Kwa wale wenye umri wa miaka 50 na kuendelea unakumbuka jiji la Dar mwaka gani?

Kwa wale wenye umri wa miaka 50 na kuendelea unakumbuka jiji la Dar mwaka gani?

With due respect usinichokonoe hunijui sikujui so keep your distance from me. Mimi sio wa kuhadithiwa mambo ya mji huu!unapajuwa Tuwatugawe? unapajuwa kwa Pipino? unaujuwa mtaa wa Donge au Chura please kuwa na heshima Mzizima ina wenyewe na for your information neno sahihi la kiswahili fasaha si
umeadisiwa =umehadithiwa
Zamiluni Zamiluni thanks huyu jamaa yako aliyeni-tag akiutaja mtaa wa New Street upo wapi leo hii uni pm nikutumie laki umzawadie it's a promise!
Shikamoo mkubwa
 
Wakati huo ukienda Private hospital kwa matibabu ilikuwa hayazidi Tzs 3 hadi nne basssss...
madokta wa kweli na wenye huruma na mwili!!
Duh ZZ naona stori za 60s na 70s zimemvuta kaka Mtebetini.Mzizi Mkavu Ubarikiwe Mkuu
Miaka ya 70s nilikuwa nakuja Dar Toka Dom
Na reli,mabasi ya Kamata Na mabasi ya railways wakati huo Shaban Robert secondary ilikuwa secondary kweli
 
Mkuu Zamiluni mi nimesoma St Joseph Mwalimu wangu mkuu alikuwa Mrs Simkoko! Snow cream na Fish and Chips maeneo ya Shesh Mahal na Topaaz ndiyo anga zangu. Beano,Dandy,Topaaz ndiyo Comic zangu. Unataka ni kwambie kitu! sikukuu ya Idd nilikuwa natembelea wapi utotoni? Mji umeharibiwa! kidongo chekundu ndiyo maeneo yetu! Mnazi mmoja garden pamevurugwa hata chemchem hazirushi maji na samaki hakuna kwenye ile sanamu inatoka maji! Viatu nilivyokuwa navaa ni Prefect za Bata![emoji23] mi nilikuwa hodari wa kutengeneza kishada/tiara[emoji324]
Lakini klabu yangu ni ile ya mitaa ya Mafia na Nyamwezi [emoji460]
Mi ni kama Robinson cruise
Namshukuru Mwenyezi Mungu nimeona mengi alhamdulillahi.

Kaka Mtebetini kama hiyo ndio ilikuwa mitaa yako basi itakuwa nimekuona mtaa wa Kipata Kwa mzee Abdulrahmani Miaka hiyo ya 70
 
Hapo ndiyo pale sasa wanafanya sherehe za mashujaa, opposite na Cooperative Building, Kidongo Chekundu. Maarufu "Garden".
1967 nikiwa form one....how old were you..?
Kama sijakosea Lumumba ndiyo ikiitwa New Street
 
Kwa faida ya wadau nimeona niyatoe majina kwa ukamilifu.

GM - Gordian Mapango
CK - Charles Kilinda
RM - Roma Mapunda
SMC - Salum Mwinyimkuu Carlos
JM - Jella Mtagwa
KM - Kitwana Manara (Popat)
KM - Kassim Manara
SM - Sunday Manara (Kompyuta)
IK - Ibrahim Kiswabi
JPM - Juma Pondamali Mensah
MRA -Mohammed Rishard Adolf
PT - Peter Tino
MM - Mohamed Mkweche

Kama nimesahau wengine naomba mwongezee.
Muhaji muki
Mohamed yahya tostao
 
Kaka Mtebetini kama hiyo ndio ilikuwa mitaa yako basi itakuwa nimekuona mtaa wa Kipata Kwa mzee Abdulrahmani Miaka hiyo ya 70

Mnakumbuka pale karibu na taa za fire kulikuwa na hoteli moja jina limenitoka. Pilau ilikuwa shilingi 1 na senti 50. Nusu Pilau ilikuwa senti 75. Wanafunzi wa Azania pale lunch safi sana tukichoka ile mihogo ya kukaanga na juisi ya machungwa ama ukwaju ya saa nne asubuhi shuleni. Huo ni mwaka 1971.
 
Mie nimeshangazwa na usafi hasa kwenye hiyo picha ya kwanza na jiji kutokuwa na watu.
Wajanja walikuwa bado kuingia mjini. Uzazi wa mpango ulikuwepo sio sasa tumekuwa wengi isipo Wahindi walikuwa wengi sana mjini miaka ya late 70s na 80s Wengine tulikuwa shule za awali
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom