Tuchukulie una Tsh 5,000,000 ambayo umeiwekea malengo ije kutumika kama ada ya shule ya wanao miaka 15 ijayo.
Ukaamua kuikopesha shillingi shillingi millioni 5 kwa mda wa miaka 15......Je,kwa mda wa mwaka mmoja utapata kiasi gani....?Na mpaka mkopo ufike ukomo utakuwa umezalisha kiasi gani....?
Taarifa muhimu
Hati fungani ya miaka 15 huwa na riba ya faida ya 13.5% kwa mwaka.
Ongezeko la riba kwenye Hatifungani za serikali huwa ni kwa siku
kanuni
Ongezeko la riba huwa ni la compound(Riba huzaa faida endelevu)
I=P(1+r/n)nt-p
ambapo
I = Faida utakayopata kwa mwaka
p = Fedha uliyowekeza , =5,000,000
r = Kiwango cha riba ,13.5% =0.135
n =idadi ya ongezeko la riba kwa mwaka ,=365 (Kila siku kuna ongezeko la faida kwenye riba ,ambapo kwa mwaka kuna siku 365)
t =mda =(Unataka kujua faida kwa mwaka mmoja)
kwahiyo
I= 5,000,000 (1+0.135/365)365X1-5,000,000
=5,000,000(1+0.000369863)365-5,000,000
=5,000,000(1.000369863)365-5,000,000
=5,000,000 X 1.1445082118-5,000,000
= 5,722,541-5,000,000
=
722,541
Baada ya mda wa mwaka mmoja,itazalisha faida ya
Tsh 722,541....
kwa,mda wa miaka 15,utakuwa umetengeneza
Jumla= 15x722,541 =10,838,115
Na 5,000,000 yako wata kurudishia,
kwenye kikokotoo chao serikali huongezea 0.03% kwenye riba,,faida yako yawa kubwa
Kikotoo cha benki kuu kuhusu Hati fungani....