Kwa waliokojoa kitandani tu!!

Kawaida yake, mbwa ukimjua jina hakusumbi.
Aisee binti unanini na mimi ?

Si mara moja si mara mbili nakuona nikipishana kauli kidogo na watu unakuja mbio mbio kutema shombo zako.

Aisee tusizoeane hivyo kwa kweli.
 
Kwani madume ndio walikojoa tu, mbona picha moja hapo ya me, ke siion?
 
Miaka miwili? Kweli unamaanisha mtoto akifikisha miaka miwili anaacha kujikojolea? Hivi pampers mwisho miaka mingapi na kwanini?

Kwa kukufahamisha kujikojolea usingizini kwa watoto mara nyingi inasababishwa na uchovu, unalala hoi sana. Huoni kila mtu kisa chake ni ndoto?
 
Binti yangu wa kwanza aliacha kukojoa akiwa na miaka miwili na nusu.
 
daaaaa weee jamaa umenikumbusha mbali nakumbuka, Mama alinikuwa ananichapa sana mara kila siku ilikuwa ni lazima niumwage wa kutosha, sasa siku moja mama akaniambia nikikojoa navalishwa manguo na kuimbiwa kindumbwe ndumbwe, usiku huo si nikalimwaga kama saa tisa hivi nikashtuka eebwana nilihangaika usiku kucha nikiwaza kitakachonikuta asubuhi. ilipofika asubuhi nikavalishwa manguo yaliyochakaa, namshukuru marehemu bibi yangu alikuja akamgombesha sana mama kwa tabia hiyo, yaani nilipata tabu sana maana sikuacha mpaka nilipofika darasa la nne nakumbuka ndoo nikawa nakojoa mara moja moja
 
Nilikojoa nikiwa mtoto mpk darasa la sita. Sasa hilo suala linamuathiri vipi sasa hivi mimi nina miaka 40 na sikojoi tena kitandani?
Ni kama sikuelewi vile
Kwanini unapenda kubishana na watoto?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…