Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Ufunuo 2:5
Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ufunuo 2:5
Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Naijua biblia kama kiganja cha mkono wangu , huko huniwezi pia, ila Niko sehem nyingine sasa, ambayo pia na kwenyewe nako huniwezi


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Dah!nimecheka kama chizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yangu inafanana na yako.
Nimewahi kuwa na rafiki wa kuaminika sana.Ni mchapakazi kwelikweli na anajituma.
Katika biashara zetu yeye alikua anaenda kuloga mana uncle wake ni mganga.Ila mimi nilikua nagoma.Kwa kiasi flani tulikua tunafanikiwa.
Miaka kadhaa nikapata ajira.Nikaachana na biashara....stori isiwe ndefu

Alinipeleka kwa mganga zikapigwa ramli pale na blah blah blah nyingi.Nikaacha pesa ya kununua madawa ili nirudi week inayofata.

Hata week ya kuaguliwa haikufika nikapigiwa simu ya kazi.

Sasa kama angeniagua ndio nikapata hio kazi hadi leo ningekua naamin ushirikina.

Sikuwai kwenda tena hadi leo ni miaka 8 sasa na mambo yangu yako sawia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fungua uzi wako mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania sie hatujambo kwa unafiki,yaani ukizisoma comments utahisi kuwa jamii yetu ni ya wacha Mungu haswaaa wasiojua waganga ila ukweli 85% ya waliokoment ooh mi sijawahi sijui nyenyenye ni wazoefu na wanaojua machimbo ya waganga tena wale wa ndani ndani...

Mi ht sijui km kuna mganga asiyenifahamu Tanzania hii full stop maswali sitaki.[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nilikuwa kwenye daladala basi kulikuwa kuna jamaa mmoja anaongea balaa.

Akawa anasema ukisikia mtu anasema hajawahi kwenda kwa mganga ujue 'Hajapata shida huyo au hajaugua'

Nikajaribu kufikiria, nikaona alikuwa sahihi kabisa.

Mtu akiugua kabisa akakosa tumaini au akipata matatizo mfululizo yasiyo na kikomo kichwani kwake anachotamani ni SULUHISHO tuu haijalishi atalipata kwa nani hata kama nikwa shetani LIVE !!!

------------------------------------

Binafsi kuna jamaa yangu alikuwa na ukumbi wa kuonesha Movie ( Kibanda umiza ) na kwa kuwa vilikuwa vingi akasema twende kwa mganga. Tukaenda, sema mimi nilienda kwa basi tu wala sikuwa nkiamini kama anasaidia maana nawachukulia kama matapeli. Basi akatupa dawa ya kuchoma moshi unatoka kabla ya kufungua.

Jamaa akawa anafanya kila siku.
 
Hii ilitokea kwa jirani yaani ana jumba nzuri ukipita lazima utowe macho, Siku moja mchawi alinasa ndani ya geti wanapopaki magari yao, mbibi yupo uchi asubuhi watu wanapita, watu wakajaa, huyo mbibi sio wa mbali alikuja kutolewa saa 3 asubuhi, ilikuwa aibu sana.
 
Waganga wote wanamwamini Mungu sijawahi kutana na hata mmoja anaekataa nguvu ya Mungu. Kuna wazuri na wabaya kama walivyo masheikh na mapadri wazinzi na waovu. Wengi wanasaidia ndio maana bado wapo. Nawajua mpaka maaskofu wanaokwenda kwa waganga. Kama huamini acha wanaoamini usiwaonee wivu. Mshana Jnr nielekeze kilingeni nijee.
 
Yanawahi ila HAYADUMU na YANACOST SANA MAISHA.

Nina mifano mitatu mikubwa ya wazi hapa jirani kabisa na nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwahi kuendewa Kwa mganga na mtu aisee hii dunia ni nzuri niliteseka miaka miwili bila kujua ila nilikuja kupata ufumbuzi wa matatizo na uchawi niliofanyiwa Kwa siku moja tuu kweli Mungu yupo


Sent using Jamii Forums mobile app
Ilikuwaje ndugu tuelezee kiundani nini kilikuwa chanzo na lipi lilisababisha akakufanyia hivyo? Pia uliteseka kivipi.? Nataka tujifunze jambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2016 KULIKUWA NA UZI HAPA UNASEMA ULIZA CHOCHOTE KUHUSU UCHAWI....
NIKIUSOMA WOTE..NIKAENDA PM.NIKAENDA ARUSHA NIKAPEWA DAWA TATIZO NDO LIKAZIDI...HALAFU KUNA NDUGU YANGU ALIUGUA USIKU AISEEE NIKAHIS NACHEZEWA ..HAYA MAMBO BWANA..
TANGU HAPO NILIACHANA NA HIZO MAMBO...MR jooohs COME HAPA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…