikua nawaona waswahili, hawajenda shule na nilikua Naona wanapoteza muda kufanya huo upuuzi. Inshort nikikuona una mambo ya kishirikina nakutenga na kukukwepa kama ukoma.

Ila Maisha yana siri nzito sana, Na hapa duniani binadamu tumeumbiwa mitihani mizito sana, Mitihani ambayo unafikia hatua kabisa unakiri kwa nafsi yako Mungu hayupo, na kama yupo basi sio kwa ajili yako, Yupo kwa ajili ya watu wengine.

Nakumbuka nilipata changamoto za maisha, nilijitahidi kuomba na kufunga kutokana na dini yangu , kwa kweli nilisimama imara sana na Dini yangu , nilimwabudu Mungu katika roho na kweli. Kama nilivyosema, binadamu tumeumbiwa changamoto kubwa sana hapa duniani, kuna matatizo mengine yanakupelekea kufanya mambo ambayo toka uzaliwe hujawahi kufikiria kuwa utakuja kufanya. Nikatubu kwa Mungu na kuvunja laana zote za ukoo zinazonitesa, pia bado ikagonga mwamba .

Nilikata tamaa sana , niliomba na kulia kwa Mungu anisaidie lakini Mungu hakunisikia. Nikajiuliza Mungu kuna watu hawakujui wewe, hawana muda na nyumba za Ibada, na maisha yao wamejaa furaha tele, wanaishi maisha ya anasa, mambo yao yanawaendea vizuri, wanafanya uchafu wote hapa duniani, Mimi nimeamua kukukimbilia Wewe bado unaniaibisha, mpaka inafikia hatua watu wanakutukana Mungu wako yuko wapi ? unajifanya mlokole kila siku kanisani na mambo yako hayaeleweki.

Kwa kweli kama binadamu, ilifikia stage nikasema NIMECHOKA, Ndipo ikanibidi nitafute njia mbadala ya kuweza kutatua changamoto zangu Sugu iliyonisumbua kwa mda mrefu. Nakumbuka usiku nilioamua kuwa ngoja niende kwa mganga, nililia sana , Kwani nilikua sitaki kabisa kufanya hivyo, nililia kama mtoto mdogo. Ila nilivyomaliza kulia, uchungu wote ukaisha na sikujutia chochote kuhusu maisha yangu mapya niliyoamua kuyachagua.

Tofauti na watu wengine ambao huangaika huku na kule kutafuta waganga, Mimi naweza kusema nilipata bahati, Kwani nilipata rafiki ambayo alikua anafanya sana hayo mambo , so alikua anajua waganga wengi sana kuanzia kigoma, pemba, Mbeya , Tanga na sehem nyingine nyingi.

Sijui niseme ni shetani alikua ameniingia, wakati naenda kwa mganga kwa mara ya kwanza, moyo wangu ulijawa na furaha sana, na nilikua nimeshaamini kuwa ntaenda kufanikiwa Tatizo langu . Yani moyo ulikua mwepesi na kujisemea pengine huku Ndipo nilipotakiwa kwenda miaka yote hiyo, Sijui kwa nini nilikua napoteza mda kwenda kanisani.

Basi safari yangu ya kwenda kwa waganga ikaanzia hapo, na niseme tu , mambo yangu kweli yalibadilika, na kwenda kwa waganga ndo ikawa kama fashion kwangu. Na niweze kusema tu toka nimeanza kujihusisha na ushirikina ni miaka mitatu sasa , na hakuna hata siku ambayo nimewahi kujuta wala kutamani nilipotoka.

Je na wewe ilikuaje mara yako ya kwanza kwenda kwa waganga? Nini kilikusukuma?View attachment 1431306View attachment 1431307View attachment 1431308




Sent from my iPhone using JamiiForums
biashara matangazo.
 
Back
Top Bottom