Kwa walio Dar es Salaam tu: Hili ndilo suluhisho la uhakika kukabiliana na gharama zilizopanda za internet

Nipo hapa natamba na Zuku Fiber nishasahau bei za bando, data na speed limits toka mwaka juzi
 
Dunia inaondoka kwenye mifumo ya analog kwenda wireless! Wewe unakuja na idea ya kuunganisha miwaya kama TTCL!
Cable bado zipo hata Ulaya. Unaletewa cable ila unaunga kwa router
 
Dunia inaondoka kwenye mifumo ya analog kwenda wireless! Wewe unakuja na idea ya kuunganisha miwaya kama TTCL!
Ni fiber internet, the modern whole internet infrastructure runs on underwater fiber cables usichanganye na ADSL za TTCL
 
Umesema elfu70?!! Umenikumbusha kuna watu walikuwa wanaandamana bei ya mkate kupanda. Mwanamfalme kusikia hivyo akasema kama mkate umepanda si wale keki!
Internet kwa dunia ya sasa ni kama basic needs.. ila tutaoneshana makali tu
 
Inabidi tu tukutane Kibo Tegeta juma 2 jioni tulijadili hili aisee turudi tu kwenye p.o Box! Au watu wa Tegeta tuta ruhusiwa kwenda kufanyia kikao juliana 😂
Tutafanya semina zote za kuwapaka choo hawa mafisiem pale Juliana. Wameshatukoroga sana nafsi, kila member ahakikishe ana pepper spray ili wale vijana wa sirro wakileta mbwembwe waseme nazo wakati tunatoka nduki.
 
Mbona haujatoa suluhisho, hicho ulichoelezea ni saws na simu za zamani za mezani, watu wanataka mobile.
 
1.Kama una familia kitasaidia kuoungiza gharama za kila mtu kujinunulia data

2.unapata channels za kingamuzi cha zuku

3.utatumia bila kikomo, hata ukitumia gb 20 kwa siku ni wewe tu, nenda hata halotel uulizie hio gb 20 kwa siku sh ngap .
kwaio nikitoka nyumbani sipati internet au?
 
Kumbe huko Dar 70k ni ndogo. Kweli mpo uchumi wa katikati. Yule waziri aliyesema mbadala wa bei kubwa ya sukari ni kutumia asali, alikuwa sahihi.
Akasahau kuwa chupa Moja ya asali, ile ya konyagi napa, Siyo faru John, ni Elfu 10-15.

Kama mkate gharama nunueni keki. Hata wale majani ndege ya Rais itanunuliwa.
 
Tutafanya semina zote za kuwapaka choo hawa mafisiem pale Juliana. Wameshatukoroga sana nafsi, kila member ahakikishe ana pepper spray ili wale vijana wa sirro wakileta mbwembwe waseme nazo wakati tunatoka nduki.
Dah nimecheka kweli mkuu au upupu!
 
Mkuu tumia lugha rahisi wengine sisi darasa la tatu D
Hahah samahani mkuu, FTTH maana yake ni "fiber to the home", kwa mantiki ya kwamba miundombinu ya fiber inasogwezwa hadi mahali watu wanapoishi kama vile tu unavyoona huduma ya simu za mezani, maji na umeme...

Kwa nchi zilizoendelea hii ipo sana na huduma hizo almaarufu kama cable ambapo mtu hupata internet, voice na entertainment (Tv)...

Sasa TTCL yeye hana hizi huduma kwa miundombinu ya fiber yake kwenda kwenye makazi ya watu, isipokuwa ana mkongo wa taifa "NICTBB=National ICT broadband backbone" ambao wenyewe ni mahususi kwa ajili ya kubeba taarifa za internet na mambo mengine ya kimawasiliano kati ya Dar es Salaam na mikoani na hata kuunga na nchi za jirani Rwanda, Malawi etc...

Mkongo wa taifa wa mawasiliano unaweza ukaumithilisha na mtandao wa barabara, kwamba atokee mtu ajenge barabara nchi nzima, halafu kila anayetaka kutumia barabara kwa ajili ya uchukuzi awe analipia matumizi hayo...

TTCL kajenga huo mkongo kwa nia mbili, mosi, mawasiliano ya kiserikali (nadhani umeshawahi ona mara kadhaa viongozi wa serikali wanafanya video conf) na mbili ni kwa ajili ya watumiaji wengine wakubwa kukodisha/kununua bandwidth (hapa ndio makampuni ya simu hununua bandwidth ili internet zao ziweze kufika mikoani) kwa ajili ya matumizi ya sisi watu binafsi na mitandao mingine ya kibenki, polisi n.k
 
Asante.
 
Ni kweli, nshanunua kifurushi cha 50k hapa maisha yanaendelea
 
Kuna mtu kaniambia Tigo 1.5 Gb ni sh 10,000.

Halafu linganisha na flat rate ya 70,000 kwa mwez (of course limitation ni mobility).
 
Walioko huko masaki jamani nikaribisheni kwenu nije na hii tekno yangu nikae hata getini tu Kisha nikimaliza nirudi zangu kiluvya
 
Kuna mtu kaniambia Tigo 1.5 Gb ni sh 10,000.

Halafu linganisha na flat rate ya 70,000 kwa mwez (of course limitation ni mobility).
2.5GB ni Tsh 10,000 hata sasa nimeshindwa kununua aisee
Natumia ya TTCL
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…