Si kwamba tulikuwa watata bali tulikuwa tukifanya plan za uhakika bila kabla ya kufanya jambo... Always nilikuwa na Plan B na C...
Kuna siku tumetoroka wanne kwenda st. Magreth kuna jamaa wa darasa la mbele walinipatia hela kidogo kwa lengo la kuwafanyia mpango wa kwenda St.Magreth. Kidume nikaandaa mipango na baada ya muda wa masifu ya jioni tukaanza safari. (kipindi hicho simu zilikuwa adimu sana).
Kwenye plan ilikuwa imeshatumwa barua kwa wale viwavi watusubiri kwenye uzio wa shule yao...bila kujua kuwa wale viwavi wameshakamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi huku wakitusubiri.
Wanaume tukafika na kupenya kwenye tundu nililokuwa nikilitumia kuingia huko. Ile anamaliza wa mwisho tukasikia "chini ya ulinzi" ...kutahamaki pale pembeni kuna mlinzi na gobore lake.
Niliwaza kwa kasi kuwa pale ni kufukuzwa tu shule kwani Gombera alishasema nikamatwe red handed anihukumu. Pia nilijiona ninafukuzwa shule huku hakuna hata kiwavi niliyemfuata ila kwa kuwa tu master mind wa mkakati.
Nyumbani kuna gobore hivyo najua ili upige risasi unahitaji zaidi ya sekunde 5.Kwa wakati ule nilihitaji sekunde 2 tu kujinusuru. Mithili ya umeme nilichomoka kwa kasi na kuruka uzio ule wa wavu kabla ya mlinzi kujua cha kufanya.
Sikusimama popote nilikimbia kwa kasi niwezavyo (bahati njema nilikuwa mchezaji na kipindi cha likizo nilikuwa nikishiriki riadha mtaani)... Nilikatiza kule mtoni kama vile hakuna mabonde.
Kama nilivyosema simu zilikuwa adimu hivyo nilijua wazi kuwa mlinzi hakuwa na simu hivyo kutoa taarifa ni lazima awadhibiti mayeka wake kisha ndio apeleke taarifa kwa uongozi wa shule kisha nao watoe taarifa SAJASE. Nilikadiria watahitaji dakika 20 hivi na mimi sikuhitaji muda wote huo.
Nilifika shule nikaingilia upande wa uwanjani kwa juu. Nikakatiza uwanja wa basket kisha nikaingia majuu na kutulia huku ninacheki usalama halafu bila kupoteza muda nikaingia chumbani...(kile chumba pembeni ya ofisi ya nidhamu)....
Sikuweza hata kuvua viatu nikapanda kitandani navyo na kujifunika. Wakati huo transfoma ilikuwa imeungua na tulikuwa tumemaliza mitihani hivyo jenereta liliwashwa kwa muda tu kisha tukaenda kulala.
Huku nyuma wenzangu waliokamatwa walihojiwa na wakanitaja.( my rule no 1: die alone...hakuna kutajana) kisha simu ikapigwa SAJASE kisha nikaanza kutafutwa.... Kwa mawazo yao ni kuwa kwa muda ule nisingeweza kufika shuleni kwa vyovyote. Kunitafuta ilikuwa ni sehemu ya kujenga ushahidi kwamba sikuwepo shuleni. Mwisho walikuja chumbani kwetu na kuja hadi kitandani kwangu (enzi hizo majina na namba ya kitanda yanawekwa mlangoni). Hawakuamini macho yao waliponikuta nimelala na waliponiamsha nikaamka kwa hasira kwani walinimulika na tochi. Ilibidi wapige simu tena kuuliza jina kama wamekosea (wangenifunua wangegundua nimevaa viatu bado)....
Ilibidi waniacha hadi asubuhi wale wengine walipoletwa shule kisha wakanitaja....kumbuka wamevunja sheria ya mastermind hivyo ni kuwakana tu! Niliitwa kuhojiwa na yule mlinzi alipoletwa anitambue alishindwa kabisa...mie nikamwambia mwalimu wa nidhamu kuwa "wewe unajua uhasama unaokuwepo kati ya madarasa yetu...inawezekana vipi nikashirikiana nao? Hakika hawakuwa na mimi na ninyi walimu ni mashahidi mliniamsha jana usiku..."
Jumatatu inayofuata wale jamaa walifukuzwa shule ika kama kawaida Makusaro hakuacha kunipa onyo...." Isaac jiangali, jiangalie wakati mwingine nitakufukuza, nitakufukuza,,,nssssssh nssssh"
Ilikuwa mara yangu ya mwisho kutoroka usiku....