Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Ila waganga bana wametusaidia sana sie wafanya biashala nakumbuka kuna kipindi biashala zilikuwa haziendi na kila ukiingiza hela unaona imepotea yani hujui hata hela inapopotelea unatoa hela sehemu unaingiza kwenye biashala zako ila ndio kwanza inakata mtaji basi ndio nikaenda sehemu kwaa mara ya kwanza nikaambiwa nikatafute nywele za kichaa nikaenda nikamchukua kichaa mmoja hivi nikampeleka saloon hapo nikapata nywele zake nikapeleka basi zile nywele zikachanganywa na madawa mengi nikapewa kichupa chenye maji yaliyochanganyika na nywele zile niweke kwenye biashala yule mganga aliniambia wakati kichaa akiwa anatembea na ndio biashala yako itakuwa inaenda na kweli bana nilipofika niliweka ile chupa sehemu inayotakiwa ndani ya siku kadhaa kuanzia siku ile nilipiga biashala we ogopa hujafungua biashala ila watu wanakungoja ww tu dah ndio mana mimi naedelea kuwaheshimu waganga na sio wachungaji wala masheh mana sina faida nao.Acha wanaosema sijui hawajawahi kwenda au kuwa waganga waongo waendelee tu ila mimi siachi madhari kila nalofanya linakwenda
 

Siri kubwa ya mafanikio hapa ulimwenguni ni ushirikina/ nguvu za giza , sema kikundi flan cha watu kinataka kiwapumbaze watu kwa kuwaaminisha kwenda kwa waganga ni dhambi au laana Sijui , wakati wenyewe ndo washirikina wakubwa, tena wengine uchawi wao wa kutisha, ila kwenye jamii wanaonekana wacha mungu , wanasaidia jamii ila ndani ni mbwa mwitu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu shida hutoi connection

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe pekee ndio umenivutia Sana Reply yako, Allah ndio kila kitu NDUGU. nimeipenda Sana Tena Sana natamani ata kulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe pekee ndio umenivutia Sana Reply yako, Allah ndio kila kitu NDUGU. nimeipenda Sana Tena Sana natamani ata kulia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Allah atustiri ndugu yangu, sisi ni viumbe dhaifu mnoo, tunamkosea kila uchwao, tujibidiishe kwake, tutende mema zaidi na zaidi! Allah atusamehe pale tunapokosea, atujaalie mwisho mwema mzee.
🤲🏾
 
Naona umeamua kujisifu kwa kumroga batuli. Yatakurudia tu wewe na mapacha wako [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent From Galaxy S9
 
Sasa unataka tuseme tumeenda kwa waganga wakati hatujawahi kwenda. Kwani nikidanganya nafaidika nini? Kwa hiyo stories za humu wewe huziamini au hii ya kwenda/kutokwenda kwa waganga ndio unaona ina walakini?

Jaribu kufikiria vinginevyo, sio kila mtu atafanya unachofanya wewe. Ukijua hilo hutakuja na conspiracy theories za namna hii.
 
Mkuu mm sipingi kuna ambao kweli hawajawahi kwenda kwa waganga kweli ila kuna ambao wanaongopa humu hasa hawa wafanyabiashara ndo sipendi kuwaamini ht kidogo..

Kinachonijeraga ni pale mtu anaposhahadia uongo ilhali ktk uhalisia ni mfuasi mzururi wa huo upande..

By the way sie tuliozaliwa bara wengine sometym huwa wanapelekwa na familia zaoyaani wazazi na ni tamaduni za kawaida hasa ktk matatizo ya kikawaida ila wakishakuja mjini utasikia wanavyoponda hizo imani zao..

Binafsi niliwahi kuvutiwa na dawa flani ya kinga ya mwili inaitwa Kinkuti kwa wale wa kanda ya magharibi wanaijua ila nilipofika kwa mtaalamu akaniambia ananichanja ktk maungio yote ya mwili wangu dah nilinyong'onyea na kuahirisha nikihofia kuonekana mwanga machale kila sehemu ila njilaumu sababu ss hv naona umri sio rafiki tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Boss watu tuna stress acha tutoe kwa namna yoyote itupendezayo🤣🤣🤣hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…