Kwa wale wanaohitaji kuanza kilimo cha machungwa

Kwa wale wanaohitaji kuanza kilimo cha machungwa

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,047
Reaction score
1,832
Habari wakulima na wafugaji,

Kuna watu ambao wanataka kujiingiza kwenye kilimo cha michungwa muda ni huu wa kuandaa shamba,

1. Lima shamba
2. Ng'oa visiki
3. Fanya layout
4. Piga mashimo
5. Weka mbolea ya samadi
6. Subiri mvua hasa zile za masika

Mimi nipo Muheza Tanga na mkulima
mdogo wa machungwa. Mbegu zipo
nyingi ila zinazotumika kwa sasa ni
msasa na valencia. Tofauti yake ni
kwamba msasa unakomaa mapema
na unakulazimisha kuuza mapema.

Mbegu hii hulimwa na wakulima
wenye kipato cha chini ambao
hawawezi kuvumilia njaa. Bei yake
shambani huanzia Tsh 20 mpaka Tsh
50.

Valencia ndio mbegu
inayopendwa na wakulima wengi
kwani inaweza kukaa muda mrefu
shambani. Pia chungwa linaweza
kuuzwa mpaka Tsh 100 au zaidi ya
hapo.

UNAPATAJE FAIDA?
Ukiwa na shamba ekari moja inaweza
kuingia michungwa 80 ambao
utakapokomaa vizuri unaweza kuzaa
hata machungwa 1000.

Wekea umezaa machungwa 800
zidisha mara michumgwa 80 unapata
64000 zidisha mara 100 kama ni
valencia unapata Tsh 6400000/=

GHARAMA ZA KUHUDUMIA
Shamba la michungwa litahitaji
huduma za ukaribu katika miaka
mitatu ya mwanzo baada ya hapo
itakuwa ni kulimia tu na kufanya
usafi Mwingine kama prunning
ambazo hazifiki hata laki tano kwa
mwaka. Kumbuka hapo nimepiga
hesabu ya ekari moja tu.

CHANGAMOTO
Machungwa hasa valencia
uwezekano wa kushambuliwa na
magonjwa ni mdogo sana
changamoto kubwa ni wezi na
machungwa kuanguka kama utakuwa
unasubiri bei kubwa.

SOKO
Zamani soko la machungwa lilikuwa
ni changamoto kubwa kwani mikoa
iliyokuwa inapokea machungwa
ilikuwa ni Dar na Arusha tu ila kwa
sasa soko ni kubwa mpaka Nairobi
na Mombasa kwa mfano inafikia
kipindi ukiwa na machungwa
shambani wateja wanakusumbua
wewe.

UPATIKANAJI WA MASHAMBA
Mashamba yanapatikana ila kwa tabu
na bei yake iko juu kidogo.

KUHUSU WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wanapatikana pia
unaweza kujenga nyumba ya kawaida
shambani na Mtu akakaa huko huko
kwa Ulinzi.

Nafikiri nimekujibu japo kidogo.
Pia nimepiga hesabu ya ekari moja
na pia mchungwa unaweza kuzaa
mara mbili kwa mwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran sana kwa ushauri wako kaka
Habari wakulima na wafugaji,

Kuna watu ambao wanataka kujiingiza kwenye kilimo cha michungwa muda ni huu wa kuandaa shamba,

1.lima shamba
2.Ng'oa visiki
3.Fanya layout
4.piga mashimo
5.Weka mbolea ya samadi
6.Subiri mvua hasa zile za masika

Mimi nipo Muheza Tanga na mkulima
mdogo wa machungwa. Mbegu zipo
nyingi ila zinazotumika kwa sasa ni
msasa na valencia. Tofauti yake ni
kwamba msasa unakomaa mapema
na unakulazimisha kuuza mapema
mbegu hii hulimwa na wakulima
wenye kipato cha chini ambao
hawawezi kuvumilia njaa. Bei yake
shambani huanzia Tsh 20 mpaka Tsh
50. Valencia ndio mbegu
inayopendwa na wakulima wengi
kwani inaweza kukaa muda mrefu
shambani. Pia chungwa linaweza
kuuzwa mpaka Tsh 100 au zaidi ya
hapo.
UNAPATAJE FAIDA?
Ukiwa na shamba ekari moja inaweza
kuingia michungwa 80 ambao
utakapokomaa vizuri unaweza kuzaa
hata machungwa 1000.
Wekea umezaa machungwa 800
zidisha mara michumgwa 80 unapata
64000 zidisha mara 100 kama ni
valencia unapata Tsh 6400000/=
GARAMA ZA KUHUDUMIA
Shamba la michungwa litahitaji
huduma za ukaribu katika miaka
mitatu ya mwanzo baada ya hapo
itakuwa ni kulimia tu na kufanya
usafi Mwingine kama prunning
ambazo hazifiki hata laki tano kwa
mwaka. Kumbuka hapo nimepiga
hesabu ya ekari moja tu.
CHANGAMO
Machungwa hasa valencia
uwezekano wa kushambuliwa na
magonjwa ni mdogo sana
changamoto kubwa ni wezi na
machungwa kuanguka kama utakuwa
unasubiri bei kubwa.
SOKO
Zamani soko la machungwa lilikuwa
ni changamoto kubwa kwani mikoa
iliyokuwa inapokea machungwa
ilikuwa ni Dar na Arusha tu ila kwa
sasa soko ni kubwa mpaka Nairobi
na mombasa kwa mfano inafikia
kipindi ukiwa na machungwa
shambani wateja wanakusumbua
wewe.
UPATIKANAJI WA MASHAMBA
Mashamba yanapatikana ila kwa tabu
na bei yake iko juu kidogo.
KUHUSU WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wanapatikana pia
unaweza kujenga nyumba ya kawaida
shambani na Mtu akakaa huko huko
kwa Ulinzi.
Nafikiri nimekujibu japo kidogo.
Pia nimepiga hesabu ya ekari moja
na pia mchungwa unaweza kuzaa
mara mbili kwa mwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakulima na wafugaji,

Kuna watu ambao wanataka kujiingiza kwenye kilimo cha michungwa muda ni huu wa kuandaa shamba,

1.lima shamba
2.Ng'oa visiki
3.Fanya layout
4.piga mashimo
5.Weka mbolea ya samadi
6.Subiri mvua hasa zile za masika

Mimi nipo Muheza Tanga na mkulima
mdogo wa machungwa. Mbegu zipo
nyingi ila zinazotumika kwa sasa ni
msasa na valencia. Tofauti yake ni
kwamba msasa unakomaa mapema
na unakulazimisha kuuza mapema
mbegu hii hulimwa na wakulima
wenye kipato cha chini ambao
hawawezi kuvumilia njaa. Bei yake
shambani huanzia Tsh 20 mpaka Tsh
50. Valencia ndio mbegu
inayopendwa na wakulima wengi
kwani inaweza kukaa muda mrefu
shambani. Pia chungwa linaweza
kuuzwa mpaka Tsh 100 au zaidi ya
hapo.
UNAPATAJE FAIDA?
Ukiwa na shamba ekari moja inaweza
kuingia michungwa 80 ambao
utakapokomaa vizuri unaweza kuzaa
hata machungwa 1000.
Wekea umezaa machungwa 800
zidisha mara michumgwa 80 unapata
64000 zidisha mara 100 kama ni
valencia unapata Tsh 6400000/=
GARAMA ZA KUHUDUMIA
Shamba la michungwa litahitaji
huduma za ukaribu katika miaka
mitatu ya mwanzo baada ya hapo
itakuwa ni kulimia tu na kufanya
usafi Mwingine kama prunning
ambazo hazifiki hata laki tano kwa
mwaka. Kumbuka hapo nimepiga
hesabu ya ekari moja tu.
CHANGAMO
Machungwa hasa valencia
uwezekano wa kushambuliwa na
magonjwa ni mdogo sana
changamoto kubwa ni wezi na
machungwa kuanguka kama utakuwa
unasubiri bei kubwa.
SOKO
Zamani soko la machungwa lilikuwa
ni changamoto kubwa kwani mikoa
iliyokuwa inapokea machungwa
ilikuwa ni Dar na Arusha tu ila kwa
sasa soko ni kubwa mpaka Nairobi
na mombasa kwa mfano inafikia
kipindi ukiwa na machungwa
shambani wateja wanakusumbua
wewe.
UPATIKANAJI WA MASHAMBA
Mashamba yanapatikana ila kwa tabu
na bei yake iko juu kidogo.
KUHUSU WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wanapatikana pia
unaweza kujenga nyumba ya kawaida
shambani na Mtu akakaa huko huko
kwa Ulinzi.
Nafikiri nimekujibu japo kidogo.
Pia nimepiga hesabu ya ekari moja
na pia mchungwa unaweza kuzaa
mara mbili kwa mwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa uzi mzuri mkuu

Nina interest sana na hii biashara ya machungwa, kuna maswali kadhaa, naomba kuuliza kama hutojali

1. Hvi kwa mwaka machungwa unavuna mara ngapi?

2. NasIkia machungwa ukimwagilia unavuna mwaka mzima, je kuna ukweli?

3. Nikipanda mchungwa ni baada ya miaka mingapi naanza kuvuna?

4. Mti mmoja wa mchungwa unaweza vuna machungwa mangap?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzaaji wa machungwa ni Mara mbili kwa mwaka na huku hakuna kilimo cha kumwagilia

Mchungwa mmoja unaweza kuzaa mpaka machungwa 1500 inategemea na umri wake
Asante kwa uzi mzuri mkuu

Nina interest sana na hii biashara ya machungwa, kuna maswali kadhaa, naomba kuuliza kama hutojali

1. Hvi kwa mwaka machungwa unavuna mara ngapi?

2. Naskia machungwa ukimwagilia unavuna mwaka mzima, je kuna ukweli?

3. Nikipanda mchungwa ni baada ya miaka mingapi naanza kuvuna?

4. Mti mmoja wa mchungwa unaweza vuna machungwa mangap?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa uzi mzuri mkuu

Nina interest sana na hii biashara ya machungwa, kuna maswali kadhaa, naomba kuuliza kama hutojali

1. Hvi kwa mwaka machungwa unavuna mara ngapi?

2. Naskia machungwa ukimwagilia unavuna mwaka mzima, je kuna ukweli?

3. Nikipanda mchungwa ni baada ya miaka mingapi naanza kuvuna?

4. Mti mmoja wa mchungwa unaweza vuna machungwa mangap?

Sent using Jamii Forums mobile app
Unavuna mbili kwa mwaka ; mwezi wa pili na wa tisa.

Hakuna haja ya umwagiliaji. Bali upuliziaji wa dawa (mara moja moja)

Mchungwa huanza kutoa machungwa mwaka wake wa tatu lakini machungwa yanakua machache kutokana na umri. Mchungwa wenye miaka mitano na kuendelea hutoa machungwa zaidi ya 900-1500.

Bei ya mashamba ni kuanzia 150k-250k (pori). Shamba lenye michungwa ni kuanzia 8M per acre (subjected to changes depending on the financial condition of the farmer)

Nb; Nashauri muwekeze kwenye kilimo cha machungwa kwanini hakina complications nyingi. Unaweza usiende shambani mwezi mzima.

Usifocus kwenye outcome wakati wa kuanza. Focus kuwa na acres nyingi Za michungwa.

~Mbolea ya Shamba ni Miguu ya Mkulima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mku hongera sana.
Naweza kulima Mahindi au ni Machungwa yanayostawi huko
Asante
Habari wakulima na wafugaji,

Kuna watu ambao wanataka kujiingiza kwenye kilimo cha michungwa muda ni huu wa kuandaa shamba,

1.lima shamba
2.Ng'oa visiki
3.Fanya layout
4.piga mashimo
5.Weka mbolea ya samadi
6.Subiri mvua hasa zile za masika

Mimi nipo Muheza Tanga na mkulima
mdogo wa machungwa. Mbegu zipo
nyingi ila zinazotumika kwa sasa ni
msasa na valencia. Tofauti yake ni
kwamba msasa unakomaa mapema
na unakulazimisha kuuza mapema
mbegu hii hulimwa na wakulima
wenye kipato cha chini ambao
hawawezi kuvumilia njaa. Bei yake
shambani huanzia Tsh 20 mpaka Tsh
50. Valencia ndio mbegu
inayopendwa na wakulima wengi
kwani inaweza kukaa muda mrefu
shambani. Pia chungwa linaweza
kuuzwa mpaka Tsh 100 au zaidi ya
hapo.
UNAPATAJE FAIDA?
Ukiwa na shamba ekari moja inaweza
kuingia michungwa 80 ambao
utakapokomaa vizuri unaweza kuzaa
hata machungwa 1000.
Wekea umezaa machungwa 800
zidisha mara michumgwa 80 unapata
64000 zidisha mara 100 kama ni
valencia unapata Tsh 6400000/=
GARAMA ZA KUHUDUMIA
Shamba la michungwa litahitaji
huduma za ukaribu katika miaka
mitatu ya mwanzo baada ya hapo
itakuwa ni kulimia tu na kufanya
usafi Mwingine kama prunning
ambazo hazifiki hata laki tano kwa
mwaka. Kumbuka hapo nimepiga
hesabu ya ekari moja tu.
CHANGAMO
Machungwa hasa valencia
uwezekano wa kushambuliwa na
magonjwa ni mdogo sana
changamoto kubwa ni wezi na
machungwa kuanguka kama utakuwa
unasubiri bei kubwa.
SOKO
Zamani soko la machungwa lilikuwa
ni changamoto kubwa kwani mikoa
iliyokuwa inapokea machungwa
ilikuwa ni Dar na Arusha tu ila kwa
sasa soko ni kubwa mpaka Nairobi
na mombasa kwa mfano inafikia
kipindi ukiwa na machungwa
shambani wateja wanakusumbua
wewe.
UPATIKANAJI WA MASHAMBA
Mashamba yanapatikana ila kwa tabu
na bei yake iko juu kidogo.
KUHUSU WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wanapatikana pia
unaweza kujenga nyumba ya kawaida
shambani na Mtu akakaa huko huko
kwa Ulinzi.
Nafikiri nimekujibu japo kidogo.
Pia nimepiga hesabu ya ekari moja
na pia mchungwa unaweza kuzaa
mara mbili kwa mwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu shukran sana.

Je miche unaotesha mbegu kweye kiriba afu unapanda ama unahitaji grafting?
 
Habari wakulima na wafugaji,

Kuna watu ambao wanataka kujiingiza kwenye kilimo cha michungwa muda ni huu wa kuandaa shamba,

1.lima shamba
2.Ng'oa visiki
3.Fanya layout
4.piga mashimo
5.Weka mbolea ya samadi
6.Subiri mvua hasa zile za masika

Mimi nipo Muheza Tanga na mkulima
mdogo wa machungwa. Mbegu zipo
nyingi ila zinazotumika kwa sasa ni
msasa na valencia. Tofauti yake ni
kwamba msasa unakomaa mapema
na unakulazimisha kuuza mapema
mbegu hii hulimwa na wakulima
wenye kipato cha chini ambao
hawawezi kuvumilia njaa. Bei yake
shambani huanzia Tsh 20 mpaka Tsh
50. Valencia ndio mbegu
inayopendwa na wakulima wengi
kwani inaweza kukaa muda mrefu
shambani. Pia chungwa linaweza
kuuzwa mpaka Tsh 100 au zaidi ya
hapo.
UNAPATAJE FAIDA?
Ukiwa na shamba ekari moja inaweza
kuingia michungwa 80 ambao
utakapokomaa vizuri unaweza kuzaa
hata machungwa 1000.
Wekea umezaa machungwa 800
zidisha mara michumgwa 80 unapata
64000 zidisha mara 100 kama ni
valencia unapata Tsh 6400000/=
GARAMA ZA KUHUDUMIA
Shamba la michungwa litahitaji
huduma za ukaribu katika miaka
mitatu ya mwanzo baada ya hapo
itakuwa ni kulimia tu na kufanya
usafi Mwingine kama prunning
ambazo hazifiki hata laki tano kwa
mwaka. Kumbuka hapo nimepiga
hesabu ya ekari moja tu.
CHANGAMO
Machungwa hasa valencia
uwezekano wa kushambuliwa na
magonjwa ni mdogo sana
changamoto kubwa ni wezi na
machungwa kuanguka kama utakuwa
unasubiri bei kubwa.
SOKO
Zamani soko la machungwa lilikuwa
ni changamoto kubwa kwani mikoa
iliyokuwa inapokea machungwa
ilikuwa ni Dar na Arusha tu ila kwa
sasa soko ni kubwa mpaka Nairobi
na mombasa kwa mfano inafikia
kipindi ukiwa na machungwa
shambani wateja wanakusumbua
wewe.
UPATIKANAJI WA MASHAMBA
Mashamba yanapatikana ila kwa tabu
na bei yake iko juu kidogo.
KUHUSU WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wanapatikana pia
unaweza kujenga nyumba ya kawaida
shambani na Mtu akakaa huko huko
kwa Ulinzi.
Nafikiri nimekujibu japo kidogo.
Pia nimepiga hesabu ya ekari moja
na pia mchungwa unaweza kuzaa
mara mbili kwa mwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
HABARI,
"Mkulima na Mfugaji,
Asante na Hongera kwa taarifa nzuri ni kweli kwa Tanzania ilimo cha machungwa bado hakijawekewa mkazo inaitajika nguvu kubwa ya Serikali kuhamasisha kilimo hiki hasa wa kukaribisha makampunimakubwa kuja kununua kama inavyofanyika kwenye Korosho na Parachichi kwa sasa.Soko lake ni kubwa sana kwa Nchi za ulaya.Hiyo mbegu ya Valencia ni Nzuri sana inalimwa sana Africa ya Kusini na wanauza sana Ulaya na ni maarufu sana kwa kutengeneza Juice kutokana na ganda lake kuwa jembamba lina mbegu chache na mchuzi mwingi.
Aina za Machungwa ya kuuza nje yenye umaarufu yako mengi kama
  1. Mandarin
  2. Navel
  3. Blood
  4. Satsuma
  5. Seville
  6. Clementine
  7. Hamlin Pampja na hiyo Valencia ikiongoza.
Mkoa wa Tanga unaweza kunufaika sana na kuingia kwenye kilimo cha machungwa kama watu wake wakiwekeza sana huko,Na hivi sasa wakenya wengi wanakuja kununua machungwa Tanga na kuyapeleka Kenya wanayaandaa vizuri kwenye viwango na kuyasafirisha Nje hapo ni jukumu la watu wenye mitaji mikubwa hapa kwetu kutafuta masoko kwa msaada wa Serikali hayo yote yanawezekana.
Kwa mfano Nchi ya Misri inavuna zaidi ya Tani Metriki 3 kila mwaka na hasa wakilima Aina ya Valencia na Navel na soko lao kubwa ni Nchi zaChina, Russia, Saudi Arabia, Netherlands, China, UAE, Bangladesh, UK, Kuwait, Iraq na Ukraine huku wakipata zaidi ya dollar za marekani milioni 400 mwaka 2016 na ikipanda haraka kuwa kati ya nchi Tano bora za uzalishaji wa machungwa.Na ukiangalia kwa mwaka jana kwa taarifa za kimataifasoko la matunda duniani lilikuwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekani bilioni 5 kwa machungwa yaliyouzwa nje ya nchi huku umoja wa ulaya wakiuza asilimia 40 na africa asilimia 28 ya machungwa yote.Sasa ukiangali kwa hali ya hewa ya kwetu ni maeneo mengi kilimo cha mwachungwa kinafaa hapa ni uhamasishaji tu.Lakini pia nafikiri tumekuwa na wafanyabiashara wengi waliowekeza kwenye biashara za Aina moja sijui shida iko wapi kwani wengi wanasafiri nje ila hawaoni hiyo fulsa sekta ya kilimo inafulsa nying sana nje kuanzia mazao ya mboga,Maua,Matunda,Nyama na mengineyo.Kuna haja ya kizazi cha sasa kuamka.

HII NI ORODHA YA NCHI15 DUNIANI ZILIZOONGOZA KWENYE MAUZO YA MACHUNGWA NJE YA NCHI KWA MWAKA 2017
  1. Spain: US$1.3 billion (25.2% of exported oranges)
  2. South Africa: $752.5 million (14.9%)
  3. United States: $632.4 million (12.5%)
  4. Egypt: $547 million (10.8%)
  5. Netherlands: $299.9 million (5.9%)
  6. Australia: $228.1 million (4.5%)
  7. Hong Kong: $157.2 million (3.1%)
  8. Turkey: $157 million (3.1%)
  9. Greece: $126.9 million (2.5%)
  10. Italy: $108.3 million (2.1%)
  11. China: $106.1 million (2.1%)
  12. Portugal: $95.4 million (1.9%)
  13. Morocco: $84.3 million (1.7%)
  14. Chile: $63.9 million (1.3%)
  15. France: $43.6 million (0.9%)
LUMUMBA
 
Back
Top Bottom