Kwa wale waliosoma Seminari za Katoliki

NAAMINI

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
672
Reaction score
235
Tumsifu Yesu Kristu.

Jamani mpo na maisha yanaendaje? Hebu tukumbushane yale maisha wakati ule tupo kitaluni kule seminarini, mambo ya masifu ya asubuhi, misa takatifu, joint masses n.k. Hakika nimeyamisi sana yale maisha visiga seminary, St. Peter's Seminary, St. James Seminary, Uru Seminary, Maua Seminary, Likonde Seminary, Stella Matutina (Ligano), Kasita Seminary, Don Bosco Seminary, Bihawana Seminary, Lubya Seminary, Itaga Seminary n.k. Na enzi zetu nakumbuka tokeo la form four na form six yaani seminary zilikuwa ziking'aa. Nimekumbuka sana seminary.
 
daaah!Maisha fulani ya ajabu kwa sisi tuliosoma Rubya seminary

Waalimu sio professional yaani ni full mapriest wenye philosophy na Theology....classs full porojo na student based learning....yaani mwalimu ka hana uhakika fulani anasubiri mwanafunzi aliyepiga zake tuition aje kutufundisha....

Anywayz nilipenda life hilo maana nimeadapt kuishi hata environment iwe harsh kivipi

Adhabu za kutoa visiki yaani ni shida tupu
 
St Joseph or Kaengesa Seminary... dah enzi za Mzee Matipa na Sangu Mkubwa kama Rector... issue za kuchoma mahindi msituni... issue za kukata mkia form one... tarehe tisa mwezi wa tisa saa tisa usiku....
 
Binafsi ni tunda la St. James Seminary, Kilema Moshi. Najivunia kuwa nilipita pale na nikaenda Kibosho kwa philosophy. Baadaye nikaachana na hayo maisha na nimekuwa mwanaharakati.
 

Ndio maana ulifukuzwa! Hata hivyo Rubya ya enzi hizo za Fr. RWOMA, siyo ya wakati wako!
 
Dah pand fulan hivi za bihawana seminary nimemiss sana mvinyo coz kuna kiwanda cha kutengeza mvinyo na maisha mengne kwe ujumla St. Augustine Seminary, Father Mwaja, Father Ndaona, na Father Kilolelo oyeeee.
 
Asalam aleykum warmatulah wabarkatu.. ex-seminarians wa Consolata seminary ...umenikumbusha sana wakati wa kuwa sakastia na kuvizia "dompo" , kula mdudu , chai ya maziwa,na siku za sikukuu kupenda kushika cheteso wakati misa inaendelea....inshalah yalikuwa maisha ya kitambo fulani.
 
Nimekumbuka maisha ya Rubya Seminary tukiws na misemo ya silensium magnum; INCAUDA VENENUM; tridum sacrum; niliyafurahia sana. Pia namkumbuka kashera; kajoki; majaba; chaba; chako n.k

na hiyo jina yako mkuu...kweli ulipita rubya...hivi kwanini ulikimbia.
 
Kwa wale wa Lighano, bado namchukia sana Father Chilewa, ila Nchimbi (pope) alikuwa poa sana. Da! Ila sitakaa nisahau Father Deo Mapunda (RIP) alivyotuchimbisha miti wakati wa kutengeneza mashamba mampya. Ila tuliiba sana kuku na kuwachinja na kuwabanika usiku wa manane. Maisha ya seminari yalikuwa na raha na karaha nyingi sana. But thanks GOD ndio yamenifanya nijue maisha na kuwa na elimu isiyo na mgogoro
 
Wapi wale wa NAMUPA SEMINARY-Wazee wa NAKADI na LITENG'ENDE-anywayla msingi ni kwamba mbona miaka hii hizi shule hazifanyi vizuri y?
Nilikua pale, full machungwa, mapera, maembe chitumba. RIP Fr J Mlaponi (madale) and the Rector Fr Nnunduma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…