Kwa wale wapenzi wa matangazo ya TV na Radio, tangazo lipi unalipenda?

Ukiwa na mtoto mdogo mjanja mjanjaa anayependa kuigilizia unayapenda tu.
yaaah umegundua hilo kumbe mi mwanangu alikuwa analipenda lile la coca....utamsikia "hey cocacola?
..na kuna mda ukienda nae dukani akiziona coca anakuambia umnunulie anywe kama vile
 
Tangazo la chai jaba.
Chai nzuri yenye nguvu,chai bora chai jabaaa

Jambo kubwa,jambo katikati na jambo dogo

Sabuni ya mshindi
Mshindi ni sabuni mpya yenye nguvu,yenye kutakasa kuliko zote,mshindi ee mshindiiiii

Tangazo la bia ya safari
Safari ni safari iwe kwa mguu au kwa basi safari ni safari iwe mchana au usiku,kiangazi au masika safari ni safari.
 
Mtoto:Mama mi sitaki mi sitaki

Mama:hutaki nini wewe

Mtoto:sitaki kula mkate bila blueband
 
yaaah umegundua hilo kumbe mi mwanangu alikuwa analipenda lile la coca....utamsikia "hey cocacola?
..na kuna mda ukienda nae dukani akiziona coca anakuambia umnunulie anywe kama vile
Mimi kuna lile la kunyuoa la airtel sijui la kunyoa..

Sasa siku naingia saloon na dogo anaulizwa tukunyoeje anamwambia kinyozi ninyoe paap paap kama mshikaji fulani hivi. Alichekesha watu hatari
 
Tangazo la chai jaba.

Jambo kaubwa,jambo katikati na jambo dogo

Sabuni ya mshindi

Tangazo la bia ya safari
Safari ni safari iwe mchana au usiku,kiangazi au masika safari ni safari.
Na ww je? Mimi naitwa jambo katikatii
Ifanye ngozi yako kuwa laini na nyororo kwa kutumia jambo lotion, jambo lotion yako nunua sasa [emoji4][emoji4][emoji4]
 
Kuna hili.
Wamekata! Wamekata!
Eeh kweli wamekata.
heee wamekata?...wamekataje?[emoji23][emoji23]....wa mwisho analia...wamentumia ada ya shule...wamekataaaaaa[emoji23][emoji23]
 
heee wamekata?...wamekataje?[emoji23][emoji23]....wa mwisho analia...wamentumia ada ya shule...wamekataaaaaa[emoji23][emoji23]
Haha
Kuna lile la mountain dew.

Faru anatoka porini anakimbia kuja kwenye screen kama anatoka vilee kisha anasimama.

Mara kwanza kuna mtu aliliona akakimbia sebuleni anamwogopa faru. [emoji23] [emoji23]
 
Na ww je? Mimi naitwa jambo katikatii
Ifanye ngozi yako kuwa laini na nyororo kwa kutumia jambo lotion, jambo lotion yako nunua sasa [emoji4][emoji4][emoji4]
Haaha kuna ile ya joti ya tigo anapaulizia kwa mzee marurubadu...

Anakutana na mmasai anamuuliza rafiki kwa mzee mrarabadu anamwambia rafiki angalia usije ukanikanyagia mbusi yangu... linachekesha hatari.

Anakutana na joti mwenzake anamuuliza. Anamwambia kuuliza jero kuelekezwa buku.. anamwambia nakuja nakuja[emoji23] [emoji23]
 
Lingine joti yupo kanda ya ziwa anatangaza ile kila kona tumefika.

Yupo anaongea na simu sasa joti mwenzake wa kike yupo mgahawani anamchungulia joti anavyoongea kwenye simu joti akamkonyeza aseeh utacheka ufe.

Sema mengine hayasimuliki kwa maandishi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndorobo wewe iyo buku si bora ninunue gazeti nijipepee
Haha tangazo bora kabisa 2016.

Pangaboy sio..
Jamaa: anaulizia jumla shingapi muuzaji: anamwambiwa elfu 65 ...
Jamaa: eti mbona nyingi
Muuzaji: mbona unalilia kwani unashingapi wewe?
Jamaa: buku

Muuzaji: ndorobo wewe hiyo buku si bora ukanunue gazeti ujipepeee haha
 
Aibu yako hata wewe? Aibu yako hata wewe?
 
Kuna tangazo moja hivi la bia inatengenezwa kaskazini huwa naliskia clouds kwenye jahazi ni kama wimbo flani hivi wanaimba " kaaaaribu kaskazini......
Sema sijashika lyrics zake huwa nalielewa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…