Niende moja kwa moja
shirki ni kufanya kitu katika aina za ´ibaadah kumfanyia asiyekuwa Allaah .
Ibada zipo za aina nyingi zinazochukuliwa kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Hivyo basi, yule mwenye kufanya kitu katika aina ya ´ibaadah hizi kwa asiye Allah, basi huyo ni mshirikina ambaye kafanya shirki kubwa inayomtoa katika Uislamu.
Mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, akaweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah, akasujudu kwa asiyekuwa Allaah, akamuomba asiyekuwa Allaah,akamtegemea asiyekuwa allah katika wafu na viumbe vilivyoko mbali, akawataka uokozi wafu,majini n.k., huyu kamshirikisha Allaah (´Azza wa Jall). Kwa sababu ´ibaadah kwa aina zake zote ni haki ya Allaah (Azza wa jall).
Jua kuwa hakuna jini mzuri anayeingilia maisha ya binadamu jini ni kiumbe kama mimi na wewe na ameumbwa kwa dhumuni moja na sisi ambali ni kumuabudu Allah pekee .
Unapotaka muongozo kutoka kwa majini either elimu au chochote hauwezi kufanya hivyo bila kuyaita au yenyewe yawe yamekukalia hii inamaanisha umemuona allah hana msaada kwako umeshindwa kutumia alivyokubariki navyo sasa unayafuata majini yakupe muongozo?
Kuna watu mnachafua dini kwa makusudi hakuna sehemu kwenye uislamu umeabiwa utegemee asiye allah.