Kwa wale wasiojua, Yesu atakuja hivi...

Kwa wale wasiojua, Yesu atakuja hivi...

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Watu wanaukubali usemi huu wa Waswahili kwamba: "Lisemwalo lipo, kama halipo linakuja" lakini ni wagumu kukubali kuwa Yesu atakuja.
"Ninyi nanyi vumilieni, tena simameni imara, kwa sababu kuja kwa Bwana Yesu kumekaribia."(Yakobo 5:8)

Kwa wale wasiojua, Yesu atakuja hivi:
  • Atakuja siku watu wasiyodhani — Mathayo 24:44
  • Atakuja ghafla kama mwivi ajavyo usiku — 1 Wathesalonike 5:2
  • Atakuja kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu. Nuhu aliwatahadharisha watu kwamba gharika itatokea wakampuuza. Ghafla, gharika ikaja, watu wakarambwa na maji — Mathayo 24:37
  • Akija, waliokufa katika Kristo(yaani waliookoka kabla ya kufa) watafufuliwa, kisha Yesu atawanyakua hao pamoja na watakatifu watakaokuwa hai duniani na kuwapeleka mbinguni — 1 Wathesalonike 4:16-17
  • Katika nchi ambazo itakuwa usiku - wawili watakuwa wamelala, mmoja(anayeamini) atanyakuliwa, mmoja(asiyeamini) ataachwa — Luka 17:34
  • Katika nchi ambazo itakuwa mchana - wawili watakuwa shambani, mmoja(anayeamini) atanyakuliwa, mmoja(asiyeamini) ataachwa — Mathayo 24:40
Kataa uongo wa Ibilisi eti hakuna kuokoka, eti Yesu haji. Tubu dhambi zako leo, kabla hujachelewa. Kumbuka pia, Yesu tu ndiye njia na kweli na uzima — Yohana 14:6

Kwa kuwa umesikia ujumbe huu hutakuwa na udhuru siku ya hukumu, Hutakuwa na nafasi ya kujitetea kwa nini ulikataa kuokoka — Mathayo 25: 41-46
 
Kwa kuwa umesikia ujumbe huu hutakuwa na udhuru siku ya hukumu, Hutakuwa na nafasi ya kujitetea kwa nini ulikataa kuokoka — Mathayo 25: 41-46
“Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.”
— Mathayo 25:41-46
 
Kristo alisharudi kutimiza (ufunuo 20:6)ila sivyo kama wengi walidhania na wachache waliojua ni yeye walimkataa kama ilivyokuwa kwa israel miaka 2000 iliyopita.

Hivi sasa ni majira ya Muumba mwenywe aliyemtuma Yesu(Yohana 17:3) kama alivyosema katika:-

Ufunuo 21:3
Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
 
Ukimsoma vema Setfree utadhani anataka kufungua JF Assemblies of God church
Hahaa, umenisoma vibaya, mkuu. Makanisa yaliyopo yanatosha. Nikifungua kanisa la Assemblies of God humu, nitawabatizaje watu kwa maji mengi?
Watu wenyewe humu wameficha IDs zao, huwezi kujua kama wako China au Azerbaijan 😀

Nasaidia kuifanya jamii iwe na maadili mazuri. Watu wengi wakiokoka, mambo maovu kama ubakaji, ufisadi, ujambazi, ushoga... yatapungua sana.
 
Full of conspiracy theories.
Your assertion is emblematic of a deeper crisis of discernment — a failure to distinguish eternal truth from modern cynicism. To reduce biblically grounded eschatology to 'conspiracy theories' is not merely a mischaracterization; it is a dismissal of divine revelation that has been meticulously preserved, faithfully proclaimed, and prophetically unfolding across generations. The truths I shared are not speculative constructs, but immutable declarations of Scripture. Their fulfillment does not hinge upon human belief, for what God has spoken shall, in its appointed time, be fulfilled — regardless of public opinion.
 
Kristo alisharudi kutimiza (ufunuo 20:6)ila sivyo kama wengi walidhania na wachache waliojua ni yeye walimkataa kama ilivyokuwa kwa israel miaka 2000 iliyopita.
Usipotoshe Maandiko. Ufunuo 20:6 inazungumzia ufufuo wa kwanza. Yesu atakapokuja waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Huo ndio ufufuo wa kwanza
Hivi sasa ni majira ya Muumba mwenywe aliyemtuma Yesu(Yohana 17:3) kama alivyosema katika:-

Ufunuo 21:3
Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Hilo bado halijatokea. Mstari wa 4 unasema: "mauti haitakuwepo tena." Sasa hivi watu bado wanakufa
 
Hahaa, umenisoma vibaya, mkuu. Makanisa yaliyopo yanatosha. Nikifungua kanisa la Assemblies of God humu, nitawabatizaje watu kwa maji mengi?
Watu wenyewe humu wameficha IDs zao, huwezi kujua kama wako China au Azerbaijan 😀

Nasaidia kuifanya jamii iwe na maadili mazuri. Watu wengi wakiokoka, mambo maovu kama ubakaji, ufisadi, ujambazi, ushoga... yatapungua sana.
Ushoga ni Nini
 
.
 

Attachments

  • images - 2025-03-15T220722.147.jpeg
    images - 2025-03-15T220722.147.jpeg
    39.8 KB · Views: 26
  • images - 2025-03-15T220952.307.jpeg
    images - 2025-03-15T220952.307.jpeg
    10.9 KB · Views: 24
  • images - 2025-03-15T215638.823.jpeg
    images - 2025-03-15T215638.823.jpeg
    21.4 KB · Views: 29
  • images - 2025-03-15T215904.856.jpeg
    images - 2025-03-15T215904.856.jpeg
    12.7 KB · Views: 28
  • images - 2025-03-15T215427.402.jpeg
    images - 2025-03-15T215427.402.jpeg
    35.2 KB · Views: 26
  • images - 2025-03-15T215338.447.jpeg
    images - 2025-03-15T215338.447.jpeg
    16 KB · Views: 31
Atakuja kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu. Nuhu aliwatahadharisha watu kwamba gharika itatokea wakampuuza. Ghafla, gharika ikaja, watu wakarambwa na maji — Mathayo 24:37
Sawa mtumishi, ila ni kwamba watumishi mnatupiga sana hebu fanyeni kampeini ya kuigeuza injili iwe huduma badala ya bidhaa
 
Unaweza ukakuta mimi ndio Yesu mpo tu kila siku tunapishana huku JF bila kujua nmesharudi
 
Your assertion is emblematic of a deeper crisis of discernment — a failure to distinguish eternal truth from modern cynicism. To reduce biblically grounded eschatology to 'conspiracy theories' is not merely a mischaracterization; it is a dismissal of divine revelation that has been meticulously preserved, faithfully proclaimed, and prophetically unfolding across generations. The truths I shared are not speculative constructs, but immutable declarations of Scripture. Their fulfillment does not hinge upon human belief, for what God has spoken shall, in its appointed time, be fulfilled — regardless of public opinion.
Religion is a fraud with a concept that only fills people with fear about the existence of fire. The Bible is just a book that people invented, just like the detailed scriptures of Eric Shigongo. Today, you are coming to deceive people when the holy scriptures have come with the concept of deceiving and fooling people.
 
Back
Top Bottom