Kwa wale wenye "MAJINI" vichwani au pembeni yao

Rakims

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2014
Posts
5,002
Reaction score
4,571
Majini ni viumbe ambao wameumbwa kwa Moto na walikuwa wakiishi duniani kabla ya binadamu miaka Milioni nyingi iliyopita.

Viumbe hawa wana tabia kuu mbili;

Yaani ya kibinadamu kwa maana wanakuwa wanafanya mapenzi, wanazaa na wanakufa.
Tabia nyingine ni ya Kimalaika ambayo ni kwamba wana uwezo wa kujigeuza katika umbo lolote wanalotaka na vile vile wanaruka na kwenda wanakotaka au kupita wanakotaka bila kutumia chombo chochote.
Taifa la Majini limegawanyika katika makabila zaidi ya Milioni Sabini na na sehemu na wana uwezo wa kujifunza lugha yeyote wanaoitaka. na umbile lolote wanalolipenda au la kukupumbazia.


Idadi ya Majini ni kila Binadamu mmoja kuna Majini 360 na zaidi kwa copy yake moja wanaishi katika Majumba yetu, kwenye Miti, Majangwani, Kwenye Mapango na Sehemu zenye Misitu Mikubwa.

Majini wako katika aina Mbili (2);
Maruhani na Mashetani:
Hizi aina mbili hazina tofauti sana na aina mbili za binadamu yaani wema au wabaya.


Majini aina ya kwanza:
Tunaweza kuwaweka katika kundi la maruhani kwa kuwa hawa ni Majini wema ambao wanamtii Mwenyezi Mungu na wanawasaidia Binadamu katika mambo mengi na wengine humtii mwenyezi mungu na kuishi kivyao mbali bila kuingiliana na wanadamu.


Aina ya pili ya majini:
Hawa tunaweza kuwaita mashetani kulingana na sifa yao ya kuhakikisha maovu yanaendelea na kuzidi duniani na kuendelea kuwatesa wanadamu kwa kujifurahisha au kwa kumtumikia Ibilis,
Mashetani ni Majini Waovu ambao ni wakorofi na wanawaletea Watu madhara na Matatizo mara kwa mara.




Majini Ni Viumbe Ambao WAPO Kama WANAADAMU Kwa kuwa na free wills yani maamuzi ya uhuru kwamba naamini au siamini iwe katika mungu au shetani.. sita waelezea sana kwa maana wameshaelezewa sana ila mimi napiga mng'arisho au msasa ili ufahamu wa watu uzidi kuongezeka..

VIUMBE Hawa wamegawanyika makundi mawili wapo waliomuamini mungu mmoja hawa huitwa marohani na wapo ambao hawajaamini wanamfuata shetani pia wao wanaitwa mapepo wachafu au majini wabaya mradi tu wawekwe kwenye ubaya ubaya..

ila wao kwa jina la kundi tunaweza kuwaita walioasi au waislamu huwaita makafiri wa kijini na wakristo huwaita mapepo wachafu.

Pepo wachafu au makafir wa kijini kwa ujumla majini waliumbwa kabla ya wanaadamu na walipewa machaguo ya uhuru wengi wao wakamuasi mwenyezi mungu ndio amri ikashuka kwamba waangamizwe wote na malaika viumbe watiifu wakashuka na kuja kuangamizi majini wengi..

Lakini hawakuangamizwa wote kwa maana wengine walipewa uwezo na mwenyezi mungu kuingia popote vyovyote hivyo waliingia majabarini chini ya mabahari na wengine waliingia katika matumbo ya wanyama..
.
vile malaika hawakupewa uwezo huo wakarudi na kumtaarifu mwenyezi hali halisi ndipo wakaruhusiwa kuwaacha wale waliokimbia....


Baadhi waliogopa sana kwa kuona mwenyezi mungu ni mkali wa kuadhibu wakaanza kutubu ndio hawa huitwa leo Majini wema Au Maruhani..


Waliobaki wengine walijiona wenye nguvu na waliweza kujihisi wamemkimbia mwenyezi na Wakaendelea Kufanya Maasi Yao...

kitu kingine watakiwa kujua majini wapo mara 300 yako wewe yani kila binaadamu wapo mara idadi hiyo yake Viumbe Hawa huishi miaka mingi wengine hufika hadi miaka 1000/-

majini wema hawamkalii mtu kwa ubaya humpenda na kutamani kumsaidia.. hawampotoshi imani yake alionayo humuangalia tu nakumsaidia mambo mengi tu bila kujijua kama mtu kufaulu vema bila kujijua wala kusoma sana, kupendwa pendwa na watu, kupenda mambo ya kiroho zaidi kuliko ya kimwili, humfanya mtu awe na huruma.

Kumletea ndoto njema akilala na humpunguzia maumivu ya mwili bila kujijua.. kumfanya afikirie jambo jema mtu hadi alifanye.. hawana roho mbaya hulia pale unapofanyiwa ubaya wengine hupanda kichwani na kulia sana pale unapouziwa wengine hukupitishia kitu kama hope rohoni au barafu unajiskia umekaa sawa na kusema one day yessss! huomba pamoja na wewe pale unapotupa malalamiko yako kwa mwenyezi mungu kwa imani yako....

majini wabaya au pepo wachafu humfunga mtu riziki zake na humrudisha nyuna mtu mambo yake na kumbaka kumfedhehesha mpaka akaanza kumkufuru mola wake, na kuanza kujihusisha na ushirikina ndio anaona anafanikiwa humnyanyasa ndotoni kwa kuota anakimbizwa anapigana anatukanwa.. anadhalilishwa anaumwa anateswa na akiamka anakuwa hana raha... humjaza mtu ujasiri anapotaka kufanya tukio chafu....


jinsi ya kujijua kama una jinni:

MSAFI/MCHAFU AU Huna tu

kwa kuwa hawa ni viumbe tuwafananishe na bacteria wanapokuingia huwaoni lakini madhara mwili unapata...

ZIFUATAZO NI DALILI ZA KUJUA KAMA UNA JINI MSAFI AU MCHAFU KIIMANI
..


1: Kuumwa kichwa kisichojulikana mwanzo wala mwisho mradi tu kinauma kila siku muda wowote

2. Uzito ktk Mabega au hata kichwani kwenyewe.


3. Kuota vitu vya kutisha usingizini

4. Kuchukia kuona au kuolewa km bado hujaoa au kuolewa.

5. Kwa alie Oa au kuolewa huchukia Tendo la ndoa

6. Kupatwa na maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au baada

7. Baadhi ya wanawake hukosa Maji maji katika UKE wakati wa kufanya tendo la ndoa na hivyo wakati mwingine hupatwa na michubuko endapo lita lazimishwa tendo hilo

8. Baadhi ya wanaume hushindwa kumalizia vizuri tendo la ndoa au kumaliza haraka zaidi na kisha kupatwa na usingizi Mzito Mara tu baada ya kumaliza Tendo la ndoa.

9 Km una mke au Mme hutaki kufanya nae tendo la ndoa na usiku huo ulio kataa unaota unafanya na mtu mwingine.

10.Kuwa na hasira za ajabu wakati wa kuamka asubuhi.

11.Wakati mwingine huona km kuna mtu kakuinamia wakati ukiwa umelala taa imezima(kiza)

12.Wakati mwingine huhisi km kuna mtu anatembea ndani ya chumba ulicho lala. Ukijaribu kuwa makini kumsikiliza au kuwasha taa humuoni mtu yeyote.

13: kujilaumu hadi kuhisi kulengwa na machozi kwa kosa dogo tu

14: kuchukia kutumwa na hupenda kujiajiri

15: kuchukia sana dhambi

16: ukikaa sehemu ya kimya sana unasikia watu wanaongea kichwani

17: kuota unasali kila mara hali ya kuwa kama unajilazimisha kusali ikiwa imekupita hata sala moja

18: kustuka saa nane usiku baada ya kuota umeamshwa kusali au adhana ya kwanza kwa mwislamu

19: kuota unamuombea mtu na mwili wako kujaa nguvu kwa mkiristo

20: kuota unaongea na kiumbe asiekuwa binaadamu either mnyama au ndege..

zipo hizo ni baadhi tu.. hii ni fursa kwako wewe mwenye majini kujitambua je ulionayo ni mema au mabaya? na unayatumia au yanakaa tu? unayatoa au unabaki nayo unaongeza elimu ili usimkufuru mwenyezi kwa kuwa na majini....

karibuni
P.M Namba Yako Tutengeneze group ya WHATSAPP Ya watu wenye maruhani tufundishane namna ya kuwatumia vema ili wasitupotoshe ikiwa unao na unajificha basi kumbuka huwezi kukimbia kivuli chako..


Walikupeleka wapi walikufundisha nini? yapi ya ajabu uliyaona? yapi yalikufanya ukainua mikono juu ukasema kweli mwenyezi umeumba hawa viumbe? haya na mengine mengi tutayaangalia humo kwenye group.

kuna watu hawana na wanawish wawajue na wawe nao nafasi zipo 15 tu na kuingia kwenye group jini wachafu hatuta fundisha...
. 30 wale wenye marohani wasiojuwa jinsi ya kuwaongoza na kuwatumia...


Kwa haya na mengineyo:
Tembelea:

Rakims
 
Kwa nini usiseme kuwa kuumwa kichwa au kukosa maji maji kwenye uke kunaweza kuwa kumesababishwa na sababu za kibiolojia? Kwa maelezo yako hapo 90% ya matatizo kwenye mwili ya binadamu yanaweza kuwa yamesababishwa na viumbe unao waita majini!

Pengine haya majini ndio wale wakiroho uya hita mapepo? Maana hata wao muda mwingine uzikataa sababu za kisayansi na kusema ni mapepo!

Kuna watu wakiuma kichwa au kuumwa kwa kipindi kirefu watu wao wa kiroho huwambia wana Mapepo!

Haya mambo yana kwenda na imani tuu!

Duuu ina maana wakina Gwajima nao wana Majini 300? Noma sana!
 
Pgakwa huyu jamaananamajini mengi anata kakugaia wenzake 0656 438 488

Majininyake mazito anajiita sheikh khalifa

Ila nambazake reg kwa Alphonsina mtei

Alikuwa mkristu kahamia uislamu mrudishe ukristoni aachane nanmajini

Yesu amwokoe
 

Only in Tanzania, majini wanashauri watu...
 
Hiyo kuumwa kichwa mhh inanitokea hata nipimeje na namba kumi na tisa na ji feel ni malaika
 
Hapana dawa yao Mbuzi katoliki na ukiona watu wanachukia sana huyu mnyama ujue tayari majini yameshakuingia.majini yote hayapendi kukaa karibu na Mbuzi katoliki.

dawa yao kitimoto
 
Majini wazuri?! Hamna jini mzuri katika ukristo labda uislamu, katika ukristo, mungu kaumba malaika, hao majini walihasi

Acha kuleta udini basi.
mara nyingi ukimkuta mtu analeta za udini udini anakuwa hana kitu kichwani na hufuata tu mkumbo kwa vile kazaliwa kwenye dini hiyo.

poor you.

na kama unahoja weka niione.
 
Mkuu Rakims nna maswali mengi ya kuuliza kwa kuzingatia topic hapo. naamini una majibu yakutosha but ili tuende vizuri ningependa nikuulize moja ujibu moja then tuendelee.

SWALI LA KWANZA.

Umesema kuna majini aina mbili, 1 majini wema/wazuri na hapo umesema maruhani ndio wazuri na waliobaki ndio jini wabaya.

Je, hao majini wabaya (ambao sio maruhani) wanataka nini hasa kwa watu? maana kuna friend wangu anao wanne na wote wanamlinda but walimtaka rafiki awe anafanya dawa (uganga) ila kutokana na wazazi wa rafiki walikataa hilo na hatimaye walimtaka rafiki aoe na amesha oa. jee unafikiri ni nini kitafuata? do you think kwa vile walimtaka aowe na amesha owa ndio itaishia hapo?
 
kiukweli kwenye biblia hakuna somo la majini wazuri wala wabaya wote ni mapepo sasa usilazimishe watu

nimekusoma vyema moeleven. but do you think ametumia luga nzuri kuwakilisha wazo hilo?

swali la pili.
jee unaijua vizuri bible?

kama unaijua niambie imezungumzia nini kuhusu majini?

kama hujui mimi nitakwambia.

karibu tujadili.
 

Safi sana kiongozi.
umeuliza swali moja miongoni mwa maswali niliyoyafrem ingawa umeuliza kwa mtindo tofauti.

nasubiria akujibu ili nijue naendelea wapi pindi nitakapomuuliza swali hilo.
 
Only in Tanzania, majini wanashauri watu...

Huo ni uongo usio na mfano.
sadly nakumbuka ulisema unafanya karesearch juu ya uchawi na majini. kitendo cha kusema majini wanashauri Watanzania tu nadaut research yako!!!

Too hoojja.
 
Uongo mtupu.

Vizuri sana.

I hope utakua na nondo za kutosha kuhusu hii mada.

na kama hatutoshindwana ningependa tujadili hapa.

kwa kuanzia tu naomba uthibitishe uongo wa hii mada.

i hope utaweka reference kwa madai yako.

plz come up.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…