Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari zenu wapendwa!!....... Kama mnavyoona tetesi zilivyonyingi kuhusu ajira za walimu mwaka huu,ni mwendo wa danadana tu na kupigwa karenda ila hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho,subira yavuta heri!! Ndo mambo ya serikali yetu hayo hatuna budi kuwa wavumilivu(esp for those who lost opportunities)anyway................. Lengo la uzi huu ni kupeana mauzoefu tu juu ya changamoto tutakazokumbana nazo huko vituoni hasa kwa siye fresh from schools siyo mbaya kama nyie walimu wazoefu mkatujuza ama kutuambia walau jinsi ya kujipanga na kukabiliana na changamoto hizo huku tukiendelea kusubiri badala ya kuilaumu serikali ama kulalamika humu hadi wengine kutukana mitusi loh! mana hapa nshatishwa miye ooh mshahara hadi miezi 6!! Sijui unaenda kukaa kwa mwenyekiti wa kijiji sijui mwalimu mkuu jamani!! Hakuna kuhama na blah blah kibao haki ya nani!!............... So ningependa tuambizane hapa which is which?.......Karibuuni saana walimu wenzangu(angalau tuliwazane kipindi hiki)(simu yangu haina paragraph mtanisamehe)
La msingi kama jamaa zako au wazazi wanajiweza ,wajiandae kukupa fedha kidogo ya kukusaport kabla ya mshahara, .....ishu ya mishahara inategemea na halmashauri uliyopo, wapo wakurugenzi wanaojali watawalipa kwa muda ht kabla hazina haijatoa salary..........ninavyojua fedha ya kujikimu inategemeana na eneo kama ni jiji, manispaa au halmashauri ya wilaya na sio kutokana na level of education........MUHIMU; mwl tunza tiketi zako kwa kuna hela ya mizigo mnatakiea kulipwa,............++++++++++++(asante kwa maelezo na ushauri wako mzuri tena hilo la tiket nilikuwa silijui loh ntaitunza!
Kwa cheti na diploma pesa ya kujikimu ni sh 30 elf kwa cku na shahada n shlng 45 elf,
nowdays naona dhana ya wito inaanza kufutika,anyway thenks 4 your comment!!
Amen!!!!!Ndugu zangu waalimu wenzangu. Japo neno moja niwaambie. Tumekuwa tukiogopa mazingira ya kufanyia kazi. Kwanini? Huwezi pelekwa sehemu ambayo haina watu. Je wanaishije licha ya kuwa huduma muhmu hawana. Je unataka raha asilimia mia? Haiwezekani. Wazungu wanasema FIFTY FIFTY. Jipange kupambana na magumu. Hata siku moja usipange kupata raha ugenini. Je ulipo unaraha? Gani wakati unalalamika? Tujipe moyo tuirudishe hadhi ya ualimu. Tukawafundishe watoto wa M ungu nao wakapate maisha maz uri. Wenzetu huku kenya wanasomea ualimu lakini ajira hawana. Tumshukuru Mungu huko nyumbani tunasomea na serikali inatupatia kazi. MUNGU NI MWEZA. Maandalizi ya roho na mwili ni muhmu sana wajamani. Nitawatakie subra njema.
mbona walimu tarajali mnatusumbua sana tuongelee maswala muhimu kama krasimu ya katiba kama umefaulu utaajiriwa tu, vipi vyuoni hamukupewa elimu ya ujasirimali, jishighulisheni tengenezeni crips za viazi, ndizi na kunde pitisheni kwenye super market, sipendi vijitabia vyenu
changamoto kubwa ni mazingira ya ufanyaji wa kazi unapelekwa kijiji ambacho huduma muhimu za kijamii haizpatikani kiurahisi sasa kwa sisi wanawake ndio tunapata shida sijui kama utaweza kupanda milima ndugu Munkari
Je utakao wakuta huko kijijini wanamiili ya shaba ambao unawasaidia kukabili changamoto hizo?..
....La msingi ni kukubali kwanzj kiakili na kimtazamo kuwa hapo ndo kazini kwako then set malengo kuwa baada ya muda flani natakiwa kutokuwepo hapa eg utaenda masomoni au kubadilisha kituo. Kifupi popote pale utakapo pangiwa ni vema ukaripoti na kufanya kazi huko.
You never know ufunguo wako wa mafanikio upo!