Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
WAKUU MIMI NINATAFUTA WATU WA 8 TUWEZI KUSHIRIKIANA KWENYE KUSINDIKA MAZAO NA KILIMO CHA MAHINDI, MAHARGE, ALIZETI, MBAZI NA UFUTA . WATU HAO (8) TUTACHANGA MTAJI WA KUNUNUWA TRECTA JIPYA AINA SWARAJ 744, TUTAKODI WOTE MASHAMBA YA KULIMA HAYO MAZAO. GHARAMA ZA KUNUNUWA TRECTA 28MILIONI, MAHINDI NA MBAZI TUNACHANGANYA KWENYE SHAMBA MOJA ALIZETI NA MAHARGE TUNALIMA TOFAUTI Eg Mahindi ekari 300 alizeti ekari 150 na maharge kama ekari 50. BAADA YA KUVUNA TUNAKOBOA SEMBE, KUKAMUWA MAUTA YA ALIZETI SISI WENYEWE, HUKU TUKIWA NA MALENGO YA MUDA MREFU KUWA SIKU MOJA TUTAMILIKI VIWANDA VYA KUSINDIKA MAZAO MBALI MBALI. TUNAWEZA KUSAJILI KIKUNDI OR TUSAJILI LTD CO. YETU . WADAU TUFUNGUKE KUTOA MAWAZO AMBAYO YATABORESHA. NAPATIKANA KUPITIA NAMBA HII 0765616178. (NAFAHAMU MAENEO MAZURI SANA KWA KILIMO NA MAENEO AMBAYO TUNAWEZA KUKODI MASHAMBA KWA URAHISI) TUNAWEZA FANYA FEASIBILITY STUDY YA HAYO MAENEO BEFORE
wilshere mawazo mazuri kama jinsi kijana Wilshere anayoitendea vyema Arsenali....big uppp.....
Hilo ni wazo zuri sana na la msingi ambalo vijana wa kitanzania tunashindwa kuchangamkia fursa kwasababu ya kufanya kitu mmoja mmoja matokeo yake ni matokeo hafifu. Idea ni nzuri na inawezekana kabisa, mimi nafahamu vijana wa nchi jirani (watani wa jadi) wenye kikundi kama hichi na hufanya kila kitu chenye kuleta faida kupitia kikundi chao...kwao ilikuwa rahisi maana wanafanya kazi sehemu moja ndipo waliamua kujiunga na kuanzisha kampuni yao, kwa sasa wanalima mpaka matunda na kuuzia viwanda vya juisi.
Kwakuwa wewe una-nia inabidi uwe mwanzilishi ujitahidi kuandaa mapendekezo katika maandishi na kisha kujaribu kupata vijana wenye usongo huo (mimi natamani pia). Sasa kwasababu ya kutofahamiana na hivyo kutoaminiana, ni vyema ikawa katika mfumo wa LTD COMPANY yenye katiba na MoU ili kuweka kila kitu wazi na haki na majukumu ya kila mshiriki wazi.
Kwa watu wa nchi za mbali haya mambo ya kukutana bar/chuo/restaurant/online na kuanzisha biashara inayofanikiwa ni jambo la kawaida sana. Ni wakati muafaka kwa sisi kuunganisha nguvu kuzitumia fursa chungu tele nchini....sio kuchangiana katika harusi tu.....mkuu mkijikita katika kilimo na kuainisha jinsi mnavyotaka kuondoa njaa, kuna mashirika na asasi nyingi zinazotoa funds/grant katika kilimo ikiwa mmjiweka rasmi....ni rahisi sana ku-lobby kama company na sio mtu mmoja mmoja.
Espirit de corps
mawazo mazuri yapo mengi sana tatizo ni nyenzo. hv unadhani watu wangekuwa na uwezo hata wa kukopa wangebaki hapa mjini na kuzunguka na vibahasha? hebu fikiria huo mtaji hapo. ni kijana gani wa kitanzani (graduate) hata yule hajaenda shule anaweza kupata mtaji huo? kwa harakaharaka tu hapo watu wanane angalau kila mtu atoe mil 7 mana hekari hizo ni nyingi sana
WAKUU MIMI NINATAFUTA WATU WA 8 TUWEZI KUSHIRIKIANA KWENYE KUSINDIKA MAZAO NA KILIMO CHA MAHINDI, MAHARGE, ALIZETI, MBAZI NA UFUTA . WATU HAO (8) TUTACHANGA MTAJI WA KUNUNUWA TRECTA JIPYA AINA SWARAJ 744, TUTAKODI WOTE MASHAMBA YA KULIMA HAYO MAZAO. GHARAMA ZA KUNUNUWA TRECTA 28MILIONI, MAHINDI NA MBAZI TUNACHANGANYA KWENYE SHAMBA MOJA ALIZETI NA MAHARGE TUNALIMA TOFAUTI Eg Mahindi ekari 300 alizeti ekari 150 na maharge kama ekari 50. BAADA YA KUVUNA TUNAKOBOA SEMBE, KUKAMUWA MAFUTA YA ALIZETI SISI WENYEWE, HUKU TUKIWA NA MALENGO YA MUDA MREFU KUWA SIKU MOJA TUTAMILIKI VIWANDA VYA KUSINDIKA MAZAO MBALI MBALI. TUNAWEZA KUSAJILI KIKUNDI OR TUSAJILI LTD CO. YETU . WADAU TUFUNGUKE KUTOA MAWAZO AMBAYO YATABORESHA. NAPATIKANA KUPITIA NAMBA HII 0765616178. (NAFAHAMU MAENEO MAZURI SANA KWA KILIMO NA MAENEO AMBAYO TUNAWEZA KUKODI MASHAMBA KWA URAHISI) TUNAWEZA FANYA FEASIBILITY STUDY YA HAYO MAENEO BEFORE
Natamani sana kuwemo, kikwazo ni kwamba, kwa sasa nina project moja kubwa na inapanuka kila siku,na hata wilshere anafahamu ninachosema.
Niko interested sana na kilimo cha vitunguu! Wadau wangu nipeni muongozo wa hili!
Uko tayari nikuunganishe na jamaa aliyewahi kulima kitunguu pale Ruaha Mbuyuni Iringa?