Kwa wale wenye umri wa miaka 50 na kuendelea unakumbuka jiji la Dar mwaka gani?

Kwa wale wenye umri wa miaka 50 na kuendelea unakumbuka jiji la Dar mwaka gani?

Na sisi makabwela usafiri wetu ulikwa DMT.
403108171589b2642597af177ec05071.jpg

Hapo ni mnazi mmoja ghorofa linalooneka upande wa kulia opposite kuna mnara wa mashuja watoto wa mji nani anakumbuka Bar maarufu iliyokuwa kwenye ghorofa hilo?
MziziMkavu
Zamiluni Zamiluni
 
"Pijo" 504, 506, VW- mgongo wa chura na Combi, pamoja na Morris ndio zilikuwa nyingi, Landrover 109 ndio zilikuwa gari za serikali, polisi wao walikuwa sana kwenye "Pijo" family
Nafikiri pijo 403 ndizo zilikuwapo miaka hiyo,504 zimekuja late 70s kama sikosei
 
Kumbe unafahamiana na kina Bobeya,Mussa Simba na Eddie Manji ndugu yake Machismo? na Congo united ulicheza na kina Leny Simba (Obua) na Feruzi? Red Star kiongozi akiwa Mzee Lumelezi au Kesi Mjinga? Pan Africa unanitia wasiwasi kama ulikuja kwa sababu wee Abijo! [emoji13] [emoji12] maana Mzee Mangara Tabu asingekuku
bali
Jamani mmenikumbusha class mate wangu Mussa Simba tulisoma wote Tambaza nae akiichezea Congo United miaka hiyo.Mwenye taarifa zake tafadhali anicheki inbox.Natanguliza shukrani.
 
Mkuu Zamiluni mi nimesoma St Joseph Mwalimu wangu mkuu alikuwa Mrs Simkoko! Snow cream na Fish and Chips maeneo ya Shesh Mahal na Topaaz ndiyo anga zangu. Beano,Dandy,Topaaz ndiyo Comic zangu. Unataka ni kwambie kitu! sikukuu ya Idd nilikuwa natembelea wapi utotoni? Mji umeharibiwa! kidongo chekundu ndiyo maeneo yetu! Mnazi mmoja garden pamevurugwa hata chemchem hazirushi maji na samaki hakuna kwenye ile sanamu inatoka maji! Viatu nilivyokuwa navaa ni Prefect za Bata![emoji23] mi nilikuwa hodari wa kutengeneza kishada/tiara[emoji324]
Lakini klabu yangu ni ile ya mitaa ya Mafia na Nyamwezi [emoji460]
Mi ni kama Robinson cruise

Namshukuru Mwenyezi Mungu nimeona mengi alhamdulillahi.
Mkuu umemaliza kila kitu yaani hayo ndio yalikuwa Mapito yetu haswa.Nimekumbuka mbali sana mkuu
 
Usafi na heshima kwenye mazingira wakati huo unawezekana ulikuwa sawa na Ulaya.

Wakati huo si unaona Barabara hata vumbi wala kipande cha sigara hukuti. Ni hivyo hivyo hata mitaa yetu ya Kariakoo kwa siku hizo. 1967 ndiyo kila kitu kikaanza kuvurugika.
 
Mie nimeona hiyo 1964 baba alinitembeza mitaa hiyo Mara kwa Mara.
 
Ngoja ni cross check kwenye kumbukumbu kama ulikubalika kote kote if you don't mind unipe hint Pan ulicheza na kina nani please?
Zamiluni Zamiluni

Ataje orodha ya Pan ndio utamjua. Kuna wachezaji panga pangua watakuwemo katika list. GM, CK, RM, SMC, KM, KM, SM, IK, JPM, MRA, PT, MM na wengineo.
 
Back
Top Bottom