TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 15,266
- 25,555
Unamsikia binti anasema
“Mimi siasa sio vitu vyangu”
Kikubwa nakula nashiba nalala naamka!
Au kijana wa maana kabisa anakwambia
“Mimi ishu za siasa sizimii kabisa zinanipotezea muda”
Kikubwa uhai tu!!.
Binti au kijana huyo huyo akienda
kupanda mwendokasi akakutana na zile mbilinge mbilinge anaanza lawama.
Akiambiwa nauli zimepanda anapagawa.
Akienda sokoni au golini kwa mangi kununua mahitaji akakuta sukari imepanda bei anaanza kubishana na kulalamika kwa mangi! 😁
Unamuonea tu mangi wa watu….mangi hawezi kuwa na majibu ya kukupa, majibu anayo mwanasiasa/kiongozi/serikali yako
Ambayo ulisema SIO VITU VYAKO😁
Haya nunua Big Jii katafune na chai, Kikubwa si utamu tu!!
Unakuta hapo ulipo umeshapoteza ndugu na marafiki wengi tu kwa ajali, wamekufia mikononi/usoni ukiwatazama, kisa tu wamekosa PF3 hawawezi kutibiwa!!
Hospital iko sinza, kituo cha polisi kiko kijitonyama, hadi uende kuifata hiyo PF3 urudi unakuta nduguyo tayari katema ndoano💔 Unaanza kulaumu wauguzi!
Ulisema siasa sio vitu vyako, hukujua kuwa hao wanasiasa ndio wanatunga hizi sheria?🤷🏿
Wangeweza kila hospital wakaweka dawati la polisi anayetoa PF3 kuzuia hayo!!
Au wakajenga hata kituo cha polisi kila hospital, hela zipo basi tu wanajali matumbo yao.
Siasa ndio maisha yako ya kila siku, kuanzia unaamka kunywa chai hadi usiku unakung’uta miguu kupanda bed kulala!
Siasa ndio inaamua mustakabali wa maisha yako!!
Mwanasiasa anaweza akaamua Dar wote mlalae saa moja jioni hamna cha kumfanya!!
Anaweza amua maduka yote kariakoo yafungwe jumamosi na ikawa hivyo!
Siasa ndio kila kitu Dada angu!
Usiseme siasa sio vitu vyako Kaka Yangu!
Labda useme hujui ni kwa namna gani maisha yako yana connect na siasa za nchi!!
Mifano ndio kama hiyo hapo Juu!
Badilika Sasa!!
#NRNE
CC @ Nipeni Maua Yangu.