Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Uk
Kiukweli mie nilikuwa kati ya watu wazito kuamini hayo mambo!
Kuna kipindi nikawa desperate sanaMume wangu alikua na kesi imelala upande wake,

Basi shogaangu akaniitia babu mmoja, yule babu akasoma wee akachukua maji akayafanyia mambo yake, kisha akaondoka!
Ile kesi iliisha kipuuzi sana

Yule babu aliomba ela ya sigara nikampa 10,000 akarejesha 9,000

Ila mpaka leo sielewi kama ni uganga ama sheria ilimaliza ile kesi
Ukiona hivyo ujue huo ni uganga na huyo ni mganga wa kweli, maana unampa 10k na anachukua buku tu then anarudisha chenji inamaana hilo buku ni kiingilio cha madhabahu ya giza, kifupi umeshaingia mkataba na shetani
 
Uk
Ukiona hivyo ujue huo ni uganga na huyo ni mganga wa kweli, maana unampa 10k na anachukua buku tu then anarudisha chenji inamaana hilo buku ni kiingilio cha madhabahu ya giza, kifupi umeshaingia mkataba na shetani
Ni kweli kuwa dawa za kienyeji zisizo na masharti huwa s mbaya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uk
Ukiona hivyo ujue huo ni uganga na huyo ni mganga wa kweli, maana unampa 10k na anachukua buku tu then anarudisha chenji inamaana hilo buku ni kiingilio cha madhabahu ya giza, kifupi umeshaingia mkataba na shetani

Mie hayo madhabahu na shetani wala sivijui
 
Waganga wengi ni waongo balaa
Kuna dada mmoja tulikuwa tunajua anaumwa nini lakini tuliamua kwenda kwa mganga ili tumsikie anasema nini
Mganga akaanza kumwambia umetupiwa jini na mchepuko wa mmeo na ndio linalokutesa
Daah tulicheka balaa baada ya kusikia uwongo wa mganga

Sasa na nyie kwanini mliamua kumchoresha mwenzenu? kama mlijua anachoumwa si mngempeleka sehemu atakayopata tiba sahihi. au mliamua kumgeuza mwenzenu futuhi?
 
Hawa mafundi bwana wapo Mafundii kwelii na wengine wachumia tumboo,,,niliwahi kupata fundi mmoja wa kike yule anaweza hata kukuambia matendo yako yote ya wiki nzima,,,ikiwemo uliyofanya ukiwa peke yako...Huyu yeye hakutozii nakupa hudama unakwenda ukiona shida yako imekwisha utampelekea shukrani kulingana na ulivyowiwa ukichuna sijui itakuaje.. Ila ki ukweli alikua na karama ya aina yake.. ....... KAMA UMEISHI KIJIJINI HUKOSI KWENDA KWA FUNDI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi binafsi nimekulia kwenye familia ya dini. Na toka nipo mdogo , nilishawahi kukiri, hata itokee nini kwenye haya maisha, Siwezi kumuacha Bwana Yesu , Kwani yeye Ndio kila kitu kwangu , hakuna kinachomshinda.

Na siku zote nikiona mtu akizungumzia masuala ya kwenda kwa mganga Sijui nilikua namuonaje, yani nilikua nawaona waswahili, hawajenda shule na nilikua Naona wanapoteza muda kufanya huo upuuzi. Inshort nikikuona una mambo ya kishirikina nakutenga na kukukwepa kama ukoma.

Ila Maisha yana siri nzito sana, Na hapa duniani binadamu tumeumbiwa mitihani mizito sana, Mitihani ambayo unafikia hatua kabisa unakiri kwa nafsi yako Mungu hayupo, na kama yupo basi sio kwa ajili yako, Yupo kwa ajili ya watu wengine.

Nakumbuka nilipata changamoto za maisha, nilijitahidi kuomba na kufunga kutokana na dini yangu , kwa kweli nilisimama imara sana na Dini yangu , nilimwabudu Mungu katika roho na kweli. Kama nilivyosema, binadamu tumeumbiwa changamoto kubwa sana hapa duniani, kuna matatizo mengine yanakupelekea kufanya mambo ambayo toka uzaliwe hujawahi kufikiria kuwa utakuja kufanya. Nikatubu kwa Mungu na kuvunja laana zote za ukoo zinazonitesa, pia bado ikagonga mwamba .

Nilikata tamaa sana , niliomba na kulia kwa Mungu anisaidie lakini Mungu hakunisikia. Nikajiuliza Mungu kuna watu hawakujui wewe, hawana muda na nyumba za Ibada, na maisha yao wamejaa furaha tele, wanaishi maisha ya anasa, mambo yao yanawaendea vizuri, wanafanya uchafu wote hapa duniani, Mimi nimeamua kukukimbilia Wewe bado unaniaibisha, mpaka inafikia hatua watu wanakutukana Mungu wako yuko wapi ? unajifanya mlokole kila siku kanisani na mambo yako hayaeleweki.

Kwa kweli kama binadamu, ilifikia stage nikasema NIMECHOKA, Ndipo ikanibidi nitafute njia mbadala ya kuweza kutatua changamoto zangu Sugu iliyonisumbua kwa mda mrefu. Nakumbuka usiku nilioamua kuwa ngoja niende kwa mganga, nililia sana , Kwani nilikua sitaki kabisa kufanya hivyo, nililia kama mtoto mdogo. Ila nilivyomaliza kulia, uchungu wote ukaisha na sikujutia chochote kuhusu maisha yangu mapya niliyoamua kuyachagua.

Tofauti na watu wengine ambao huangaika huku na kule kutafuta waganga, Mimi naweza kusema nilipata bahati, Kwani nilipata rafiki ambayo alikua anafanya sana hayo mambo , so alikua anajua waganga wengi sana kuanzia kigoma, pemba, Mbeya , Tanga na sehem nyingine nyingi.

Sijui niseme ni shetani alikua ameniingia, wakati naenda kwa mganga kwa mara ya kwanza, moyo wangu ulijawa na furaha sana, na nilikua nimeshaamini kuwa ntaenda kufanikiwa Tatizo langu . Yani moyo ulikua mwepesi na kujisemea pengine huku Ndipo nilipotakiwa kwenda miaka yote hiyo, Sijui kwa nini nilikua napoteza mda kwenda kanisani.

Basi safari yangu ya kwenda kwa waganga ikaanzia hapo, na niseme tu , mambo yangu kweli yalibadilika, na kwenda kwa waganga ndo ikawa kama fashion kwangu. Na niweze kusema tu toka nimeanza kujihusisha na ushirikina ni miaka mitatu sasa , na hakuna hata siku ambayo nimewahi kujuta wala kutamani nilipotoka.

Je na wewe ilikuaje mara yako ya kwanza kwenda kwa waganga? Nini kilikusukuma?
IMG_2082.JPG
IMG_2083.JPG
IMG_2084.JPG





Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Duuh..sijawahi kukanyaga huko hata siku moja..Mungu kweli anasaidia magumu mengi nimepitia lakini huko bado sijafika...ila kuna jambo moja la kuweka wazi mara nyingi mambo ya Mungu yanachelewa ila ya giza hua yanawahi sana ila kama vile Mungu anavyosema yeye hua hawahi wala hachelewi..
 
Pole sana, changamoto katika maisha hazikwepeki hata kidogo, ilà jinsi ya kuzitatua, hapo ndio kazi inakuwa kubwa zaidi. Nikiri sijawahi kufikiria kwenda huko, naomba sana nisiende huko, japo wanasema mtu ukishajihusisha na ujasiriamali lazima kuna siku utatumbukia huko as kuna nyakati utapitia ugumu wa kazi nk.
 
Najiuliza tu, mganga anafannya watu wanafanikiwa sana, pesa, nyumba, magar ya kifahar, mali za kutosha...lkn nikimuangalia yeye na maisha yake najiuliza maswal bila majibu......Its all about Spiritual World, kwa Mungu kuna mafanikio ya kweli na wala hakuna kudaiana na kuwekeana mashart magumu, kwa mganga kuna mafanikio yenye mashart na mwisho wake huwa sio mzur na kukosa amani

Take care, jifunze hayo, lkn watotk wako wafunze waende upande wa Mungu wa kwel.....ila kuna siku saut ya Mungu wa kweli utaisikia...just wait.....
 
Back
Top Bottom