Kwa walio tayari kufanya kilimo cha mahindi, alizeti, mbazi na ufuta


Big up Mkuu wilshere umenigusa sana! Umekuja na wazo kubwa, you think big, it is a revolutionary idea ili watanzania tuende level ya juu zaidi. Badala ya kutumia zaidi simu naomba wakati mnaendelea kunong'onezana kwa simu mengine andikeni hapa tujadili, tuelimishane na tuamshane, hili wazo kilichonifurahisha ni kuona kuwa kumbe kwa watu 8 hadi 10 trekta la Mil 28 linanunulika na ninaujua mziki wa trekta kubwa, it is a good idea worth discussing. Unapatikana maeneo gani maana wasomaji tumetapakaa Tanzania nzima, sasa mtu uko Sumbawanga na mwingie Mtwara halafu tunakusanya nguvu pamoja na wa Dodoma na wa Mwanza, naomba kama ulivyokuwa specific kwenye idadi ya watu 8 ungesema na sifa zingine za washirika wako mfano unapendelea kuwekeza mikoa ipi, hivyo washirika wawe wakazi wa mikoa ipi, ukubwa wa mradi ulioubuni ni wazi ni kwa wenye mitaji mikubwa na ninajua hao wapo na watapatikana tu.
 

Heshima kubwa sana kwako Mkuu wehoodie najivunia sana uwepo wa Great thinkers kama wewe hapa JF, maneno uliyoandika hapo juu yanasisimua kwani ni ukweli halisi! Moyoni mwangu nime-bold na nimepigia mstari kila neno uliloandika! Ni wazi nguvu ya wanyonge ni umoja tu, mambo mengi ambayo ni magumu kufikiwa na mtu mmoja mmoja inawezekana kuyafikia kwa kukusanya nguvu! Mimi huwa nachukulia kuwa ni bahati sana unapokutana na watu wenye moyo wa kukusanya nguvu pamoja! Ukiishi eneo ambalo watu wanautamaduni wa kushirikiana huleta matumaini na raha maishani. Kwa kuwa na umoja ingewezekana kila mtu akawa na jambo la kufanya likafanyika na ndoto za watu wengi zikatimia!! Tatizo mkuu ni huyo mdudu aliyewahi kututafuna Tanzania kutokana na kufa na kuporomoka kwa ushirika na ujamaa Tanzania! Hilo limeshaua mioyo ya watu kufikiri kushirikiana! Watu wengi hawataki kusikia neno ubia, ushirikiano, ushirika. Watu wengi wanaogopa sana kuzikwa pesa zao! Ujanja wa kijinga umetawala Tanzania, watu wengi sana ni wajanja na ni wezi! Inakuwa ni vigumu kuijua dhamira njema ya mtu yeyote hasa anaekujana wazo kubwa, zuri na la akili kama hili.

Nakupongeza sana Mkuu kwa idea ya Limited company, pengine kwa thread hii ili iwe ni msaada kwa wasomaji tujadili zaidi ni mazingira gani au mkakati gani ambao mtu akidumbukiza pesa yake itakuwa salama kwa maana ya watu kutokuaminiana! Tuweke pembeni hasara za kibiashara hizo kwa mjasilia mali siziogopi lakini hizi za wajanja wa mjini kwa kweli zinatisha, tujadiliane jinsi ya kuepukana na kamba zao ili tuingie kifua mbele pasi kuogopana! Ninaamini kabisa kuwa shughuri hii ikianza lazima inaweza kupata support kubwa kutoka kwenye taasisi mbali mbali za kifedha.

Mkuu please tuelimishe zaidi ni jinsi gani mfumo wa Ltd Company unaweza kulinda maslahi ya wadau?! Je kwa uzoefu wako watu huwa wanaheshimu MoU na katiba zao ? Maana hizi nchi zetu ambazo tunashuhudia watu hawaheshimu sheria na wenye nguvu ya pesa wako above the law inakuwaje, tujadiliane hili kwanza wakati tunajipanga kwenda level hii ya juu!!
 

Ni kweli hekari alizotaja ni nyingi sana ila hapo ujue kuwa amelenga watu wenye nguvu kubwa! Kumbuka hapa JF wadau ni watu aina zote kielimu na kikipato. Usilalamike maana hapa JF kuna watu wananguvu kubwa kifedha nao wanahaki na wanahitaji mawazo na ili wasonge mbele! Kumbuka kuna watu wengi ambao hata huu mradi bado kwao ni mradi chamtoto tu!

Kwa hiyo Mkuu kama watu watavutiwa na wazo hilo la kushirikiana wanaweza kuliboresha na kulifaya kulingana na mazingira yao, uwezo wao, na rasilimali zao, si lazima iwe scale kubwa hivyo na si lazima iwe ni kilimo tu na si lazima iwe ni kutumia pesa bali kwa wasio na pesa wanaweza kuanza na mambo mengi yasiyohitaji mtaji wa pesa.

Siri kubwa kwa wasomi wote waliobaki wakizunguka mijini na vibahasha popote mtakapo soma post hii, kama mtu amekaa anasubiri apate mtaji ndiyo aanze shughuri na atakaa sana!! Mtaji wa masikini ni nguvu zake, na mtaji wa msomi ni nguvu zake na elimu yake! Let us think and grow rich! Uvivu wa kufikiri ndiyo unaofanya watu wasubiri mitaji! Think think!! Kunamengi ya kufanya yasiyohitaji mtaji wa pesa, then ukipata pesa kidogo let it grow ili ufike unapotaka, wewe unataka upate limtaji siku moja halafu uanze kuzoa mapesa ghafla kesho yake?! Mkuu Chasha popote ulipo naomba ujazie hapa nilipoishia ili wenye kupenda ukweli, ukweli utawaweka huru!
 

It can be done mkuu Wilshere! So count me in niko interested mazima. Tena hilo tractor tunaweza hata kuagiza kupunguza gharama kwani hayana kodi. Nina uzoefu kidogo kwenye kuagiza hivyo vyuma. Nakupm
 
Napenda kuwakumbusha kitu kimoja kuwa kwa Trecta jipya hekari 300 -400 ni kazi ya siku 10-15. Na msimu wa kilimo unachukuwa siku 60 miezi miwili kwa maeneo ambayo nimeyalenga. Hao watu 8 watakakuwa wanamiliki hilo trecta wanaweza kuwalimia mashamba wadau wengine kwa kuwakodishia wale ambao uwezo wao ni mdogo wanaweza kujiunga 3,5,7 hata 10 wakalima hata hekari 30,40,50........... kwakuchangishana kiasi cha pesa.
 
Good idea. Mimi ni gwiji wa precision agriculture. Just pm in case unahitaji ufundi zaidi.
 
Kwa walio tayari tukutane tarehe 22/06/2013 jmosi eli tuanzi kufanya vikao na kushauriana jinsi ya kufanya huo mradi ni vizuri tukafahamiana vizuri . Kwahiyo wadau pangini muda mzuri wa kukutana na venue itakuwa wapi ni vizuri venue ikawa sehemu ambayo inafikika kwa urahisi kwa wote hapa dsm . Mimi binafsi nipo free kuanzia saa 8 mchana hadi saa 4 uciku 0765616178
 
Wakuu napendekeza jmosi 22.06.2013 kikao chetu tufanyie MANZESE hapo ndio penye soko la mahindi eli tukimaliza tufanye simple suvery kwani maeneo hayo ndio centre ya wakulima na wafanya biashara ya mahindi wanapokutania, eli tuwenze upata infor nyingi kwa watu mbalimbali piya mkajionea watu wanavyoshika mamilioni kirahisi tu. 0765616178
 
Wakuu napendekeza jmosi 22.06.2013 kikao chetu tufanyie MANZESE hapo ndio penye soko la mahindi eli tukimaliza tufanye simple suvery kwani maeneo hayo ndio centre ya wakulima na wafanya biashara ya mahindi wanapokutania, eli tuwenze upata infor nyingi kwa watu mbalimbali piya mkajionea watu wanavyoshika mamilioni kirahisi tu. 0765616178
 
ni wazo zuri na linalotekelezeka, cha msingi ni kuwa na mpango madhubuti. mabilionea wa baadae watatokea kwenye kilimo na chakula.
 
ni vizur pia wandugu kuhusu ufuta na mtama lindi kama sehem bora ya mazao haya naweza toa ushauri wa maeneo mazur kabisa
 
Niko interested sana na kilimo cha vitunguu! Wadau wangu nipeni muongozo wa hili!
Natamani sana kuwemo, kikwazo ni kwamba, kwa sasa nina project moja kubwa na inapanuka kila siku,na hata wilshere anafahamu ninachosema.
 
Niko interested sana na kilimo cha vitunguu! Wadau wangu nipeni muongozo wa hili!

Uko tayari nikuunganishe na jamaa aliyewahi kulima kitunguu pale Ruaha Mbuyuni Iringa?
 
Uko tayari nikuunganishe na jamaa aliyewahi kulima kitunguu pale Ruaha Mbuyuni Iringa?

Mkuu malila heshima kwakobado nafanya feasibility study kama vipi naomba uniunganishe na huyo jamaa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…