Kwa wale wapenzi wa matangazo ya TV na Radio, tangazo lipi unalipenda?

Tangazo la Majuto anamletea mke wake nguo na viatu alafu mke anakataa na kuvitupa, anamtupia Majuto usoni... Majuto anainama kuziokota alafu akadondosha pipi ivory, eti mke akapagawa na pipi badala ya zawadi alizoletewa like seriously? Tangazo la kipuuzi kwakweli
 
Hehe zile zile ivory nazozijua? Sio bure, hizo pipi ni tamu kupindukia. Kuna matangazo mengine ambayo nia yazo haswa ni kuudhi mtazamaji, lengo lao, usije ukasahau kamwe kinachotangazwa. Kama wewe na pipi za Ivory, malengo yao yalitimia. Shida ni, waliyemtumia kufikisha ujumbe, Majuto. Pole sana. 😀😀😀
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] kwakweli linaniboa sana hili tangazo
 
Kuna tangazo linaboa sana la mzee anamkimbiza jamaa mmoja ampe sh 200 yake. Hivi kwa hali ya kawaida yule bwege alikuwa anakimbia nini alivoitwa? Na yule mzee anamkimbiza ili ampe 200 yake.
 
Kweli hapo ni ujinga mtupu, choo ni kibovu isitoshe kimeng'olewa, halafu unaambiwa usikitumie
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] kwakweli linaniboa sana hili tangazo
Mimi mwenyewe sijatizama tangazo lenyewe lakini ulivoeleza na navomjua majuto nikajua lazima majanga. Kuna moja ya huku Kenya ilikuwa kama slogan. Baada ya utoto mwingi usioeleweka wanamaliza na 'Usiseme maziwa sema Ng'ombe!' Wakati maziwa yenyewe wanayoyatangaza yanaitwa Tuzo Milk. Afu star ni Majuto wa Kenya, anaitwa Jalang'o. Acha tu yaani hata tv unatamani uizime milele. 🙂
 
Tatizo ni upeo... Wote unakuta wana upeo mdogo na kwa upeo wao wanaona ile ndo comedy. Kumbe anajidhalilisha na kudhalilisha wazee wenye umri kama wake wenye akil.inasikitisha sana

mi nashindwaga kuelewa sijui hakuna hata wazee wenzie wamshauri kwamba ana bugi sana kwa umri wake alafu kufanya ule ujinga
 
Haya matangazo ya kusafisha nyota, kurudisha nyota iliyo potea, mvuto wa biashara, mvuto wa wapenzi, kuongeza akili darasani na upupu unaofanana na huo kwangu mimi hio ni uzwazwa kiwango cha SGR.
Wapo na wale Manabii !
 
Wa Tanzania kila mtu ana dunia yake kichwani nwake shida inaanzia pale unapotaka dunia yako itawale wengine....
 

Kwa ulaya wanakuwa na makesi ya ajabu ajabu sana, ili kujihami wahusika ndio wanaweka hizo warning signs ambazo kwa huku tunaziona ni za ajabuajabu.
 
Mbona tangazo la tigo halipo kwenye list yako? Lile tangazo linatia kichefu chefu sana.
TCRA wamekaa kimya mpaka leo. Wash.nzy sana tigo.
Kwa huu ukimya tutarajie kupata nyimbo za ovyo zaidi ya wowoo

Lipoje hilo, na linahusu nini maana wengine TV hatuna asee [emoji16][emoji16]
 
Wahenga wenzangu mnamkumbuka dada mmoja enzi zile ITV ndio inaanza kulikuwa na Tangazo moja la sabuni ya Revola alikuwa mzuri sana na mwisho wa tangazo alikuwa anaachia bonge ya tabasamu mpaka mwili unasisimka. Sijui yuko wapi yule dada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…