Kwa wale vijana wa kiume, mnawezaje kusema sitakuja kuoa mwanamke aliyezaa?

Mm nilishasema mzalishe ndugu yangu alafu usimuoe. Lazima nikutoe kafara Freemason ili nitajirike. Wanaume eeeh NB single mother ili ufurahie ndoa yako hakikisha aliyekuzalisha awe kafa jamani hapo kwa mbali soko linaweza kuwepo.
 
Hapa duniani kuna wanaume wamezaliwa kuja kuficha maovu ya wanawake mara nyingi wanawake huwatumia kama ngao ya kuficha maovu yao pale jamii inapowashitumu na wakimaliza kipindi chao cha mpito huwavua kama kandambili za kuogea kwa vile ndala za kuogea unazitumia uwapo sehemu chafu na hatari kama chooni na mwisho huzitelekeza nje zikiwa na uchafu.bahati mbaya wanaume hawa ndio huona fahari kutumika kama hivyo na mwisho wa siku husikia wanawake wakisema we love bad boy with harsh attitude.kwa hiyo mtoa mada endelea kuficha upuuzi wao nadhani huwajui roho za wanawake japo angalia wao wanavyoishi na watoto wa kambo na jinsi wanavyo watreat nadhani kama utakuwa makini utapata mwanga kuhusu roho za wanawake ndio maana mama yake diamond japo alikuwa single mother lakini yeye ndio mwiba wa ndoa ya zari ambaye pia ni single mother hii yote ni kwa sababu wanajijua walivyo na tabia mbovu
 
Wewe "dogo" usione huku ni Fb kuna baba zako huku labda una andika for fun! soma ulicho andika na hasa sentesi yako ya mwisho.

Mkuu wangu, mimi sio dogo kiivyo na pia sio mkubwa kiivyo. Nimeweka hiyo hoja hapo Chini kuzihirisha kuwa single mother sio laana ni wanawake kama wanawake wengine. Unaweza kumuoa na ukafurahia maisha ya Ndoa kuliko hata yule ambaye ameoa binti amezaa. Yote hii nimeweka kuonyesha kuwa sio vibaya kuwa nao na pia wanazobaraka zao.
Ukisoma koment ya huyo jamaa kuanzia juu jamaa kaonyesha kana kwamba kuwa na single mother ni kama unachukua laana. Sio sahihi hata kidogo, na nimewahi kuwa kwenye mahusiona sijawahi kuonyeshwa dharau au upuuzi basi tu inatokea sema kipindi nikiwa nadate nao nilikuwa sijawa tayari kuwa na Mke. Muda ulivyofika sasa hivi huyu niliyenaye akanisumbua narudi kwa single mother. Nitampenda, nitamtunza na kumheshimu sana na naamini kuna mafanikio na Baraka tele kwa hawa SM. Kuna jamaa yangu ameoa single mother, wanaishi vizuri na wanafanya maendeleo tu vizuri tu bila hata shida.
 
Mm nilishasema mzalishe ndugu yangu alafu usimuoe. Lazima nikutoe kafara Freemason ili nitajirike. Wanaume eeeh NB single mother ili ufurahie ndoa yako hakikisha aliyekuzalisha awe kafa jamani hapo kwa mbali soko linaweza kuwepo.

We jamaa hufai [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
umesoma comment ukaielewa kweli?

Nimeielewa ndio maana nikajibu hivyo. Anaposema inadharirisha watu unadhani yuko sawa ? Watu wanazungumzia madhaifu ya single mother ambayo yanapelekea mtu akioa single mother anaonekana amekosea. Mbona tunaposema madhaifu akina Baba hatusemi mnafanya udharirishaji wa kijinsia. Hapa tupo kuwekana sana na sio vingine Mkuu. Hakuna anayedharirisha mtu na huyu mdada amezungumza bila kusoma Bandiko. Bandiko halizungumzii mwanamama aliyeachika kwenye ndoa kisa udharirishaji bali wale ambao wanapata ujauzito kabla ya ndoa zao. Nawewe nakuona unaunga tera…! Unganisha tu hamnaga shida, mods nao wana akili na wanaangalia comment mbovu wanaziondoa.
 

Mkuu inaokena una uwezo wa kuelewa mambo.! Hivi nikisema dada zangu je nimemanisha dada zangu wa kuzaliwa nao ?? Ninaposema dada zangu, namanisha wanawake waliowarika langu. Mimi namheshimu kila mwanamke, Kutumia neno dada zangu haijamanisha dada zangu kuzaliwa nao tumbo moja. Sasa unasema nifiche aibu sijui aibu gani labda. Nenda kajifunze tena lugha ya kiswahili. Kuna dada wa kuzaliwa tumbo moja na dada kwa sababu yeye ni msichana ndio maana ni nimetumia neno la DADA ZANGU. Period
 
Hahahaaa sikujua kama ungekuja na utetezi wa kitoto hivi, haya ngoja na mimi nijitetee kama wewe.

Niliposema dada zako sikumaanisha wa nyumbani kwenu na hakuna sehemu nimesema ni hao mliozaliwa nao tumbo moja
nimemaanisha wa mitaani mkuu wacha kujishtukia .
 
wanawake single mother wanajua maisha, acheni kuhangaika na viserengeti.
 
Suala lililopo ni kuwa awe amezalishwa na dume mwingine then mi nije kuoa, haitakaa itokee.Sasa nimzalishe mimi halafu nije kukataa kumuoa si inabidi nipelekwe Mirembe.

Kuhusu mtoto wangu siku aje kuzalishwa tena nje ya ndoa, mawasiliano naye kwa kheri. Ukilea sana ujinga wasichana wanazoea kila uchao utakuwa unaletewa watoto tu.
 
Usiingie kwenye mahusiano kwa sababu ya huruma ,na matatiZo hayarithishwi amka wewe


Yaaani unataka nimlelee mwanaume alie hai mtoto wake dah
 
Shida mtoto akija kumtaka baba yake...hapo itakuwaje!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…