Kwa wale waliopunguzwa kazini (USAID na wengine)

Kwa wale waliopunguzwa kazini (USAID na wengine)

6m ni kubwa aisee, kama hakujipanga imekula. Kwa kiasi hiko kama ni muanja atakuwa hata na maduka makubwa mjini. Ni watu wachache sana waliobahatika kufikia 6m salary
Ukiwa na mshahara mkubwa na matumizi makubwa ,meneja wangu back 2023 alikuwa anakunja zaidi ya hiyo ,ilq ananipiga vizinga vya 30k ,alikopa laki 5 ya mshkaji hakurudisha mpaka ilikuwa kivumbi .

Mafanikio anayo kama nyumba na gari kali.
 
Mkuu nyingi hazirudi! Nimeangalia kwenye mojawapo ya TV US , Kulikuwa na mradi Tanzania, wanauliza hii pesa yote ya nini kwenye mradi huo! Jina la mradi (Support Gender Equality for Climate change in Tanzania ) Pesa ya mradi ni $ 14,000,000! Hii ni pesa kubwa mno! Ilikuja kwa nani, na inafanya nini!
Nahisi upigaji ulitawala
 
Mkuu, kwa mambo yanavyokwenda baada ya siku 90 kutakuwa na kitu kingine kabisa!Sio USAID Tuliokuwa tukiijua! Kutoka wafanyakazi 10,000 mpaka 300! Kanda ya Africa itakuwa na wafanyakazi 12, na Asia kama sikose 8! Maanake miradi mingi mno itaondolewa, hivyo wafanyakazi wengi kwenye miradi locally inayopokea pesa toka USAID hakuna kazi!
Trump/Elon Musk wanaiunganisha kama kitengo tu katika Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani, sio taasisi inayojitegemea!
Inauma sana 😢 roho inaniuma kama nilikuwa nimeajiriwa huko..aisee naona mfyekeo unavyopita..watu wanavyokuwa jobless ee Mungu awatie nguvu
 
Usimwonee mwenzako wivu. Leo kwangu kesho kwako. Haya ni ya dunia. Nasikia Trump anataaka kubadilisha mawazo yake na kuirudisha UASAID iendelee.
 
Hoja ya msingi sana , pale unapoweza bana matumizi jibane hasa, hii inatukumbusha waajiriwa wengi Anza kuwekeza kwenye kilimo,biashara, nyumb
 
Wekeza mapema ktk maeneo mengi maana hatujui siku wala saa mikataba ya kazi itaisha lini, vipo viwanda unapewa mikataba wa siku 30 kila mwezi mikataba mpya, bosi akiona biashara imeshuka hakupi mkatabq mpya !
 
Back
Top Bottom