Jeshi la Marekani lina branch kuu sita, ya mwisho ilianzishwa kipindi cha Trump kama sikosei.
1. US Army
2. Marine Corps
3. Navy
4. Air Force
5. Coast Guard
6. Space Force
Kuna branches zinafanana kidogo mfano US Navy na US Coast Guard zinaelekeana ila hazifanyi kazi sawa. Ingawa ukiivamia Marekani zitashirikiana, ila mfano kupigana vita mbali sijui Yemen na Taiwan hutowaona Coast Guard. Na kwenye kupambana na narcos pwani zile sijui Miami hutowaona US Navy bali DCEA wataomba assist kwa Coast Guard. Hata silaha zao ni tofauti, Coast Guard wana meli zina rangi nyeupe na nyekundu, ni meli nyepesi.
Space Force ni ndogo sana. Hizo nne za mwanzo zina uwezo wa kujitegemea kivyake kwa kiasi fulani kwenye silaha, special forces na misheni.
US Army ina jeshi lake lenyewe la anga (USAAF) hivyo haihitaji kuwaita Airforce (USAF) kwenye mission yake.
Wakati huo jeshi la maji (US Navy) lina jeshi lake la anga (Naval Air Force) ambalo hili lina idadi kubwa ya ndege kuliko ndege zote za Urusi. Ndege kama F/A-18 Super Hornet ni fightet ila inatumiwa na Navy tu, Airforce haitumii. US Navy ina jeshi lake la ardhini, US Marine Corps
Marekani inaifanya Marine Corps ni branch ya jeshi iliyo independent (kati ya 6), ila iliyo tawi la branch nyingine (Navy). Na huwa wana silaha tofauti kama bunduki, armour na weapons systems. Mfano F-35 kuna A ya Airforce, B ya Marines na C ya Navy.
Marine Corps wanaendesha zile amphibious landing crafts na hovercrafts. **** Wana missions ngumu na ndio hufa sana vitani, alafu ndio wa kwanza kutangulia kufungua njia kwenye battlefield ya mbali. Na wana mafunzo makubwa zaidi na uzoefu mzuri. Na huwa wanachukuliwa kwingineko hawaanzii Marine Corps.
*** Ndio maana wanapewa kazi za haraka zenye ugumu. Wako easily deployable na hawatumii muda mrefu kufundishwa mazingira ya ugeni.
Mwanzoni nilisema kila branch kati ya zile nne inaweza jitegemea kiasi, sasa kila branch ina special force yake. Special forces wa Navy ni SEALs (hawa wanapiga popote), wa Marines wanaitwa Raiders (hawa sanasana wanapiga Pwani kwenye mwambao tu).
Hivyo badala watumie Raiders, wanatumia SEALs. Kwanini hawatumii soecial forces za Army kama Green Berets?
Sababu Green Berets wao huwa ni special force ya muda mrefu na malengo mengi. Ukisikia jeshi la Marekani limewafundisha XXX ujue waliofundisha ni Green Berets. SEALs ni kufanya kazi ya malengo ya muda mfupi kama kuua Osama bin Laden.
Kwenye vita Raiders watavia fukwe wafe sana wafungue beachheads, SEALs watafuata wafe kwa wingi muda mfupi wamsome adui waondoke, Green Berets waje baadae ila wakae muda mrefu wakipiga misheni ngumu za rasharasha. Troops wa kawaida wapigane kila siku wao wafe mamilioni.