Kwa wale wenye umri wa miaka 50 na kuendelea unakumbuka jiji la Dar mwaka gani?

"Pijo" 504, 506, VW- mgongo wa chura na Combi, pamoja na Morris ndio zilikuwa nyingi, Landrover 109 ndio zilikuwa gari za serikali, polisi wao walikuwa sana kwenye "Pijo" family
Nafikiri pijo 403 ndizo zilikuwapo miaka hiyo,504 zimekuja late 70s kama sikosei
 
Jamani mmenikumbusha class mate wangu Mussa Simba tulisoma wote Tambaza nae akiichezea Congo United miaka hiyo.Mwenye taarifa zake tafadhali anicheki inbox.Natanguliza shukrani.
 
Mkuu umemaliza kila kitu yaani hayo ndio yalikuwa Mapito yetu haswa.Nimekumbuka mbali sana mkuu
 
Usafi na heshima kwenye mazingira wakati huo unawezekana ulikuwa sawa na Ulaya.

Wakati huo si unaona Barabara hata vumbi wala kipande cha sigara hukuti. Ni hivyo hivyo hata mitaa yetu ya Kariakoo kwa siku hizo. 1967 ndiyo kila kitu kikaanza kuvurugika.
 
Mie nimeona hiyo 1964 baba alinitembeza mitaa hiyo Mara kwa Mara.
 
Ngoja ni cross check kwenye kumbukumbu kama ulikubalika kote kote if you don't mind unipe hint Pan ulicheza na kina nani please?
Zamiluni Zamiluni

Ataje orodha ya Pan ndio utamjua. Kuna wachezaji panga pangua watakuwemo katika list. GM, CK, RM, SMC, KM, KM, SM, IK, JPM, MRA, PT, MM na wengineo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…