Kwa wale waliopunguzwa kazini (USAID na wengine)

6m ni kubwa aisee, kama hakujipanga imekula. Kwa kiasi hiko kama ni muanja atakuwa hata na maduka makubwa mjini. Ni watu wachache sana waliobahatika kufikia 6m salary
Ukiwa na mshahara mkubwa na matumizi makubwa ,meneja wangu back 2023 alikuwa anakunja zaidi ya hiyo ,ilq ananipiga vizinga vya 30k ,alikopa laki 5 ya mshkaji hakurudisha mpaka ilikuwa kivumbi .

Mafanikio anayo kama nyumba na gari kali.
 
Nahisi upigaji ulitawala
 
Inauma sana 😢 roho inaniuma kama nilikuwa nimeajiriwa huko..aisee naona mfyekeo unavyopita..watu wanavyokuwa jobless ee Mungu awatie nguvu
 
Usimwonee mwenzako wivu. Leo kwangu kesho kwako. Haya ni ya dunia. Nasikia Trump anataaka kubadilisha mawazo yake na kuirudisha UASAID iendelee.
 
Hoja ya msingi sana , pale unapoweza bana matumizi jibane hasa, hii inatukumbusha waajiriwa wengi Anza kuwekeza kwenye kilimo,biashara, nyumb
 
Wekeza mapema ktk maeneo mengi maana hatujui siku wala saa mikataba ya kazi itaisha lini, vipo viwanda unapewa mikataba wa siku 30 kila mwezi mikataba mpya, bosi akiona biashara imeshuka hakupi mkatabq mpya !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…