Kwa wale wenye "MAJINI" vichwani au pembeni yao

Kwa wale wenye "MAJINI" vichwani au pembeni yao

Mimi sijaingia deep ila nimekosoa hayo maneno yako si lengo la kuendelea kutoa somo. Kama upo kwa nia njema, usipotoe watu..

[emoji2]ukaamua unipige mkwara kama unanijua vile, ukiniambia hayo ya kufuatwa na Jini naona kama stori maana Mungu ndiye mlinzi wangu nikilala naomba ulinzi wake. Kuna wa kimtisha na hayo ila si mimi
Vema sana kama unamtegemea mungu lakini bado hujawajua vema majini endelea na utabib
 
[emoji2] Mbona yule uliyesema anakuja jana sijamwona, nilimsubiri kwa hamu
Hata kama umemuona huwezi kusema mradi umeanza kwa kupinga huta jua ulifanyalo huyu huja kila siku kukusalimia na hukupa maelekezo fulani fulani lakini vile unamasihiri yako mwilini siku zingine hukumbuki hata ndoto unazoota, taja jina lako na la mama nikwambie tu kwa msaada vitu ulivyo navyo,
 
Hata kama umemuona huwezi kusema mradi umeanza kwa kupinga huta jua ulifanyalo huyu huja kila siku kukusalimia na hukupa maelekezo fulani fulani lakini vile unamasihiri yako mwilini siku zingine hukumbuki hata ndoto unazoota, taja jina lako na la mama nikwambie tu kwa msaada vitu ulivyo navyo,
Haya unakomalia ubishi, haya litaje lina la mama yangu
 
Umeweza jua hayo ambayo hayajanipata si bure walijua pia, nitajie basi. Si uniulize mimi,
 
Mkuu Rakims nna maswali mengi ya kuuliza kwa kuzingatia topic hapo. naamini una majibu yakutosha but ili tuende vizuri ningependa nikuulize moja ujibu moja then tuendelee.

SWALI LA KWANZA.

Umesema kuna majini aina mbili, 1 majini wema/wazuri na hapo umesema maruhani ndio wazuri na waliobaki ndio jini wabaya.

Je, hao majini wabaya (ambao sio maruhani) wanataka nini hasa kwa watu? maana kuna friend wangu anao wanne na wote wanamlinda but walimtaka rafiki awe anafanya dawa (uganga) ila kutokana na wazazi wa rafiki walikataa hilo na hatimaye walimtaka rafiki aoe na amesha oa. jee unafikiri ni nini kitafuata? do you think kwa vile walimtaka aowe na amesha owa ndio itaishia hapo?[/QUOTEkama walitaka awe mganga bc atakuwa tu pia walimwambia aoe kwasababu wao hawapendi uchafu(zinaa)
 
Kwa KUANZA Naushusha UZI Huu Maalumu Kwa Watu Mwenye Marohani/Majini WASAFI Yaani ASIE Kutesa Wala Kukushurutisha Yupo Tu Labda Kukushauri Au Mambo Mengine Sizungumzii Kuwaalika Watu Hapa Wasio Na MAJINI vichwani au Ndotoni Tofauti Na Majini Wachafu(pepo mbaya).... Wala Wasioamini Uwepo Wa Hawa Viumbe.. wala wenye imani (-) na Hawa Viumbe HIVYO tafadhali Kama Haikuhusu KAA Mbali na Huu UZI....

Kwa Kuanza:

Majini ni viumbe ambao wameumbwa kwa Moto na walikuwa wakiishi duniani kabla ya binadamu miaka Milioni nyingi iliyopita.
Viumbe hawa wana tabia kubwa mbili;


Yaani ya kibinadamu kwa maana wanakuwa wanafanya mapenzi, wanazaa na wanakufa.
Tabia nyingine ni ya Kimalaika ambayo ni kwamba wana uwezo wa kujigeuza katika umbo lolote wanalotaka na vile


vile wanaruka na kwenda wanakotaka au kupita wanakotaka bila kutumia chombo chochote.
Taifa la Majini limegawanyika katika makabila Milioni Sabini na mbili (72,000,000) na wana uwezo wa kujifunza lugha yeyote wanaoitaka.


Idadi ya Majini ni kila Binadamu mmoja kuna Majini 300 na wanaishi katika Majumba yetu, kwenye Miti, Majangwani, Kwenye Mapango na Sehemu zenye Misitu Mikubwa.

Majini wako katika aina Mbili (2); Maruhani na Mashetani.
Maruhani ni Majini wema ambao wanamtii Mwenyezi Mungu na wanawasaidia Binadamu katika mambo mengi.
Mashetani ni Majini Waovu ambao ni wakorofi na wanawaletea Watu madhara na Matatizo mara kwa mara.




Majini Ni Viumbe Ambao WAPO Kama WANAADAMU Kwa kuwa na free wills yani maamuzi ya uhuru kwamba naamini au siamini iwe katika mungu au shetani.. sita waelezea sana kwa maana wameshaelezewa sana ila mimi napiga mng'arisho au msasa ili ufahamu wa watu uzidi kuongezeka..

VIUMBE Hawa wamegawanyika makundi mawili wapo waliomuamini mungu mmoja hawa huitwa marohani na wapo ambao hawajaamini wanamfuata shetani pia wao wanaitwa mapepo wachafu au majini wabaya mradi tu wawekwe kwenye ubaya ubaya..

ila wao kwa jina la kundi tunaweza kuwaita walioasi au waislamu huwaita makafiri wa kijini na wakristo huwaita mapepo wachafu.

Pepo wachafu au makafir wa kijini kwa ujumla majini waliumbwa kabla ya wanaadamu na walipewa machaguo ya uhuru wengi wao wakamuasi mwenyezi mungu ndio amri ikashuka kwamba waangamizwe wote na malaika viumbe watiifu wakashuka na kuja kuangamizi majini wengi..

Lakini hawakuangamizwa wote kwa maana wengine walipewa uwezo na mwenyezi mungu kuingia popote vyovyote hivyo waliingia majabarini chini ya mabahari na wengine waliingia katika matumbo ya wanyama..
.
vile malaika hawakupewa uwezo huo wakarudi na kumtaarifu mwenyezi hali halisi ndipo wakaruhusiwa kuwaacha wale waliokimbia....


Baadhi waliogopa sana kwa kuona mwenyezi mungu ni mkali wa kuadhibu wakaanza kutubu ndio hawa huitwa leo Majini wema Au Maruhani..


Waliobaki wengine walijiona wenye nguvu na waliweza kujihisi wamemkimbia mwenyezi na Wakaendelea Kufanya Maasi Yao...

kitu kingine watakiwa kujua majini wapo mara 300 yako wewe yani kila binaadamu wapo mara idadi hiyo yake Viumbe Hawa huishi miaka mingi wengine hufika hadi miaka 1000/-

majini wema hawamkalii mtu kwa ubaya humpenda na kutamani kumsaidia.. hawampotoshi imani yake alionayo humuangalia tu nakumsaidia mambo mengi tu bila kujijua kama mtu kufaulu vema bila kujijua wala kusoma sana, kupendwa pendwa na watu, kupenda mambo ya kiroho zaidi kuliko ya kimwili, humfanya mtu awe na huruma.

Kumletea ndoto njema akilala na humpunguzia maumivu ya mwili bila kujijua.. kumfanya afikirie jambo jema mtu hadi alifanye.. hawana roho mbaya hulia pale unapofanyiwa ubaya wengine hupanda kichwani na kulia sana pale unapouziwa wengine hukupitishia kitu kama hope rohoni au barafu unajiskia umekaa sawa na kusema one day yessss! huomba pamoja na wewe pale unapotupa malalamiko yako kwa mwenyezi mungu kwa imani yako....

majini wabaya au pepo wachafu humfunga mtu riziki zake na humrudisha nyuna mtu mambo yake na kumbaka kumfedhehesha mpaka akaanza kumkufuru mola wake, na kuanza kujihusisha na ushirikina ndio anaona anafanikiwa humnyanyasa ndotoni kwa kuota anakimbizwa anapigana anatukanwa.. anadhalilishwa anaumwa anateswa na akiamka anakuwa hana raha... humjaza mtu ujasiri anapotaka kufanya tukio chafu....


jinsi ya kujijua kama una jinni:

MSAFI/MCHAFU AU Huna tu

kwa kuwa hawa ni viumbe tuwafananishe na bacteria wanapokuingia huwaoni lakini madhara mwili unapata...

ZIFUATAZO NI DALILI ZA KUJUA KAMA UNA JINI MSAFI AU MCHAFU KIIMANI
..


1: Kuumwa kichwa kisichojulikana mwanzo wala mwisho mradi tu kinauma kila siku muda wowote

2. Uzito ktk Mabega au hata kichwani kwenyewe.


3. Kuota vitu vya kutisha usingizini

4. Kuchukia kuona au kuolewa km bado hujaoa au kuolewa.

5. Kwa alie Oa au kuolewa huchukia Tendo la ndoa

6. Kupatwa na maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au baada

7. Baadhi ya wanawake hukosa Maji maji katika UKE wakati wa kufanya tendo la ndoa na hivyo wakati mwingine hupatwa na michubuko endapo lita lazimishwa tendo hilo

8. Baadhi ya wanaume hushindwa kumalizia vizuri tendo la ndoa au kumaliza haraka zaidi na kisha kupatwa na usingizi Mzito Mara tu baada ya kumaliza Tendo la ndoa.

9 Km una mke au Mme hutaki kufanya nae tendo la ndoa na usiku huo ulio kataa unaota unafanya na mtu mwingine.

10.Kuwa na hasira za ajabu wakati wa kuamka asubuhi.

11.Wakati mwingine huona km kuna mtu kakuinamia wakati ukiwa umelala taa imezima(kiza)

12.Wakati mwingine huhisi km kuna mtu anatembea ndani ya chumba ulicho lala. Ukijaribu kuwa makini kumsikiliza au kuwasha taa humuoni mtu yeyote.

13: kujilaumu hadi kuhisi kulengwa na machozi kwa kosa dogo tu

14: kuchukia kutumwa na hupenda kujiajiri

15: kuchukia sana dhambi

16: ukikaa sehemu ya kimya sana unasikia watu wanaongea kichwani

17: kuota unasali kila mara hali ya kuwa kama unajilazimisha kusali ikiwa imekupita hata sala moja

18: kustuka saa nane usiku baada ya kuota umeamshwa kusali au adhana ya kwanza kwa mwislamu

19: kuota unamuombea mtu na mwili wako kujaa nguvu kwa mkiristo

20: kuota unaongea na kiumbe asiekuwa binaadamu either mnyama au ndege..

zipo hizo ni baadhi tu.. hii ni fursa kwako wewe mwenye majini kujitambua je ulionayo ni mema au mabaya? na unayatumia au yanakaa tu? unayatoa au unabaki nayo unaongeza elimu ili usimkufuru mwenyezi kwa kuwa na majini....

karibuni
P.M Namba Yako Tutengeneze group ya WHATSAPP Ya watu wenye maruhani tufundishane namna ya kuwatumia vema ili wasitupotoshe ikiwa unao na unajificha basi kumbuka huwezi kukimbia kivuli chako..


Walikupeleka wapi walikufundisha nini? yapi ya ajabu uliyaona? yapi yalikufanya ukainua mikono juu ukasema kweli mwenyezi umeumba hawa viumbe? haya na mengine mengi tutayaangalia humo kwenye group.

kuna watu hawana na wanawish wawajue na wawe nao nafasi zipo 15 tu na kuingia kwenye group jini wachafu hatuta fundisha...
. 30 wale wenye marohani wasiojuwa jinsi ya kuwaongoza na kuwatumia...


karibu tujadiliane....

#Rakims
Mzee ni add kweny hilo group namba zang hizo 0768174787
 
Nime yatafuta sana tangu 2001 nikapata shetani sio maruhani kwa sababu ilikua nikiomba kitu yana hitaji ujira japo nikidogo nikawa na vumilia nilikuja kuchoka yalipo omba dam ya njiwa
 
Nime yatafuta sana tangu 2001 nikapata shetani sio maruhani kwa sababu ilikua nikiomba kitu yana hitaji ujira japo nikidogo nikawa na vumilia nilikuja kuchoka yalipo omba dam ya njiwa
Mkuu ruhan ukimwambia kitu anafanya kisha anaondoka zake ila pale anapoanza kukwambia nichinjie jua sio ruhani ni shetani, na wengi wana mashetani hawana ruhani wanashindwa kutofautisha maana, ruhani huyo huyo ndio wakristo huita roho takatifu

Rakims

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majini wazuri?! Hamna jini mzuri katika ukristo labda uislamu, katika ukristo, mungu kaumba malaika, hao majini walihasi
kwa hhiyo majini waliumbwa na nani? au walijiumba wenyewe naomba unieleweshe mkuu
 
Back
Top Bottom