Mdogo wangu kama
ulivyoambiwa mwanzo ndoa hhuwa haina formular. mimi ndoa yangu ina miaka
minne nilianza kwa kufuata formular kutokana na kwamba nilikuwa nasoma
sana makala za shaluwa kwenye web ya shigongo. nikawa nafuatilizia kila
kitu. tulikuwa tunagombana sana na ke wangu coz kila nilichokisoma
nuilienda kukifanyiia kazi kwa mke wangu.
jambo la maana kwako jaribu kujiweka katika nafasi nyuma ya mkeo. yaani
kila jambo mpe mkeo kipaumbele, msifie kila mara hata pale ambapo
unajua hakufanya vizuri tafuta tu pointi moja umsifie ili ajiione
anapendwa na anakubalika. jambo lingine ambalo ndilo la muhimu kuliko
yoote jenga uhusiano na MUNGU wako kama wewe ni mkristo kama mimi
jitahidi usali pamoja na mkeo, na kuwa mstari wa mbele kwenda kanisani,
kama wewe ni mwislamu vilevile. mleteee zawadi mkeo kila mara mara 2 ama
3 kwa wiki hivi. sio lazima zawadi kubwa hata kama ni pipi, chokolate
ama chochote ili mraddi tu ajue kuwa unapokuwa mbali na yeye huwa
unamkumbuka. kama wewe ni mfanyakazi ukisafiri usirudi bila zawadi ya
kueleweka kama nguo, kitambaa, viatu ,mkoba na chochote kile
utakachoone. katika siku yako tenga muda wa kukaa na mkeo mkiwa wawili
kabla ya kulala. na wanawake maranyingi wanapenda kufanya mapenzi mchana
na asubuhi kuliko usiku maana usiku wanakuwa wamechoka kwa kazi nyingi
za mchana kutwa na wanahitaji pumnziko so epuka kudai unyumba muda mfupi
tu baada ya kwenda kulala. pia muone mkeo ndo mwanamke pekeee mzuri
duniani tena msifie mara kwa mara kwa uzuri alionao na ukiwa unasema
hayo mwangalie usoni usiseme ukiwa umeficha uso ataona unamdanganya. pia
wakati wa mamboz wanaume wengi akimaliza tu anageukia upande wa pili,
hiyo ni sumu ya penzi mwanamke anapenda kukumbatiwa mara mmalizapo mambo
yenu kwani hujiihisi kuwa hana thamani tena baada ya kukupa uroda so
kulifuta hilo just endelea kumkumbatia kwa dakika 15 hivi baada ya kuwa
mmemaliza kupeana shughuli. nawatakia ndoa njema