Kwa wale waliosoma Seminari za Katoliki

Kwa wale waliosoma Seminari za Katoliki

Sina hamu na maisha hayo,kwani yalijaa unafiki wa hali ya juu mpaka nikafukuzwa nikiwa form two sababu ya kusema ukweli
 
Bihawana seminari mbona siwaoni? Mnakumbuka mtama? Fr Mbando, Zephrine, Mwaja etc. Nilimpenda sana Fr Matonya r.i.p. Maisha ya seminari yalikuwa mazuri sana.
 
dah pand flan hv za bihawana seminary nmemiss sana mvinyo cz kuna kiwanda cha kutengeza mvinyo na maisha mengne kwe ujumla St.Augustine seminary,father mwaja,father ndaona na father kilolelo oyeeee

mkuu ilikuwa ukichaguliwa kwenda kufanyakazi kiwandani unafurah sana coz utaenda kunywa. Fr Ngunwa enzi hzo kabla fr Ndaona hajaja. Frt Fasili Sili Lubuva r.i.p alitupatia choya jamaa alilewa ikabidi tukamfiche karibu na mchangani kule pondini. Fr Mbando alikuwa bursal alitulisha dona kasoro pasaka na st Augustine's day tu ndo wali nyama.
 
Wakuu mimi sikubahatika kusoma Seminary ila nilitamani sana.....

Nawasoma hapa kwa jicho la 3D ...
 
Si kwamba tulikuwa watata bali tulikuwa tukifanya plan za uhakika bila kabla ya kufanya jambo... Always nilikuwa na Plan B na C...
Kuna siku tumetoroka wanne kwenda st. Magreth kuna jamaa wa darasa la mbele walinipatia hela kidogo kwa lengo la kuwafanyia mpango wa kwenda St.Magreth. Kidume nikaandaa mipango na baada ya muda wa masifu ya jioni tukaanza safari. (kipindi hicho simu zilikuwa adimu sana).
Kwenye plan ilikuwa imeshatumwa barua kwa wale viwavi watusubiri kwenye uzio wa shule yao...bila kujua kuwa wale viwavi wameshakamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi huku wakitusubiri.
Wanaume tukafika na kupenya kwenye tundu nililokuwa nikilitumia kuingia huko. Ile anamaliza wa mwisho tukasikia "chini ya ulinzi" ...kutahamaki pale pembeni kuna mlinzi na gobore lake.
Niliwaza kwa kasi kuwa pale ni kufukuzwa tu shule kwani Gombera alishasema nikamatwe red handed anihukumu. Pia nilijiona ninafukuzwa shule huku hakuna hata kiwavi niliyemfuata ila kwa kuwa tu master mind wa mkakati.
Nyumbani kuna gobore hivyo najua ili upige risasi unahitaji zaidi ya sekunde 5.Kwa wakati ule nilihitaji sekunde 2 tu kujinusuru. Mithili ya umeme nilichomoka kwa kasi na kuruka uzio ule wa wavu kabla ya mlinzi kujua cha kufanya.
Sikusimama popote nilikimbia kwa kasi niwezavyo (bahati njema nilikuwa mchezaji na kipindi cha likizo nilikuwa nikishiriki riadha mtaani)... Nilikatiza kule mtoni kama vile hakuna mabonde.
Kama nilivyosema simu zilikuwa adimu hivyo nilijua wazi kuwa mlinzi hakuwa na simu hivyo kutoa taarifa ni lazima awadhibiti mayeka wake kisha ndio apeleke taarifa kwa uongozi wa shule kisha nao watoe taarifa SAJASE. Nilikadiria watahitaji dakika 20 hivi na mimi sikuhitaji muda wote huo.
Nilifika shule nikaingilia upande wa uwanjani kwa juu. Nikakatiza uwanja wa basket kisha nikaingia majuu na kutulia huku ninacheki usalama halafu bila kupoteza muda nikaingia chumbani...(kile chumba pembeni ya ofisi ya nidhamu)....
Sikuweza hata kuvua viatu nikapanda kitandani navyo na kujifunika. Wakati huo transfoma ilikuwa imeungua na tulikuwa tumemaliza mitihani hivyo jenereta liliwashwa kwa muda tu kisha tukaenda kulala.
Huku nyuma wenzangu waliokamatwa walihojiwa na wakanitaja.( my rule no 1: die alone...hakuna kutajana) kisha simu ikapigwa SAJASE kisha nikaanza kutafutwa.... Kwa mawazo yao ni kuwa kwa muda ule nisingeweza kufika shuleni kwa vyovyote. Kunitafuta ilikuwa ni sehemu ya kujenga ushahidi kwamba sikuwepo shuleni. Mwisho walikuja chumbani kwetu na kuja hadi kitandani kwangu (enzi hizo majina na namba ya kitanda yanawekwa mlangoni). Hawakuamini macho yao waliponikuta nimelala na waliponiamsha nikaamka kwa hasira kwani walinimulika na tochi. Ilibidi wapige simu tena kuuliza jina kama wamekosea (wangenifunua wangegundua nimevaa viatu bado)....
Ilibidi waniacha hadi asubuhi wale wengine walipoletwa shule kisha wakanitaja....kumbuka wamevunja sheria ya mastermind hivyo ni kuwakana tu! Niliitwa kuhojiwa na yule mlinzi alipoletwa anitambue alishindwa kabisa...mie nikamwambia mwalimu wa nidhamu kuwa "wewe unajua uhasama unaokuwepo kati ya madarasa yetu...inawezekana vipi nikashirikiana nao? Hakika hawakuwa na mimi na ninyi walimu ni mashahidi mliniamsha jana usiku..."
Jumatatu inayofuata wale jamaa walifukuzwa shule ika kama kawaida Makusaro hakuacha kunipa onyo...." Isaac jiangali, jiangalie wakati mwingine nitakufukuza, nitakufukuza,,,nssssssh nssssh"
Ilikuwa mara yangu ya mwisho kutoroka usiku....

Dahh...Kama movie vile..
 
Wakuu mimi sikubahatika kusoma Seminary ila nilitamani sana.....

Nawasoma hapa kwa jicho la 3D ...

end doesnt justify the means....kwani ulikuwa na wito wa upadre mkuu na je hadi sasa unao
 
hivi ndiko MLIKOJIFUNZIA kuwapanga mabinti FOLENIiiiii? na kuwatumia B3 (beki tatu)?
 
Shule bora tanzania ni mzumbe,ilboru,taboraboys,kisimiri&kibaha wengine wababaishaji[/QUOT
aseee what is the scale?.
mi nilipangwa kisimiri 2008 bt selection ilkuja nikiwa nshamaliza wiki 3 Maua Seminary. In anycase nisingeenda as none in our family studied in govt schools.
 
umeona eeeh?mama katoke amenifanya kuwa nilivo.....long live kasemi
 
Hongereni waseminari wote,, japokua sikusoma huko lkn nashukuru kwa seminari kunitengenezea kaka bora ambae najivunia kuwa nae.
Najua utapita hapa my bro frm maua seminary,,
Nakupenda sana kaka angu ur the best thing I ever had in my life.
 
Hongereni waseminari wote,, japokua sikusoma huko lkn nashukuru kwa seminari kunitengenezea kaka bora ambae najivunia kuwa nae.
Najua utapita hapa my bro frm maua seminary,,
Nakupenda sana kaka angu ur the best thing I ever had in my life.

Aisee umesema kitu ambacho hata mimi naunga mkono.
Pia my bro amepita huko seminarini kwa miaka 6 MBULU -SANU SEMINARY, kweli naamini wanapikwa tayari kukabiliana na changamoto za duniani. He is doing good things to the society snd his family. He is a leader, entrepreneur, father, ... I believe is because of being in these schools.
He is from Karatu Not Karatu boy who is in here. I dont think he is a member here.
All in all, these people got a chance to study life Not only studies ....
I came to know more than 20 Ex-seminarians because of my bro.... they are all doing good things.
Big up seminarians.
 
Hahaa,mwenyewe hapa nacheka sana vitusu vya kwa mende,afu kulikuwa na mdada anawowo la maana alikuwa analeta pale nyuma ya mesi.
Nakumbuka sana yale maisha ila seminarini ni mahala ambapo mtu anajengeka kiukwel.

Vp kwenye mgomo wa kushinikiza kande badala ya ugali ulikukuta? Sitasahau tulipoenda kukaa uwanjani then Rector Fumakule aka Dudu alipoanza kuita majina mmoja mmoja then anakuuliza 'unakula au huli',,ilikua kvumbi kwa form 1 maana wote walijikuta wanasema 'nakulaaaa' alipofika kwa form 2 sasa,woooote wakajibu 'hatuliiiii' ilikua siku ya tata kweli maana 'mpugo' ulikua nje nje!
 
Ndio huyo mkuu fr. fabian nderumaki

Asante mkuu jamaa alikuwa mtu wa kubuni maendeleo na alisikitika pindi hicho alikuwa paroko msaidiz parokian kwangu form zililetwa sasa mm nikawa niko mbali na kijiji, kwahyo hyo nafasi akapewa mtu mwingine akafanye interview, narudi napata hizo habari roho iliniuma sana ila alinipa moyo na kuniambia kuwa yeye hakuanzia seminari ila alisoma shule za kawaida na alipofika form six ndio akaomba kujiunga na seminari,kwa kifupi jamaa anapenda maendeleo ya vijana,namkumbuka kwa mengi
 
Asante mkuu jamaa alikuwa mtu wa kubuni maendeleo na alisikitika pindi hicho alikuwa paroko msaidiz parokian kwangu form zililetwa sasa mm nikawa niko mbali na kijiji, kwahyo hyo nafasi akapewa mtu mwingine akafanye interview, narudi napata hizo habari roho iliniuma sana ila alinipa moyo na kuniambia kuwa yeye hakuanzia seminari ila alisoma shule za kawaida na alipofika form six ndio akaomba kujiunga na seminari,kwa kifupi jamaa anapenda maendeleo ya vijana,namkumbuka kwa mengi

daahh mwl. Wangu wa geografia....mara ya mwisho aliniita akaniambia "nimeweza soma tabia watu wote hapa seminarini lakini wewe peke yako nimeshindwa"...mwisho wa kunukuu
 
Vp kwenye mgomo wa kushinikiza kande badala ya ugali ulikukuta? Sitasahau tulipoenda kukaa uwanjani then Rector Fumakule aka Dudu alipoanza kuita majina mmoja mmoja then anakuuliza 'unakula au huli',,ilikua kvumbi kwa form 1 maana wote walijikuta wanasema 'nakulaaaa' alipofika kwa form 2 sasa,woooote wakajibu 'hatuliiiii' ilikua siku ya tata kweli maana 'mpugo' ulikua nje nje!
ha ha ha ha kumbe ili neno mpugo au kupugwa mlikuwa nalo hadi nyie kweli tamaduni zilikuwa moja
 
Back
Top Bottom