Kwa wale wanaotaka kuikopesha serikali kwa hati fungani

Kwa wale wanaotaka kuikopesha serikali kwa hati fungani

Baada ya Bajeti ya serikali kupitishwa na kuanza kufanya kazi mwezi Julai, kuna fedha serikali itajipatia kwa njia ya mikopo. Kuna sehemu itakopa kutoka mashirika ya nje na nchi wahisani lakini kuna kiasi serikali itakopa.

Kukopa ndani ya nchi, ndiyo huwa Hati fungani/ Government bonds.

Tayari kupitia benki kuu serikali imetangaza tarehe ambazo itaanza kuchukua mikopo ya ndani.

Yaani wewe mwananchi, Kampuni na taasisi mnaweza kwenda kuikopesha serikali na kupata hati.

Ratiba ya hati fungani kwa mwaka wa fedha 2024/2025View attachment 3060519

Kumbuka:
Serikali ya Tanzania haijawahi shindwa lipa madeni yake.
Hati fungani ndiyo chanzo kikubwa cha faida za Mabenki kama CRDB na NMB
Wakandarasi wanaokimbizana na Serikali kufuatilia malipo ya kazi walizoifanyia unawaweka wapi?
 
Wakandarasi wanaokimbizana na Serikali kufuatilia malipo ya kazi walizoifanyia unawaweka wapi?
Hapo unaoongelea Serikali za mitaa.......
Serikali zote huwa hazichezi na financial markets,mana ndipo kwenye pumzi ya uchumi..
 
Punguza kujaza watu
Hizi ni biashara za wahindi na matajiri wakubwa.

We unapeleka mil 20 huku muhindi anapeleka Bil 2..!!!

Ngoja niendelee kutafuta utajiri kwenye biashara, nikipata Billions ndio nije huko kwenye money market.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Hii ndo point muhimu, uzi ufungwe hapa
 
1.Actually,,,,hatuongelei kama business,tunaongelea kama Investment....
2.Pia elewa kuwa siyo kila mtu ni mfanya biashara,wengine ni waajiliwa,hana huo mda wa kuhangaika na biashara,,,
3.Badala ya kuweka hela Bank na kukatwa,heri ikakae na kujizalisha.....
4.Mtu hana mda wa kujiumiza kichwa,kuwaza wateja na kuagiza mizigo na ishu za hasara kama ulivyo wewe.....
 
Badala ya kubaki na hiyo notion nenda uangalie soko lilivyo....
  • Nenda kaulize brokers
  • Angalia history ya ulipaji wa madeni
  • Angali list la Taasis zinazowekeza huko
  • And Tanzania haijawahi default on its loan obligations...
Kwa serekali hii Y samia unaweza tapeli wa pesa zako zote na Huna cha kufanya au unaweza kupelekea kesi za utakayishaji pesa ukapoteza fedha
 
Kwa serekali hii Y samia unaweza tapeli wa pesa zako zote na Huna cha kufanya au unaweza kupelekea kesi za utakayishaji pesa ukapoteza fedha
Weka instance moja tu,kuonesha kama kuna mtu au taasisi ishawahi kutapeliwa fedha katika soko la hati fungani....siyo Tanzania tu,hata kwa nchi za SADC.
 
Hii ndo point muhimu, uzi ufungwe hapa
wakati wewe hauna,,,,
Ila jua kuna watanzania weusi wenye hela na hawajui wapi pa kuziweka...
  • Kuna watu wanaishia kujenga frame tu hata katika maeneo ambayo hayana faida.....
  • Kuna watu wamenunua viwanja ambavyo hawajui hata watavifanyia nini....
 
Kwa mtu ambaye ana fedha nyingi, na
a) kazipata kwa namna ambayo haijirudii;
b)kwa sababu moja au nyingine hawezi au hataki kuzitumia kufanya biashara;
c) wafanyabiashara au watafutaji wanaohitaji kuweka surplus zao mahali salama;

Government bonds ni mahali sahihi sana kuweka pesa ili uzile polepole.

Mifano ya a) ni wapatao pensheni, bahati nasibu kubwa, urithi nk.

Kwa wadundulizaji wasioweza au kutaka kufanyia biashara pesa zao, UTT inafaa zaidi kwa vile kimfumo imerahisisha upokeaji wa viwango vidogo na uwekaji wa mara kwa mara, hata kila wiki mathalan.
 
Tatizo ya hizo hatifungani za serikali, na hasa za muda mrefu zenye riba za juu zaidi, ni ugumu wa kuzipata - kwa vile mara nyingi wanaozitaka ni wengi kuliko zinazotolewa.
 
Endeleeni kujifungia kwenye hizo comfort zones zenu za ""Biashara ngumu""
Braza hakuna kirahisi duniani, every thing come with sucrifice...!!!!

Hangaika, jifunze, tafuta taarifa.
Wao wanaweza wananini, na wewe ushindwe una nini??

Never back down mtoto wa kiume, TOKA KWENYE COMFORT ZONE.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Sasa hapo nani kakwambia ni rahisi....

sasa hata hao wahindi unao wasema wewe si wafanya biashara ama....?
 
Sasa hapo nani kakwambia ni rahisi....

sasa hata hao wahindi unao wasema wewe si wafanya biashara ama....?
Ifikie mahali tukubaliane maisha ni philosophy (nn unakiamini)

Hapa nimeona wanaoamini kwenye kuwekeza katika soko la pesa na wale wanaoamini kutoboa ni kuzungusha pesa mwenyew

Nadhani kila mmoja yuko sahihi kwa mtazamo na Imani yake
Mm binafsi naona wako sahihi wote kila mmoja atembee na mtazamo wake

Cha msingi ni kuelewa njia zote na kuamua kuchagua moja kati ya hizo.
 
Nikiwekeza milioni kwa mwezi nakunja kiasi gani kwa bond ya let say miaka 15?
Tuchukulie una Tsh 5,000,000 ambayo umeiwekea malengo ije kutumika kama ada ya shule ya wanao miaka 15 ijayo.
Ukaamua kuikopesha shillingi shillingi millioni 5 kwa mda wa miaka 15......Je,kwa mda wa mwaka mmoja utapata kiasi gani....?Na mpaka mkopo ufike ukomo utakuwa umezalisha kiasi gani....?

Taarifa muhimu
Hati fungani ya miaka 15 huwa na riba ya faida ya 13.5% kwa mwaka.
Ongezeko la riba kwenye Hatifungani za serikali huwa ni kwa siku

kanuni
Ongezeko la riba huwa ni la compound(Riba huzaa faida endelevu)
I=P(1+r/n)nt-p
ambapo
I = Faida utakayopata kwa mwaka
p = Fedha uliyowekeza , =5,000,000
r = Kiwango cha riba ,13.5% =0.135
n =idadi ya ongezeko la riba kwa mwaka ,=365 (Kila siku kuna ongezeko la faida kwenye riba ,ambapo kwa mwaka kuna siku 365)
t =mda =(Unataka kujua faida kwa mwaka mmoja)

kwahiyo
I= 5,000,000 (1+0.135/365)365X1-5,000,000
=5,000,000(1+0.000369863)365-5,000,000
=5,000,000(1.000369863)365-5,000,000
=5,000,000 X 1.1445082118-5,000,000
= 5,722,541-5,000,000
=722,541
Baada ya mda wa mwaka mmoja,itazalisha faida ya Tsh 722,541....

kwa,mda wa miaka 15,utakuwa umetengeneza
Jumla= 15x722,541 =10,838,115
Na 5,000,000 yako wata kurudishia,

kwenye kikokotoo chao serikali huongezea 0.03% kwenye riba,,faida yako yawa kubwa

Kikotoo cha benki kuu kuhusu Hati fungani....

mkuu greater than tunaomba utujibie hili swali kwa mchezo wa namba.
Tuchukulie unataka kuikopesha shillingi shillingi millioni 5 kwa mda wa miaka 15......Je,kwa mda wa mwaka mmoja utapata kiasi gani....?

Taarifa muhimu
Hati fungani ya miaka 15 huwa na riba ya faida ya 13.5% kwa mwaka.
Ongezeko la riba kwenye Hatifungani za serikali huwa ni kwa siku

kanuni
Ongezeko la riba huwa ni la compound(Riba huzaa faida endelevu)
I=P(1+r/n)nt-p
ambapo
I = Faida utakayopata kwa mwaka
p = Fedha uliyowekeza , =5,000,000
r = Kiwango cha riba ,13.5% =0.135
n =idadi ya ongezeko la riba kwa mwaka ,=365 (Kila siku kuna ongezeko la faida kwenye riba ,ambapo kwa mwaka kuna siku 365)
t =mda =(Unataka kujua faida kwa mwaka mmoja)

kwahiyo
I= 5,000,000 (1+0.135/365)365X1-5,000,000
=5,000,000(1+0.000369863)365-5,000,000
=5,000,000(1.000369863)365-5,000,000
=5,000,000 X 1.1445082118-5,000,000
= 5,722,541-5,000,000
=722,541
Baada ya mda wa mwaka mmoja,itazalisha faida ya Tsh 722,541....

kwa,mda wa miaka 15,utakuwa umetengeneza
Jumla= 15x722,541 =10,838,115
Na 5,000,000 yako wata kurudishia,

kwenye kikokotoo chao serikali huongezea 0.03% kwenye riba,,faida yako yawa kubwa

Kikotoo cha benki kuu kuhusu Hati fungani....

Hiyo hapo ni sehemu ya mfano...
 
Ifikie mahali tukubaliane maisha ni philosophy (nn unakiamini)

Hapa nimeona wanaoamini kwenye kuwekeza katika soko la pesa na wale wanaoamini kutoboa ni kuzungusha pesa mwenyew

Nadhani kila mmoja yuko sahihi kwa mtazamo na Imani yake
Mm binafsi naona wako sahihi wote kila mmoja atembee na mtazamo wake

Cha msingi ni kuelewa njia zote na kuamua kuchagua moja kati ya hizo.
Watu wanashindwa kutofautisha kati ya Uwekezaji wenye RIsk ndogo na ule wenye Risk kubwa....
  • wenye Risk ,hutumika kukutajirisha
  • wenye Risk ndogo hutumika kutunza thamani ya pesa yako
  • Lakini pia siyo hela yote huwa inakaa kwenye biashara,,,sehemu ya faida huwekwa pembeni ili ijizalishe huku ukiendelea na mambo yako mingine bila kuifkria...
 
Na ndicho nilichomaanisha
Na ndicho huyo braza alichomaanisha.

NASHUKURU TUMEELEWANA.

Yaani mimi saving yangu kwa mwezi ni 100k halafu unaniambia niikimbize kwenye money market kisa return ya 11% tena NOMINAL INTEREST.

Wakati huo inflation ni 4% hivyo REAL INTEREST ni 7%...!!!

Wakina Rostam huko wana bond za Bil 10, These are what we call INVESTORS.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
1. Lowest bond price ni 500,000
2.Return interest ya chini kabisa ni 9.8
3.With that interest, hela yako haiwi affected with inflation
4.Interest inakuwa compounded daily on first year...

Sasa nimefanikiwa kupata 1,000,000 na ninataka kuitunza kwa ajili mwanangu baada ya miaka kama 10,,,
Je ,niweke benki ambapo kuna makato au nikachukue hati fungani ya 15 years yenye kunipa 13.5% daily compounded interest....?
 
Tuchukulie una Tsh 5,000,000 ambayo umeiwekea malengo ije kutumika kama ada ya shule ya wanao miaka 15 ijayo.
Ukaamua kuikopesha shillingi shillingi millioni 5 kwa mda wa miaka 15......Je,kwa mda wa mwaka mmoja utapata kiasi gani....?Na mpaka mkopo ufike ukomo utakuwa umezalisha kiasi gani....?

Taarifa muhimu
Hati fungani ya miaka 15 huwa na riba ya faida ya 13.5% kwa mwaka.
Ongezeko la riba kwenye Hatifungani za serikali huwa ni kwa siku

kanuni
Ongezeko la riba huwa ni la compound(Riba huzaa faida endelevu)
I=P(1+r/n)nt-p
ambapo
I = Faida utakayopata kwa mwaka
p = Fedha uliyowekeza , =5,000,000
r = Kiwango cha riba ,13.5% =0.135
n =idadi ya ongezeko la riba kwa mwaka ,=365 (Kila siku kuna ongezeko la faida kwenye riba ,ambapo kwa mwaka kuna siku 365)
t =mda =(Unataka kujua faida kwa mwaka mmoja)

kwahiyo
I= 5,000,000 (1+0.135/365)365X1-5,000,000
=5,000,000(1+0.000369863)365-5,000,000
=5,000,000(1.000369863)365-5,000,000
=5,000,000 X 1.1445082118-5,000,000
= 5,722,541-5,000,000
=722,541
Baada ya mda wa mwaka mmoja,itazalisha faida ya Tsh 722,541....

kwa,mda wa miaka 15,utakuwa umetengeneza
Jumla= 15x722,541 =10,838,115
Na 5,000,000 yako wata kurudishia,

kwenye kikokotoo chao serikali huongezea 0.03% kwenye riba,,faida yako yawa kubwa

Kikotoo cha benki kuu kuhusu Hati fungani....

Duh,kwa hyo nikiwakopesha mil5 mwisho wa mwaka napata lak7 na ushee?
 
Back
Top Bottom