Kwa wale wenye umri wa miaka 50 na kuendelea unakumbuka jiji la Dar mwaka gani?

Shikamoo mkubwa
 
Wakati huo ukienda Private hospital kwa matibabu ilikuwa hayazidi Tzs 3 hadi nne basssss...
madokta wa kweli na wenye huruma na mwili!!
Duh ZZ naona stori za 60s na 70s zimemvuta kaka Mtebetini.Mzizi Mkavu Ubarikiwe Mkuu
Miaka ya 70s nilikuwa nakuja Dar Toka Dom
Na reli,mabasi ya Kamata Na mabasi ya railways wakati huo Shaban Robert secondary ilikuwa secondary kweli
 
Mie nimeshangazwa na usafi hasa kwenye hiyo picha ya kwanza na jiji kutokuwa na watu.

Mkuu BAK juzi uliweka list ya miji michafu duniani Dar ilikuwa ya 12.
 

Kaka Mtebetini kama hiyo ndio ilikuwa mitaa yako basi itakuwa nimekuona mtaa wa Kipata Kwa mzee Abdulrahmani Miaka hiyo ya 70
 
Hapo ndiyo pale sasa wanafanya sherehe za mashujaa, opposite na Cooperative Building, Kidongo Chekundu. Maarufu "Garden".
1967 nikiwa form one....how old were you..?
Kama sijakosea Lumumba ndiyo ikiitwa New Street
 
Muhaji muki
Mohamed yahya tostao
 
Kaka Mtebetini kama hiyo ndio ilikuwa mitaa yako basi itakuwa nimekuona mtaa wa Kipata Kwa mzee Abdulrahmani Miaka hiyo ya 70

Mnakumbuka pale karibu na taa za fire kulikuwa na hoteli moja jina limenitoka. Pilau ilikuwa shilingi 1 na senti 50. Nusu Pilau ilikuwa senti 75. Wanafunzi wa Azania pale lunch safi sana tukichoka ile mihogo ya kukaanga na juisi ya machungwa ama ukwaju ya saa nne asubuhi shuleni. Huo ni mwaka 1971.
 
Mie nimeshangazwa na usafi hasa kwenye hiyo picha ya kwanza na jiji kutokuwa na watu.
Wajanja walikuwa bado kuingia mjini. Uzazi wa mpango ulikuwepo sio sasa tumekuwa wengi isipo Wahindi walikuwa wengi sana mjini miaka ya late 70s na 80s Wengine tulikuwa shule za awali
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…