ahh ha ha ha hayo majina mnayotumia humu JF waseminari mnanifurahisha sanaaaaa yaniiiiiiii.......ebu tusaidiane waseminari wangapi wananyazifa za uongozi Tanzania...tukianzia uraisi,ubunge,uwaziri na sector za juu wizarani...tutaje na seminari walizotoka...kwa kuanzia Membe{waziri mambo ya nje...namupa na dungunyi seminary},mnyika{maua seminary},cyril chami{uru},dr.slaa{kule arusha nimesahau jina badaae Dungunyi.....mimi mwenyewe{st.james seminary
Oh! Wapi HANGA REMINARY Namkumbuka Sana Baba Rector Chrisostom,casmiry,mgaga Baba Wa Wadufi, Esperanso Na Mzee Wa Para Ansigari Kwa Mambo Mengi Waliyoyafanya.Pia Niwakumbushe Mambo Ya Kukatwa Mikia,kuogeshwa Maji 4m 1(nyoya) Wote Room 1, Kula Kwa Vijiko Hata Ugali,mambo Ya Chepo,mambo Ya Nyali,wadufi,kulima Bustani Chini Ya Usimamizi Wa Bwana Kazi Philipo Na Luciani.Na Mengine Mengi,nawapenda Sana Waseminari Ukimaliza We Nimwanaume Wa Shoka.Seminari Oyeeeee.
NAAMINI:
Waliosoma seminary kwa uzoefu mdogo nilionao ni watu fulani wenye mwelekeo chanya katika nyanja zote za maisha. Katika uongozi wapo sawa lakini pia katika mambo mengine ya ajira (ufanisi kazini), biashara, uanzishaji na uongozi wa makampuni binafsi.
Nimesoma seminari, ninawenzangu niliosoma nao seminari moja (walionitangulia, niliokuwa nao mwaka mmoja na hata niliowatangulia). Nipo jijini Dar es Salaam, nakutana nao baadhi tunawasiliana, tunafahamiana tunafanya nini katika swala zima la maisha....... ipo wazi wote tunaona kila mmoja yupo VIZURI pale alipo (ajira, uongozi biashara, familia, etc).
Kama binadamu hatuwezi kuwa sawa wote kwa kila kitu hilo lipo wazi. wapo baadhi ambao kwa bahati mbaya mambo hayakwenda vizuri kutokana na sababu tusizozifahamu... NI MAISHA.
Haimaanishi kuwa kusoma seminari ndio kufanikiwa maishani, HAPANA!!! unaweza soma popote au hata usisome ukafanikiwa. Ila kwa kiasi kikubwa SEMINARI zinamjenga kijana/mwanafunzi kujitambua na kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha. Maadili mema yafundishwayo huko ni msingi mkubwa wa matokeo katika maisha.
Natamani kuendelea ila kwa sasa muda......
Dah..!! Maisha ya seminary matamu sana st.pius x seminary au makoko seminary Musoma R.I.P fr.Fmakure
daaah!Maisha fulani ya kisenge kwa sisi tuliosoma kule BUKOBA rubya seminary
Waalimu sio professional yaani ni full mapriest wenye philosophy na Theology....classs full porojo na student based learning....yaani mwalimu ka hana uhakika fulani anasubiri mwanafunzi aliyepiga zake tuition aje kutufundisha....
Anywayz nilipenda life hilo maana nimeadapt kuishi hata envt iwe harsh kivipi
Ha ha ha nakumbuka mbali st Pius makoko seminary rector fumakule aka pumbu ..full sala masifu plus poor diet
duuuhh hadi ndullu...
seminary sio me naona walinihalibu tu, kufungiwa ndani sana, pale nilipokuwa kwenye makundi ya watu wengi walinitambua ni product ya seminary bila hata kuuliza.. Nakumbuka nilipokuwa form one vijana wa form four walitimuliwa wote bila hata huruma, basi mwaka huo hapakuwa na form four wahitimu.
Huyu c akaanzishe uzi wa waliosomea St. Kayumba au st. Mwajuma? Msuli niliopiga mtu akinikashifu this way ananikeraje mie...!ha ha ha jamani waseminari wenzangu ule msuli tuliokuwa tukipiga na kwa jinsi tulivokuwa tukimwomba Mungu atusaidie tufaulu leo hii huyu jamaa anasema tulikuwa tukiiba mitihani na hiyo haitoshi wengi wa waseminari walioenda shule za serikali kwa form 5 na 6 walikuwa wakitoka na matokeo mazuri mno je hao pia waliiba...usiongee usilolijua...na hii ni thread ya waliosoma seminari tu sasa ww na sekondari yako kaa kando..
Tumsifu Yesu Kristu........
Jamani mpo na maisha yanaendaje hebu tukumbushane yale maisha wakati ule tupo kitaluni kule seminarini, mambo ya masifu ya asubuhi, misa takatifu, joint masses n.k. Hakika nimeyamisi sana yale maisha visiga seminary, st.peters seminary, st.james sem, uru seminary, maua seminary, likonde sem, stella matutina(ligano), kasita sem, don bosco sem, bihawana sem, lubya sem, itaga sem...n.k...na enzi zetu nakumbuka tokeo la form four na form six yani seminary zilikuwa ziking'aa...nimekumbuka sana seminar´..