Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Kwa wale waliozaliwa na waliowahi kuishi Tabora, tukumbushane vituko vya Mboka

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    564.9 KB · Views: 140
Ndugu zangu, nimekumbuka mambo mengi saana kupitia uzi huu. Hebu niulize kuna mtu anamkumbuka power chuma? Haaa haaaaa
 
Baadhi ya picha za majengo ya Mboka Manyema.
 

Attachments

  • 1913-building Tabora.jpg
    1913-building Tabora.jpg
    57 KB · Views: 103
  • cathedrale_tabora.jpg
    cathedrale_tabora.jpg
    39.6 KB · Views: 97
  • ijumaa-mosque.jpg
    ijumaa-mosque.jpg
    39.1 KB · Views: 110
Ndo

Huyohuyo, alikuwa anakaa along ile barabara inayotoka isevya kwenda stendi ya mabasi au sokoni, hivi inaitwaje ile barabara? nikumbusheni pliz, kwenye magorofa ya msajili wa majumba enzi hizo.
Unataka kusema Kazima road?
mpira wa soka ukikosekana nakumbuka tulikuwa tunatumia matonga.

Zero pub.....ukitoka hapo nawe ni Zero kabisa

Thanks mkuu
.
Niko njiani lkn nikitulia lzm nipakue kila kitu humo.

"Like" like"!
 
Enzi hizo hakunaga mboka bila Malingumu the late R.I.P, mboka kwa vichaa ilikuwa kama inaongoza sasa mzee Malingumu nadhani ndio alikuwa raisi wa machizi Tabora. Kiukweli japokuwa alikuwa mwehu lakini alikuwa na nguvu sana na kama network ilikuwa on na off.
 
Rafiki Yangu kahtaan bora tupige story tukumbushane mambo ya nyuma kuliko mijadala ya Imani kule!

Mwanangu umemtaja Yule Mwehu Teacher umenikumbusha mbali sn! Nakupa majina ya wehu wengine! Malingumu na mwingine Roshi, na Aziza Moka na Yule Muhindi Wa kwa Athumani Store na Amani Mwehu, Mwajuma Ringa?


Vp wawakumbuka wale Mbuzi waliokua wanajichunga wenyewe?

Wayakumbuka mabasi ya Mpalaye?

Mboka Manyema ni balaaaa Mkuu!
Umenikumbusha mbaali! Mimi ni mtu mzima sana ila Roshi mwehu namjua tangu miaka hiyo. Sijui jama yu hai.
 
Hiyo marahanyo nimecheka mpaka watu nilikaa nao wamenishangaa,waswezi noma aisee.watoto wa siku hizi wanakuwa kama watuwazima
Mimi bibi yangu alikuwa rafiki wa mtemi wa waswezi Marehemu binti Mpela wa ipuli. Tulikuwa tunasindikiza "WAFWEZI" ndio waswezi kweli lugha yao ni hiyo. Umenikumbusha mbali sana.
 
hahaha marahanyo, nilikuwa nawaogopa sana hawa waswez inilikuwa najua ni wachawi. kuna sehemu inaitwa kantaroli ukivuka reli ya kigoma kama unaelekea kiwanda cha maziwa unaikumbuka? nadhani walimaanisha control.
Umekumbusha kubadilishwa majina ya sehemu mfano chekeleni "check line", fotlaksi "four tracks" yote yanahusiana na reli ukivuja reli toka aidha Isevya au mjini utakutana na majina hayo.
 
wapiii ripota wetu wa RTD BENIIIIIIIIIIIII KIKOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!! kutoka tabora mimi n Beniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Kiko wa redio tanzania!!!huyu jamaa aliwahi ripoti kuhusu majambazi yaliyoteka basi la Anam kutoka Urambo kuja tbr ambako wasafiri waliamlishwa kupanda juu ya carrier ya bus then kulikuwa na askari 1 akaruka kutoka kwenye carrier ""mithili ya digidigi""(huyu n B kikooo)
Kweli huyu alikua ripota mahiri. But nadhani hatunae tena. Si uhakika mwenye taarifa atujuze.
 
*TABORA NA MADAKTARI.
Nikiwa Tabora katika miaka ya 1980s na 1990s nilifanikiwa kufahamu mengi kuhusu Madaktari wa binadamu na maishha yao, kwa kifupi nina wakumbuka hawa zaidi. Dr.Kisenge, Dr.Kobello, Dr.Mohamed.

Kwa mfano Dr.KISENGE
Alikuwa na zahanati yake katikati ya mji pembeni mwa jengo la kampuni ya sigara ikitazamana na Jengo la shirika la Bima(NIC) na benki ya zamani ya CRDB(Benki ya ushirika na maendeleo vijijini).
Alifariki 1994.
Watoto wake watatu wakaja kuwa madaktari Dar, Mmoja Dr.Sabuni(Ni daktari bingwa wa watoto pale Muhimbili), Dr.Peter Kisenge(Ni Daktari bingwa wa Moyo pale Muhimbili) na Dr.George(Ni daktari wa Mifugo, yuko Dar akifanya biashara ya vipuri vya Magari Kariakoo).

Yupo mtoto mwingine wa Dr.Kisenge anaitwa Endrew kwa sasa yupo Dar anakula bata tu, yeye ni kupiga hela na kuponda raha, enzi zile kila mrembo mkali aliyekuwa Uhazili jamaa alikuwa anamsaka kwa udi na uvumba, muda mwingi alikuwa akiendesha Kwa kasi Pikipiki Kubwa XL ya Ofisi(Zahanati), Gari ya Baba yake(Pigot 504) na baadaye alinunua Carina yake Nyekundu ili kusaka warembo, jambo la ajabu ni kuwa marafiki zake aliokuwa nao Tabora na baadhi ya warembo wengi wa Uhazili walikufa kitambo sana kwa Ukimwi lakini huyu jamaa inadaiwa mara zote alipopimwa alikuwa yuko Fit kabisa!!
Vp Dk Othman? Alikuwa daktari Kitete akaacha na kufungua clinic yake. Mkewe alikuwa mwalimu Tabira Girls nadhani.
 
Mboka ndio kwetu,
Uyui ndio wilaya,
Upuge ndio kijiji,
Mission ndio mtaa.
Japo pale town sikonge road na ipuli kwetu pia
 
Aisee, nawe ni wazamani kama mimi. Mwl Shigela ni mama yangu wa ubatizo, she is late lkn.

Nawakumbuka wengi, pamoja na mwl. Fundi.
Mihogo ya mzee Amir bwana ilikuwa something else na ile supu yake, hata waliosoma Iyui na Uhuru watakuwa wanaikumbuka sana. Kuna kipindi nilienda kuitafuta, nikakuta wanae ndio wanapika lkn haikuwa mizuri kama ile.

Unakumbuka poems za Chiboni? "Once l went to fairy land" na "water water, but no any drop to drink"

Wewe umesima UYUI, na mie: mihogo ya mzee Amir ilikuwa ni hatari[emoji106][emoji1]
 
Back
Top Bottom