Hauna uhakika kipi ninefanya siku tatu nyuma na siwezi kukwambia ila kwenye ukweli lazima tuambiane mkuu hauwezi kutangaza shirki hadharani na kuisifia kama ni kitu kizuri ,ama kweli ni moja ya dalili za kiama "vitu vya haramu vinapewa majina mazuri mazuri".
Nikuukize swali moja " siku za mwezi wa ramadhani huwa unaweza kuyaita hayo majini yako?"
Bado sana mkuu huna hoja. Unanikumbusha mzinzi mmoja alikuwa anawaambia wenzie ni dhambi kutongoza mwanamke hali ya kuwa yeye anawazini kwa kutumia nyuso mbili kama hapa unavyochacharika kuniambia nafanya shirki kwa username ya tungo.
wakati huo huo una uchafu unaoufanya nyuma ya pazia ni mekushauri kusoma hivyo SOMA!
wachawi wa kiganga peke yake ndio hufunga vikoba mwezi mtukufu wa ramadhani na hivyo hivyo wapumbavu hufanya ibada na kujipinda zaidi mwezi wa ramadhani na baada ya hapo hurudi katika maasi yao kwa swali lako hili tu linaonyesha unaunafiki hata wa imani kwa maana yawezekana ni mmoja kati ya watu wanaoabudu mwezi bila kujua.
Ingekuwa kiumbe ninachotumia ni shetani basi mwezi huu mimi na wewe na waislamu wengine tunaamini kuwa shetani yupo kifungoni lakini kwa sisi watu wa maarifa mkuu Mwenyezi Mungu yupo kila siku na kila saa na thamani yake haishuki hata sekunde moja na ukubwa wake na kumtii hatuoni kama ni sehemu specific peke yake kama ndani ya ramadhan kipindi cha eid au sala za ijumaa pekee sisi Mwenyezi Mungu yupo pia katika kila inch ya sekunde na anaona na anafanya anayoyataka na tunamuhofia kila siku,sekunde na saa.
Bila kwenda mbali na swali lako la kwamba "siku za ramadhani huwa unaweza kuyaita hayo majini yako?
JIBU NI KWAMBA:
Majini sio yangu ni viumbe vilivyoumbwa na yule aliyekuumba wewe navyo vina machaguo huru ya kuamini na kutoamini navyo popote ulipo katika mazingira yako vipo chooni chumbani sitting room mpirani na kila kona ya ulimwengu wapo nao wapo kanisani(roho safi/chafu) wapo misikitini(Maruhani/majini) wapo katika temple (budhas spirits) wapo kwenye majengo ya mashetani na kila sehemu ambazo wamepewa uwezo wa kufika.
Wapo ndani ya mwezi mtukufu wa ramadhani(kasoro shetani mpotoshaji na wafuasi wake)
sasa labda kama umenithibitisha ninachotumia ni shetani/mashetani kama wale unaoenda wakufanyie maombi mwezi huu na wanakwambia hawafanyi maana yake hakuna wanachotegemea isipokuwa ni shetani nao hufungua vilinge baada ya ramadhani kuisha na wanakuwa hawajafanya kitu ila kutii mwezi.
Nami sio mmoja wao wewe huwezi kunielewa ila tu kama ungekuwa ni mtu wa maarifa nisingepoteza muda kujielezea.
Rakims