Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Ufunuo 2:5
Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.
Mimi binafsi nimekulia kwenye familia ya dini. Na toka nipo mdogo , nilishawahi kukiri, hata itokee nini kwenye haya maisha, Siwezi kumuacha Bwana Yesu , Kwani yeye Ndio kila kitu kwangu , hakuna kinachomshinda.

Na siku zote nikiona mtu akizungumzia masuala ya kwenda kwa mganga Sijui nilikua namuonaje, yani nilikua nawaona waswahili, hawajenda shule na nilikua Naona wanapoteza muda kufanya huo upuuzi. Inshort nikikuona una mambo ya kishirikina nakutenga na kukukwepa kama ukoma.

Ila Maisha yana siri nzito sana, Na hapa duniani binadamu tumeumbiwa mitihani mizito sana, Mitihani ambayo unafikia hatua kabisa unakiri kwa nafsi yako Mungu hayupo, na kama yupo basi sio kwa ajili yako, Yupo kwa ajili ya watu wengine.

Nakumbuka nilipata changamoto za maisha, nilijitahidi kuomba na kufunga kutokana na dini yangu , kwa kweli nilisimama imara sana na Dini yangu , nilimwabudu Mungu katika roho na kweli. Kama nilivyosema, binadamu tumeumbiwa changamoto kubwa sana hapa duniani, kuna matatizo mengine yanakupelekea kufanya mambo ambayo toka uzaliwe hujawahi kufikiria kuwa utakuja kufanya. Nikatubu kwa Mungu na kuvunja laana zote za ukoo zinazonitesa, pia bado ikagonga mwamba .

Nilikata tamaa sana , niliomba na kulia kwa Mungu anisaidie lakini Mungu hakunisikia. Nikajiuliza Mungu kuna watu hawakujui wewe, hawana muda na nyumba za Ibada, na maisha yao wamejaa furaha tele, wanaishi maisha ya anasa, mambo yao yanawaendea vizuri, wanafanya uchafu wote hapa duniani, Mimi nimeamua kukukimbilia Wewe bado unaniaibisha, mpaka inafikia hatua watu wanakutukana Mungu wako yuko wapi ? unajifanya mlokole kila siku kanisani na mambo yako hayaeleweki.

Kwa kweli kama binadamu, ilifikia stage nikasema NIMECHOKA, Ndipo ikanibidi nitafute njia mbadala ya kuweza kutatua changamoto zangu Sugu iliyonisumbua kwa mda mrefu. Nakumbuka usiku nilioamua kuwa ngoja niende kwa mganga, nililia sana , Kwani nilikua sitaki kabisa kufanya hivyo, nililia kama mtoto mdogo. Ila nilivyomaliza kulia, uchungu wote ukaisha na sikujutia chochote kuhusu maisha yangu mapya niliyoamua kuyachagua.

Tofauti na watu wengine ambao huangaika huku na kule kutafuta waganga, Mimi naweza kusema nilipata bahati, Kwani nilipata rafiki ambayo alikua anafanya sana hayo mambo , so alikua anajua waganga wengi sana kuanzia kigoma, pemba, Mbeya , Tanga na sehem nyingine nyingi.

Sijui niseme ni shetani alikua ameniingia, wakati naenda kwa mganga kwa mara ya kwanza, moyo wangu ulijawa na furaha sana, na nilikua nimeshaamini kuwa ntaenda kufanikiwa Tatizo langu . Yani moyo ulikua mwepesi na kujisemea pengine huku Ndipo nilipotakiwa kwenda miaka yote hiyo, Sijui kwa nini nilikua napoteza mda kwenda kanisani.

Basi safari yangu ya kwenda kwa waganga ikaanzia hapo, na niseme tu , mambo yangu kweli yalibadilika, na kwenda kwa waganga ndo ikawa kama fashion kwangu. Na niweze kusema tu toka nimeanza kujihusisha na ushirikina ni miaka mitatu sasa , na hakuna hata siku ambayo nimewahi kujuta wala kutamani nilipotoka.

Je na wewe ilikuaje mara yako ya kwanza kwenda kwa waganga? Nini kilikusukuma?View attachment 1431306View attachment 1431307View attachment 1431308

Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naijua biblia kama kiganja cha mkono wangu , huko huniwezi pia, ila Niko sehem nyingine sasa, ambayo pia na kwenyewe nako huniwezi

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna rafki yangu alimtia mimba mwanafunzi....eehh mwanafunzi kipindi Cha magufuli ichi ichi dodoma katika mji fulani....basi acha wazazi na mkuu wa shule + mratibu wakachachamaa wanataka mtu aende jela..... solution ya kwanza mwamba ikabidi akimbie mji akaenda kwa baba ake Tanga....kufika kule akaeleza yaliyomtokea....baba ake akampeleka kwa mtaalamu..kijana akafanyiwa ufundi wa viwango vya SGR,,,basi after one week akarudi mjini,,,,uku anawasiwasi...tukamuuliza mzee hujitaki wadau walikua wanakusaka Kama Ruby mzee,,akasema nimepikwa kwa fundi uko na akatuhakikishia kua tutaona miujiza,,,,,basi ikapita siku ya kwanza simu ya pili akapigiwa simu na mama mwenye mtoto... kubabake...ikabid atuonyeshe wajuba...tukamwambia pokea...maana simu haitamfanya akamatwe papo kwa papo...alivopokea...uyo mama aliongea kwa upole utafkiri katekwa...akasema mwanangu Aya mambo ya kawaida .watu wanataka kutuchonganisha..njoo nyumbani tuyajenge...mmmh wajuba tukamwambia unaeza kua mtego maana mganga wako hatumuamini...mwamba akamwambia yule bi mkubwa kua ana mashaka na usalama wake,,,,bi mkubwa akamwambia yashaisha...basi akamwambia ataenda keshokutwa..hii ilikua lengo tukachunguze ili mjuba asishikwe....siku ya pili acha yule Mama akawape kichambo mwalimu mkuu na mratibu kua yule mtoto ni wake hivo wasifatilie mambo yasiyowahusu,,jioni baba mwenye nyumba akaenda kumuwakia mkuu wa shule kua ajikite kwenye kusimamia walimu wake na sio mtoto wake mmoja aliepewa mimba...mkuu wa shule akachokaa...maana Ni wiki tu walikua bega kwa bega kumtafta mhalifu...tulivoskia ivo visa tukamwambia mjuba tia maguu sir tutakua around incase limetokea lolote....basi siku ilipotimia jamaa kutia miguu Yani walimpokea utafkiri nabii na kuku akachinjiwa ..akaombwa msamaha kwa usumbufu waliompa... jamaa akastaajabu...basi Ni miaka 4 Sasa na jamaa alimuo yule binti na Wana watoto wawili now.....waganga wa Tanga kwa kweli mmenishinda tabia[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
Dah!nimecheka kama chizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nakumbuka nilikua nmemaliza chuo nshakaa mwaka bila kazi...siku hiyo katika cv nilizopeleka nkasikia nmeitwa interview....nmekaa zangu kijiweni jamaa akanijia anasema anipeleke kwa mzee wangu tukawafunge macho watahini nipate kazi...siku hiyo ilikua ngumu sana maana ndo golden chance sitaki ipoteza..ila kilichonizuia ni toka nazaliwa sijawahi ona wazazi wanaongelea hilo swala...kesho yake nikaenda kwe interview na kupita...sasa nawaza tu kama ningemuamini yule mtu nadhan mda huu ningekua nishawajua vigagula wote mjini....Tusimame katika Yesu yeye hashindwi
Yangu inafanana na yako.
Nimewahi kuwa na rafiki wa kuaminika sana.Ni mchapakazi kwelikweli na anajituma.
Katika biashara zetu yeye alikua anaenda kuloga mana uncle wake ni mganga.Ila mimi nilikua nagoma.Kwa kiasi flani tulikua tunafanikiwa.
Miaka kadhaa nikapata ajira.Nikaachana na biashara....stori isiwe ndefu

Alinipeleka kwa mganga zikapigwa ramli pale na blah blah blah nyingi.Nikaacha pesa ya kununua madawa ili nirudi week inayofata.

Hata week ya kuaguliwa haikufika nikapigiwa simu ya kazi.

Sasa kama angeniagua ndio nikapata hio kazi hadi leo ningekua naamin ushirikina.

Sikuwai kwenda tena hadi leo ni miaka 8 sasa na mambo yangu yako sawia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ntakufa na shida zangu, kwa mganga siendi kamwe! Mungu asiponiijilia katika shida zangu potelea mbali,

ZABURI 118
5 Katika shida yangu nalimwita BWANA;
BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi.
6 BWANA yuko upande wangu, sitaogopa;
Mwanadamu atanitenda nini?
7 BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu,
Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.
8 Ni heri kumkimbilia BWANA
Kuliko kuwatumainia wanadamu.
9 Ni heri kumkimbilia BWANA.
Kuliko kuwatumainia wakuu.

mleta uzi hujawahi kuwa mkristo wewe ni mshirikina tangu awali unatafuta watu wa kuwapotosha
Fungua uzi wako mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania sie hatujambo kwa unafiki,yaani ukizisoma comments utahisi kuwa jamii yetu ni ya wacha Mungu haswaaa wasiojua waganga ila ukweli 85% ya waliokoment ooh mi sijawahi sijui nyenyenye ni wazoefu na wanaojua machimbo ya waganga tena wale wa ndani ndani...

Mi ht sijui km kuna mganga asiyenifahamu Tanzania hii full stop maswali sitaki.[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi binafsi nimekulia kwenye familia ya dini. Na toka nipo mdogo , nilishawahi kukiri, hata itokee nini kwenye haya maisha, Siwezi kumuacha Bwana Yesu , Kwani yeye Ndio kila kitu kwangu , hakuna kinachomshinda.

Na siku zote nikiona mtu akizungumzia masuala ya kwenda kwa mganga Sijui nilikua namuonaje, yani nilikua nawaona waswahili, hawajenda shule na nilikua Naona wanapoteza muda kufanya huo upuuzi. Inshort nikikuona una mambo ya kishirikina nakutenga na kukukwepa kama ukoma.

Ila Maisha yana siri nzito sana, Na hapa duniani binadamu tumeumbiwa mitihani mizito sana, Mitihani ambayo unafikia hatua kabisa unakiri kwa nafsi yako Mungu hayupo, na kama yupo basi sio kwa ajili yako, Yupo kwa ajili ya watu wengine.

Nakumbuka nilipata changamoto za maisha, nilijitahidi kuomba na kufunga kutokana na dini yangu , kwa kweli nilisimama imara sana na Dini yangu , nilimwabudu Mungu katika roho na kweli. Kama nilivyosema, binadamu tumeumbiwa changamoto kubwa sana hapa duniani, kuna matatizo mengine yanakupelekea kufanya mambo ambayo toka uzaliwe hujawahi kufikiria kuwa utakuja kufanya. Nikatubu kwa Mungu na kuvunja laana zote za ukoo zinazonitesa, pia bado ikagonga mwamba .

Nilikata tamaa sana , niliomba na kulia kwa Mungu anisaidie lakini Mungu hakunisikia. Nikajiuliza Mungu kuna watu hawakujui wewe, hawana muda na nyumba za Ibada, na maisha yao wamejaa furaha tele, wanaishi maisha ya anasa, mambo yao yanawaendea vizuri, wanafanya uchafu wote hapa duniani, Mimi nimeamua kukukimbilia Wewe bado unaniaibisha, mpaka inafikia hatua watu wanakutukana Mungu wako yuko wapi ? unajifanya mlokole kila siku kanisani na mambo yako hayaeleweki.

Kwa kweli kama binadamu, ilifikia stage nikasema NIMECHOKA, Ndipo ikanibidi nitafute njia mbadala ya kuweza kutatua changamoto zangu Sugu iliyonisumbua kwa mda mrefu. Nakumbuka usiku nilioamua kuwa ngoja niende kwa mganga, nililia sana , Kwani nilikua sitaki kabisa kufanya hivyo, nililia kama mtoto mdogo. Ila nilivyomaliza kulia, uchungu wote ukaisha na sikujutia chochote kuhusu maisha yangu mapya niliyoamua kuyachagua.

Tofauti na watu wengine ambao huangaika huku na kule kutafuta waganga, Mimi naweza kusema nilipata bahati, Kwani nilipata rafiki ambayo alikua anafanya sana hayo mambo , so alikua anajua waganga wengi sana kuanzia kigoma, pemba, Mbeya , Tanga na sehem nyingine nyingi.

Sijui niseme ni shetani alikua ameniingia, wakati naenda kwa mganga kwa mara ya kwanza, moyo wangu ulijawa na furaha sana, na nilikua nimeshaamini kuwa ntaenda kufanikiwa Tatizo langu . Yani moyo ulikua mwepesi na kujisemea pengine huku Ndipo nilipotakiwa kwenda miaka yote hiyo, Sijui kwa nini nilikua napoteza mda kwenda kanisani.

Basi safari yangu ya kwenda kwa waganga ikaanzia hapo, na niseme tu , mambo yangu kweli yalibadilika, na kwenda kwa waganga ndo ikawa kama fashion kwangu. Na niweze kusema tu toka nimeanza kujihusisha na ushirikina ni miaka mitatu sasa , na hakuna hata siku ambayo nimewahi kujuta wala kutamani nilipotoka.

Je na wewe ilikuaje mara yako ya kwanza kwenda kwa waganga? Nini kilikusukuma?View attachment 1431306View attachment 1431307View attachment 1431308

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kuna siku nilikuwa kwenye daladala basi kulikuwa kuna jamaa mmoja anaongea balaa.

Akawa anasema ukisikia mtu anasema hajawahi kwenda kwa mganga ujue 'Hajapata shida huyo au hajaugua'

Nikajaribu kufikiria, nikaona alikuwa sahihi kabisa.

Mtu akiugua kabisa akakosa tumaini au akipata matatizo mfululizo yasiyo na kikomo kichwani kwake anachotamani ni SULUHISHO tuu haijalishi atalipata kwa nani hata kama nikwa shetani LIVE !!!

------------------------------------

Binafsi kuna jamaa yangu alikuwa na ukumbi wa kuonesha Movie ( Kibanda umiza ) na kwa kuwa vilikuwa vingi akasema twende kwa mganga. Tukaenda, sema mimi nilienda kwa basi tu wala sikuwa nkiamini kama anasaidia maana nawachukulia kama matapeli. Basi akatupa dawa ya kuchoma moshi unatoka kabla ya kufungua.

Jamaa akawa anafanya kila siku.
 
Mkuu hiyo inatokea sana huku Usukumani, unakuta Ng'wana Luhanya ameenda kuloga usiku kumbe jamaa limezindika ile nyumba, anajifalaguafalagua mpaka kunakucha yuko hapo hapo na masempele yake. Mpaka mwenye nyumba anaamka! Sasa hapo nikiamua kumfanyia mauaji?
Hii ilitokea kwa jirani yaani ana jumba nzuri ukipita lazima utowe macho, Siku moja mchawi alinasa ndani ya geti wanapopaki magari yao, mbibi yupo uchi asubuhi watu wanapita, watu wakajaa, huyo mbibi sio wa mbali alikuja kutolewa saa 3 asubuhi, ilikuwa aibu sana.
 
Waganga wote wanamwamini Mungu sijawahi kutana na hata mmoja anaekataa nguvu ya Mungu. Kuna wazuri na wabaya kama walivyo masheikh na mapadri wazinzi na waovu. Wengi wanasaidia ndio maana bado wapo. Nawajua mpaka maaskofu wanaokwenda kwa waganga. Kama huamini acha wanaoamini usiwaonee wivu. Mshana Jnr nielekeze kilingeni nijee.
 
Duuh..sijawahi kukanyaga huko hata siku moja..Mungu kweli anasaidia magumu mengi nimepitia lakini huko bado sijafika...ila kuna jambo moja la kuweka wazi mara nyingi mambo ya Mungu yanachelewa ila ya giza hua yanawahi sana ila kama vile Mungu anavyosema yeye hua hawahi wala hachelewi..
Yanawahi ila HAYADUMU na YANACOST SANA MAISHA.

Nina mifano mitatu mikubwa ya wazi hapa jirani kabisa na nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwahi kuendewa Kwa mganga na mtu aisee hii dunia ni nzuri niliteseka miaka miwili bila kujua ila nilikuja kupata ufumbuzi wa matatizo na uchawi niliofanyiwa Kwa siku moja tuu kweli Mungu yupo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ilikuwaje ndugu tuelezee kiundani nini kilikuwa chanzo na lipi lilisababisha akakufanyia hivyo? Pia uliteseka kivipi.? Nataka tujifunze jambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2016 KULIKUWA NA UZI HAPA UNASEMA ULIZA CHOCHOTE KUHUSU UCHAWI....
NIKIUSOMA WOTE..NIKAENDA PM.NIKAENDA ARUSHA NIKAPEWA DAWA TATIZO NDO LIKAZIDI...HALAFU KUNA NDUGU YANGU ALIUGUA USIKU AISEEE NIKAHIS NACHEZEWA ..HAYA MAMBO BWANA..
TANGU HAPO NILIACHANA NA HIZO MAMBO...MR jooohs COME HAPA
 
Back
Top Bottom