Juliusmujungu
Senior Member
- Mar 21, 2020
- 115
- 106
Mganga anachukua pesa halali,wewe anakupa manyau nyau yakakutese[emoji848]
Sent from my iPhone using JamiiForums
Sent from my iPhone using JamiiForums
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi binafsi nimekulia kwenye familia ya dini. Na toka nipo mdogo , nilishawahi kukiri, hata itokee nini kwenye haya maisha, Siwezi kumuacha Bwana Yesu , Kwani yeye Ndio kila kitu kwangu , hakuna kinachomshinda.
Na siku zote nikiona mtu akizungumzia masuala ya kwenda kwa mganga Sijui nilikua namuonaje, yani nilikua nawaona waswahili, hawajenda shule na nilikua Naona wanapoteza muda kufanya huo upuuzi. Inshort nikikuona una mambo ya kishirikina nakutenga na kukukwepa kama ukoma.
Ila Maisha yana siri nzito sana, Na hapa duniani binadamu tumeumbiwa mitihani mizito sana, Mitihani ambayo unafikia hatua kabisa unakiri kwa nafsi yako Mungu hayupo, na kama yupo basi sio kwa ajili yako, Yupo kwa ajili ya watu wengine.
Nakumbuka nilipata changamoto za maisha, nilijitahidi kuomba na kufunga kutokana na dini yangu , kwa kweli nilisimama imara sana na Dini yangu , nilimwabudu Mungu katika roho na kweli. Kama nilivyosema, binadamu tumeumbiwa changamoto kubwa sana hapa duniani, kuna matatizo mengine yanakupelekea kufanya mambo ambayo toka uzaliwe hujawahi kufikiria kuwa utakuja kufanya. Nikatubu kwa Mungu na kuvunja laana zote za ukoo zinazonitesa, pia bado ikagonga mwamba .
Nilikata tamaa sana , niliomba na kulia kwa Mungu anisaidie lakini Mungu hakunisikia. Nikajiuliza Mungu kuna watu hawakujui wewe, hawana muda na nyumba za Ibada, na maisha yao wamejaa furaha tele, wanaishi maisha ya anasa, mambo yao yanawaendea vizuri, wanafanya uchafu wote hapa duniani, Mimi nimeamua kukukimbilia Wewe bado unaniaibisha, mpaka inafikia hatua watu wanakutukana Mungu wako yuko wapi ? unajifanya mlokole kila siku kanisani na mambo yako hayaeleweki.
Kwa kweli kama binadamu, ilifikia stage nikasema NIMECHOKA, Ndipo ikanibidi nitafute njia mbadala ya kuweza kutatua changamoto zangu Sugu iliyonisumbua kwa mda mrefu. Nakumbuka usiku nilioamua kuwa ngoja niende kwa mganga, nililia sana , Kwani nilikua sitaki kabisa kufanya hivyo, nililia kama mtoto mdogo. Ila nilivyomaliza kulia, uchungu wote ukaisha na sikujutia chochote kuhusu maisha yangu mapya niliyoamua kuyachagua.
Tofauti na watu wengine ambao huangaika huku na kule kutafuta waganga, Mimi naweza kusema nilipata bahati, Kwani nilipata rafiki ambayo alikua anafanya sana hayo mambo , so alikua anajua waganga wengi sana kuanzia kigoma, pemba, Mbeya , Tanga na sehem nyingine nyingi.
Sijui niseme ni shetani alikua ameniingia, wakati naenda kwa mganga kwa mara ya kwanza, moyo wangu ulijawa na furaha sana, na nilikua nimeshaamini kuwa ntaenda kufanikiwa Tatizo langu . Yani moyo ulikua mwepesi na kujisemea pengine huku Ndipo nilipotakiwa kwenda miaka yote hiyo, Sijui kwa nini nilikua napoteza mda kwenda kanisani.
Basi safari yangu ya kwenda kwa waganga ikaanzia hapo, na niseme tu , mambo yangu kweli yalibadilika, na kwenda kwa waganga ndo ikawa kama fashion kwangu. Na niweze kusema tu toka nimeanza kujihusisha na ushirikina ni miaka mitatu sasa , na hakuna hata siku ambayo nimewahi kujuta wala kutamani nilipotoka.
Je na wewe ilikuaje mara yako ya kwanza kwenda kwa waganga? Nini kilikusukuma?View attachment 1431306View attachment 1431307View attachment 1431308
Sent from my iPhone using JamiiForums
Ufunuo 2:5
Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Dah!nimecheka kama chizi.Kuna rafki yangu alimtia mimba mwanafunzi....eehh mwanafunzi kipindi Cha magufuli ichi ichi dodoma katika mji fulani....basi acha wazazi na mkuu wa shule + mratibu wakachachamaa wanataka mtu aende jela..... solution ya kwanza mwamba ikabidi akimbie mji akaenda kwa baba ake Tanga....kufika kule akaeleza yaliyomtokea....baba ake akampeleka kwa mtaalamu..kijana akafanyiwa ufundi wa viwango vya SGR,,,basi after one week akarudi mjini,,,,uku anawasiwasi...tukamuuliza mzee hujitaki wadau walikua wanakusaka Kama Ruby mzee,,akasema nimepikwa kwa fundi uko na akatuhakikishia kua tutaona miujiza,,,,,basi ikapita siku ya kwanza simu ya pili akapigiwa simu na mama mwenye mtoto... kubabake...ikabid atuonyeshe wajuba...tukamwambia pokea...maana simu haitamfanya akamatwe papo kwa papo...alivopokea...uyo mama aliongea kwa upole utafkiri katekwa...akasema mwanangu Aya mambo ya kawaida .watu wanataka kutuchonganisha..njoo nyumbani tuyajenge...mmmh wajuba tukamwambia unaeza kua mtego maana mganga wako hatumuamini...mwamba akamwambia yule bi mkubwa kua ana mashaka na usalama wake,,,,bi mkubwa akamwambia yashaisha...basi akamwambia ataenda keshokutwa..hii ilikua lengo tukachunguze ili mjuba asishikwe....siku ya pili acha yule Mama akawape kichambo mwalimu mkuu na mratibu kua yule mtoto ni wake hivo wasifatilie mambo yasiyowahusu,,jioni baba mwenye nyumba akaenda kumuwakia mkuu wa shule kua ajikite kwenye kusimamia walimu wake na sio mtoto wake mmoja aliepewa mimba...mkuu wa shule akachokaa...maana Ni wiki tu walikua bega kwa bega kumtafta mhalifu...tulivoskia ivo visa tukamwambia mjuba tia maguu sir tutakua around incase limetokea lolote....basi siku ilipotimia jamaa kutia miguu Yani walimpokea utafkiri nabii na kuku akachinjiwa ..akaombwa msamaha kwa usumbufu waliompa... jamaa akastaajabu...basi Ni miaka 4 Sasa na jamaa alimuo yule binti na Wana watoto wawili now.....waganga wa Tanga kwa kweli mmenishinda tabia[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
Yangu inafanana na yako.nakumbuka nilikua nmemaliza chuo nshakaa mwaka bila kazi...siku hiyo katika cv nilizopeleka nkasikia nmeitwa interview....nmekaa zangu kijiweni jamaa akanijia anasema anipeleke kwa mzee wangu tukawafunge macho watahini nipate kazi...siku hiyo ilikua ngumu sana maana ndo golden chance sitaki ipoteza..ila kilichonizuia ni toka nazaliwa sijawahi ona wazazi wanaongelea hilo swala...kesho yake nikaenda kwe interview na kupita...sasa nawaza tu kama ningemuamini yule mtu nadhan mda huu ningekua nishawajua vigagula wote mjini....Tusimame katika Yesu yeye hashindwi
Fungua uzi wako mkuu.Ntakufa na shida zangu, kwa mganga siendi kamwe! Mungu asiponiijilia katika shida zangu potelea mbali,
ZABURI 118
5 Katika shida yangu nalimwita BWANA;
BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi.
6 BWANA yuko upande wangu, sitaogopa;
Mwanadamu atanitenda nini?
7 BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu,
Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.
8 Ni heri kumkimbilia BWANA
Kuliko kuwatumainia wanadamu.
9 Ni heri kumkimbilia BWANA.
Kuliko kuwatumainia wakuu.
mleta uzi hujawahi kuwa mkristo wewe ni mshirikina tangu awali unatafuta watu wa kuwapotosha
Kwa msisiri HandeniWaliowahi kuja Msata Kilingeni wajitokeze hapa [emoji144][emoji144][emoji144]
Jr[emoji769]
KabisaKweli mkuu, honesty is the best policy. Kama ni mjasiriamali fuata ethics na principles zote za ujasiriamali, ukiteleza tizama ulipojikwaa otherwise Nature itakuumbua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna siku nilikuwa kwenye daladala basi kulikuwa kuna jamaa mmoja anaongea balaa.Mimi binafsi nimekulia kwenye familia ya dini. Na toka nipo mdogo , nilishawahi kukiri, hata itokee nini kwenye haya maisha, Siwezi kumuacha Bwana Yesu , Kwani yeye Ndio kila kitu kwangu , hakuna kinachomshinda.
Na siku zote nikiona mtu akizungumzia masuala ya kwenda kwa mganga Sijui nilikua namuonaje, yani nilikua nawaona waswahili, hawajenda shule na nilikua Naona wanapoteza muda kufanya huo upuuzi. Inshort nikikuona una mambo ya kishirikina nakutenga na kukukwepa kama ukoma.
Ila Maisha yana siri nzito sana, Na hapa duniani binadamu tumeumbiwa mitihani mizito sana, Mitihani ambayo unafikia hatua kabisa unakiri kwa nafsi yako Mungu hayupo, na kama yupo basi sio kwa ajili yako, Yupo kwa ajili ya watu wengine.
Nakumbuka nilipata changamoto za maisha, nilijitahidi kuomba na kufunga kutokana na dini yangu , kwa kweli nilisimama imara sana na Dini yangu , nilimwabudu Mungu katika roho na kweli. Kama nilivyosema, binadamu tumeumbiwa changamoto kubwa sana hapa duniani, kuna matatizo mengine yanakupelekea kufanya mambo ambayo toka uzaliwe hujawahi kufikiria kuwa utakuja kufanya. Nikatubu kwa Mungu na kuvunja laana zote za ukoo zinazonitesa, pia bado ikagonga mwamba .
Nilikata tamaa sana , niliomba na kulia kwa Mungu anisaidie lakini Mungu hakunisikia. Nikajiuliza Mungu kuna watu hawakujui wewe, hawana muda na nyumba za Ibada, na maisha yao wamejaa furaha tele, wanaishi maisha ya anasa, mambo yao yanawaendea vizuri, wanafanya uchafu wote hapa duniani, Mimi nimeamua kukukimbilia Wewe bado unaniaibisha, mpaka inafikia hatua watu wanakutukana Mungu wako yuko wapi ? unajifanya mlokole kila siku kanisani na mambo yako hayaeleweki.
Kwa kweli kama binadamu, ilifikia stage nikasema NIMECHOKA, Ndipo ikanibidi nitafute njia mbadala ya kuweza kutatua changamoto zangu Sugu iliyonisumbua kwa mda mrefu. Nakumbuka usiku nilioamua kuwa ngoja niende kwa mganga, nililia sana , Kwani nilikua sitaki kabisa kufanya hivyo, nililia kama mtoto mdogo. Ila nilivyomaliza kulia, uchungu wote ukaisha na sikujutia chochote kuhusu maisha yangu mapya niliyoamua kuyachagua.
Tofauti na watu wengine ambao huangaika huku na kule kutafuta waganga, Mimi naweza kusema nilipata bahati, Kwani nilipata rafiki ambayo alikua anafanya sana hayo mambo , so alikua anajua waganga wengi sana kuanzia kigoma, pemba, Mbeya , Tanga na sehem nyingine nyingi.
Sijui niseme ni shetani alikua ameniingia, wakati naenda kwa mganga kwa mara ya kwanza, moyo wangu ulijawa na furaha sana, na nilikua nimeshaamini kuwa ntaenda kufanikiwa Tatizo langu . Yani moyo ulikua mwepesi na kujisemea pengine huku Ndipo nilipotakiwa kwenda miaka yote hiyo, Sijui kwa nini nilikua napoteza mda kwenda kanisani.
Basi safari yangu ya kwenda kwa waganga ikaanzia hapo, na niseme tu , mambo yangu kweli yalibadilika, na kwenda kwa waganga ndo ikawa kama fashion kwangu. Na niweze kusema tu toka nimeanza kujihusisha na ushirikina ni miaka mitatu sasa , na hakuna hata siku ambayo nimewahi kujuta wala kutamani nilipotoka.
Je na wewe ilikuaje mara yako ya kwanza kwenda kwa waganga? Nini kilikusukuma?View attachment 1431306View attachment 1431307View attachment 1431308
Sent from my iPhone using JamiiForums
Hii ilitokea kwa jirani yaani ana jumba nzuri ukipita lazima utowe macho, Siku moja mchawi alinasa ndani ya geti wanapopaki magari yao, mbibi yupo uchi asubuhi watu wanapita, watu wakajaa, huyo mbibi sio wa mbali alikuja kutolewa saa 3 asubuhi, ilikuwa aibu sana.Mkuu hiyo inatokea sana huku Usukumani, unakuta Ng'wana Luhanya ameenda kuloga usiku kumbe jamaa limezindika ile nyumba, anajifalaguafalagua mpaka kunakucha yuko hapo hapo na masempele yake. Mpaka mwenye nyumba anaamka! Sasa hapo nikiamua kumfanyia mauaji?
Yanawahi ila HAYADUMU na YANACOST SANA MAISHA.Duuh..sijawahi kukanyaga huko hata siku moja..Mungu kweli anasaidia magumu mengi nimepitia lakini huko bado sijafika...ila kuna jambo moja la kuweka wazi mara nyingi mambo ya Mungu yanachelewa ila ya giza hua yanawahi sana ila kama vile Mungu anavyosema yeye hua hawahi wala hachelewi..
Shangaa na wewe mkuu...!
Kwa kutumia ndumba
Ilikuwaje ndugu tuelezee kiundani nini kilikuwa chanzo na lipi lilisababisha akakufanyia hivyo? Pia uliteseka kivipi.? Nataka tujifunze jambo.Nikiwahi kuendewa Kwa mganga na mtu aisee hii dunia ni nzuri niliteseka miaka miwili bila kujua ila nilikuja kupata ufumbuzi wa matatizo na uchawi niliofanyiwa Kwa siku moja tuu kweli Mungu yupo
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mganga anachukua pesa halali,wewe anakupa manyau nyau yakakutese[emoji848]
Sent from my iPhone using JamiiForums